Usikubali kutoka hapo ulipoajiriwa jinsi ulivyoingia

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Wakuu habari?

Nimekuwa mtu wa kutoa comments sana na kuanzisha threads kutegemeana na uhitaji wangu. Ila nimeona ni wakati muafaka kuanza ku-share kile nilichojaaliwa na Mungu.

Twende kwenye point ya msingi. Ipo hivi, wewe uliyeajiriwa kwenye hiyo kampuni usikubali kutoka hapo jinsi ulivyoingia.

Katika kampuni yoyote ukiwepo jifunze jinsi gani inavyofanya kazi na wahusika wamewezaje kusimamisha hiyo kampuni mpaka kufika hapo ilipo. Hapa nazungumza na wewe mwenye lengo la kuja kuacha kazi ili kujiajiri, au wewe ambaye hutopenda mwanao kupitia mfumo ambao ulipitia katika harakati za utafutaji.

Ni kweli kuna watu wa aina tofauti, yupo anayefanya kazi fulani kwasababu ya kupata pesa ila wapo waliopo sehemu fulani ili kujifunza jinsi gani ya kutengeneza pesa.

Jitahidi kuingia katika kundi hili la pili. Usiwe sehemu fulani kwa lengo la kupata pesa, ila kuwa sehemu hiyo kwa lengo la kujifunza jinsi ya kutengeneza pesa.

Ukiona wewe ofisini ni kushughulika tu na majukumu yako tu unayokabidhiwa na ukishamaliza ndo imetoka, aisee unakosea.

Acha tabia ya kuijua kampuni ili usifeli interview. Fuatailia misingi ya kampuni, ujue ilianza vipi na nani, na ilikuaje mpaka ikawa hivi. Kutokana na ufuatiliaji huo unaweza gundua vitu vingi vya msingi ambavyo vinaweza kusaidia kuanzisha jambo lako na kufanikiwa pia.

Siyo jambo jepesi, lakini unapokuwa ofisi yoyote, jifunze na kuielewa kampuni husika, utajikuta una knowledge pana sana na unaweza kuwa msaada kwa wewe mwenyewe au hata kwa kizazi kingine pia.

Usikae kutumika tu.

Karibu tujadili.
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Naona unakaribia kustaafu.
Bado sana mkuu. Am still young na ndiyo kwanza na hustle.

Hii kitu nimekuja igundua nikiwa field chuo. Nimekutana na wengi wafanyakazi na nimejifunza mengi kwa wale ambao walikuwa wazi kunieleza ukweli.

Kuna kampuni moja hapa DSM (sitotaja jina) nimekutana na production manager ana miaka zaidi ya thelathini kwenye ajira na kazi ni hiyohiyo anayoifanya miaka yote. Ni mzee ambaye tuliendana na aliona nina nia ya kujifunza vitu hivyo aliniambia ukweli bila kujali nyadhifa na umri wake.

Kiufupi miaka hiyo yote yupo kazini hajawahi ona utofauti katika maisha yake, furaha yake, uchumi na hata mahusiano yake kijamii na yote kwasababu ya ajira yake, japo wengi walikuwa wanamuheshimu sana kutokana na uzoefu wake na ujuzi aliokuwa nao.

Aliongea mengi sana ya kusikitisha, na ndiye aliyenipa hilo wazo.

Sikumuelewa mwanzo ila kwasasa nimeweza kumuelewa vema.

Umeajiriwa, fanya juu chini usiwepo kwenye kampuni kwasababu ya pesa ya kula na kuishi. Kuwepo pale kupata mbinu na namna bora za kutengeneza pesa.

Jitume sana ujenge uaminifu wa kutosha.

Kuna wengine makazini kwao bila wao kazi haziendi, ila mpka hapo hawajagundua uwezo walio nao na waanzishe chao.

Wewe haupo kazi hazifanyiki, unategemewa wewe tu, na ukitaka kuacha kazi boss anakuomba tena hata kwa kukuongezea mshahara, ila bado tu hujagundua thamani yako na uwezo ulionao. Shtuka mapema, tayari unao uwezo wa kutosha kuanzisha chako ndiyo maana bosi anakubembeleza.
 
Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
2,271
2,000
Bado sana mkuu. Am still young na ndiyo kwanza na hustle.

Hii kitu nimekuja igundua nikiwa field chuo 2017 na 2018. Nimekutana na wengi wafanyakazi na nimejifunza mengi kwa wale ambao walikuwa wazi kunieleza ukweli....
Sasa mwalimu wa Biology atajifunzaje hayo ikiwa yeye haajiriwi kwenye kampuni bali shule tu kibaha ndanindani huko.
 
kissa anyigulile

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
727
1,000
Bado sana mkuu. Am still young na ndiyo kwanza na hustle.

Hii kitu nimekuja igundua nikiwa field chuo 2017 na 2018. Nimekutana na wengi wafanyakazi na nimejifunza mengi kwa wale ambao walikuwa wazi kunieleza ukweli...

Nimekuelewa vuzuri sana.

Sasa naomba nikupe ushauri mmoja. Hata siku moja huwezi ukayalazimisha maji yapande mlima.

Kama una ajira ya kudumu (permanent pensionable), tulia, fanya kazi.

