Faida za kufanya tendo la ndoa (kujamiiana) kwa wanandoa

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Faida za kujamiiana

1.Kuwa na mpenzi ambaye ni rafiki yako ni jambo zuri sana katika mahusiano. Kuwa katika mahusiano pasipo kufanya mapenzi na mwenza wako ni kama tu kuwa na rafiki yako. Mahusiano hujawa na uchu, wapenzi hutaka furaha na kuridhika. hivyo kufanya mapenzi na mwenza wako huchochea hisia nzito baina yenu, huburudisha na kuyafanya mahusiano kuwa bora.

2.Kufanya mapenzi husaidia kuondoa mawazo. ufanyapo mapenzi homoni zinazokupa furaha hutengenezwa kwa wingi wilini. Kumbuka unapokuwa na furaha ndivyo unavyoweza kufanya kazi kwa ufanisi.

3.Kufanya mapenzi hukufanya ulale usingizi mzuri. Siyo kwa sababu ya uchovu wa shughuli nzito mliyoifanya. Unapomaliza kufanya mapenzi kemikali iitwayo ‘oxytocin’ huachiwa na mwili. Hii hukufanya kulala usingizi mzuri na wa raha.

4.Wanawake ambao hufika kilele ( orgasm ) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi.

5.Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.

6.Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo ( brain stem cells ) kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa na kutambua harufu brain olfactory bulb.

7.Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini : Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.

8. Husaidia kuimalisha kinga ya mwili.

9. Husaidia kupunguza uzito na unene kwa sababu ni zoezi tosha.

10. Hupunguza uwezekano wa kupata kansa zisizo eleweka.

FB_IMG_16329771787432651.jpg
======

Kwa maoni zaidi soma>>> Faida 17 za kufanya mapenzi salama
 
Sasa kwa sisi ambao ni singo bati meridi hizi faida tutaishia kuzisoma humu JF.

Asante kwa madini mleta uzi,

Tendo la ndoa kwa wanandoa ni muhimu. hususan linapofanywa kwa furaha kati yenu wote wawili.......huleta pia closure(wenye kiinglish chenu rekebisheni) kwa wanandoa
 
Kusex na mke wako wa ndoa kunakufanya upate baraka nyingi sana kutoka kwa mwenyezi Mungu
Kusex nje ya ndo unapata mikosi mingi sana
1. Mnabadilishana nafsi na kuna uwezekano mkubwa wa kupata mikosi mingi katika maisha ikiwa ya kiuchumi, kijamii nk.
2. Sperm kwenda katika njia ya kishetani ni kafara kubwa sana inafuatia kutoka ile ya kuua mtu. kafara hiyo hutumika na wengine ktk kufanikisha biashara au kazi zao
 
Back
Top Bottom