Usilolijua kuhusu Mapenzi/Mahusiano, hisia za mapenzi kwa ujumla

j wa nmb

Senior Member
Jul 28, 2020
174
415
Mahusiano ni kama Gari la masafa marefu, Tena lenye linapitia barabara yenye mashimo, milima na mabonde.

Inabidi muda wote ucheze na usukani, ukilala tu utajikuta ulisha acha barabara mda mrefu ulio pita na unaelekea shimoni. Hii ikiwa na maana usijisahau, kumbuka hisia zinapotea kutokana na changamoto mbali mbali, Usiisahau misingi iliyo wajenga.

Tengeneza mvuto muwapo pendoni, akumiss kidogo, ajue umuhimu wako ukiwa haupo, mpe mitihani fulani flani ya kuiweka roho juu,ajue wew ni ghali na thamani yako ni kubwa (hapa uwe na kiasi, na umakini kwa misuko suko midogo midogo unayo mpatia). Kwasababu Mapenzi ni sanaa, kumbuka binadam yeyote hupenda zaidi kile kitu anacho kisumbukia, kila mtu hupenda kile kitu ambacho si rahisi kukipata.

Baada ya misuko suko midogo dogo, mpatie good time ahisi uwepo wako na amani moyoni mwake.

Mfano mdogo, chukulia umeme unavyo katika, unaudhika sana lakini baada ya mda umeme unapo rudi, unahisi raha sana tofauti hata na pale ulivyo kuwa upo nao mwanzo.

Habari za mpenzi wangu sijui anasema hana feeling na mimi tena utaishia kuzisoma tuu hapa JF.

Though Mpenzi wangu kanichunia leo siku ya 5, but i hope i will make it again, hatakama itakuwa baadae sana.
 
Nimeelewa hapa zaidi

bebe kumbe tunafanana ila me mekuzidi leo siku ya sita[/QUOTE]Njooni kwangu, nami nitawapumzisha...
[/QUOTE]
Mkuu unaleta masiara unajua ni kiasi gani moyo unauma ukiona jua linazama bila ya kuona calls wala text kutoka upande wa pili
 
acha tu dada mkubwa,kila sms ikiingia nnahisi niyeye kumbe ni huduma za kimtandao 😭
 
Back
Top Bottom