Najua, sehemu nyingi kupata promotion is an issue. Tulia fanya kazi zote kwa weledi bila kinyongo, na mambo ya promotion yape kama added advantage.

Usipende sana kuangalia angalia mafanikio ya wenzako. Mshukuru Mungu kwa ule mkate wako wa kila siku anaokupatia.
Ishi maisha ya low profile, usipende makubwa. Achana na kutaka watu wakuone, live as you and not like John.
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Sasa mwalimu wa Biology atajifunzaje hayo ikiwa yeye haajiriwi kwenye kampuni bali shule tu kibaha ndanindani huko.
Pia kuna fursa huko mkuu. Kama ana nia anaweza jifunza utaratibu wa kuendesha taasisi ya elimu kama shule na akaweza kuanzisha shule yake. Mfano mwalimu unafundisha miaka mitatu au minne kutegemeana na uwepesi wako wa kuelewa vitu na kufanya pia, baada ya hapo anarudi kutengeneza mazingira ya kuanza hata na tuition center, taratibu anahama na kuanzisha darasa moja, madarasa mawili baada ya hapo shule anaanza kuiona.

Siyo rahisi jinsi ninavyoeleza tu hivyo , kuna ups and down nyingi ambazo zitahitaji uvumilivu na jitihada za kutosha.

Na kama akiwa na nia kweli basi atafikia malengo.
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Field mwaka 2017-2018? bado kijana sana lakini umetema madini ya kiutu uzima umenifanya nifikirie upya hapa kibaruani kwangu, kongore kwako.
Shukrani mkuu. Ukiwa na malengo fulani katika maisha umri huwa ni namba tu boss, ila hekima ndiyo huwa kila kitu
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Nimekuelewa vuzuri sana.
Sasa naomba nikupe ushauri mmoja. Hata siku moja huwezi ukayalazimisha maji yapande mlima...
Asante sana mkuu. Ni kweli tusiishi kwa kuangalia wengine, lakini pia tusisahu KUJIFUNZA kupitia wao ili kuepuka kupita njia ambayo waliipita.

Zaidi ya yote ni kumuomba Mungu akupe hekima na busara kufikia yale malengo unayoyaamini.
 
Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
2,271
2,000
Pia kuna fursa huko mkuu. Kama ana nia anaweza jifunza utaratibu wa kuendesha taasisi ya elimu kama shule na akaweza kuanzisha shule yake. Mfano mwalimu unafundisha miaka mitatu au minne kutegemeana na uwepesi wako wa kuelewa vitu na kufanya pia, baada ya hapo anarudi kutengeneza mazingira ya kuanza hata na tuition center, taratibu anahama na kuanzisha darasa moja, madarasa mawili baada ya hapo shule anaanza kuiona...
Huoni tatizo hapo

Yaani mwalimu anakuwa kwenye Box la kujifunza kuanzisha shule yake tu.

Lakini Carrier kama muhasibu anaweza ajiriwa kampuni yeyote ile ya Logistics, Mining, Heath, Technology...Hana Box anapata Knowledge ya kuanzisha any kind of Company inayodili na chochote kile na kuwa na knowledge pana jinsi ya kuwa manage Officers mbalimbali HR, Wahasibu, Marketing department nk nk kwasababu hivi ni vitu common kwenye masuala ya kampuni ambapo most Accountant wanakula shavu huko.

sasa huyu mwalimu yeye shavu lake anakula Mtombo Sec kibaha buyuni huko hawi experienced na shughuri zozote za kikampuni HR, Marketing team nk Shule nyingi hazina hizi ishu.

Sijui umenielewa ila kimsingi Carrier kama uwalimu changamoto sana.
 
Mkuu usiwafunge waalimu, nao wana fursa kama ilivyo kwenye field zingine.

Unapojifunza kitu tunategemea ukatumie knowledge yako sasa kutegemeana na kile ulichojifunza ili kupata unachokitaka.

Unaposoma kitabu na kukimaliza kitabu hucho huwa hakihitajiki tena na kinachobaki kichwani ndiyo kinachohitajika (knowledge) ili kuingia katika utendaji.

Sikuwa na maana kuwa ni lazima ukaanzishe aina ya kampuni uliyopo kwasababu umejifunza namna ya utendaji kupitia kampuni hiyo.

Knowledge unayoipata unaweza kuitumia kuanzisha chochote kile ilimradi uwe na nia ya dhati kufanya hicho unachotaka kukifanya. Pia kumbuka huwezi jifunza kupitia kampuni moja na ukafanikiwa kila kitu.

Lazima ujue unataka nini? Na kwenye kampuni hii nitapata nini? Lakini pia ujue nini utahitaji na hakipatikani katika kampuni hii? Na lazima ujue wapi au kwa nani naweza kupata kitu hicho?

Mwalimu kupitia ofisi yake kuna taratibu za jumla ambazo anaweza kuelewa na ikamsaidia, kwa mfano uelewa juu ya taratibu za ulipaji mshahara kwa wafanyakazi, sheria zinazotumika kuanzisha taasisi binafsi hasa shule, haki za msingi za mfanyakazi na mengine pia.

Turudi kwenye suala la mwalimu kutokuwa na uwezo wa kuanzisha kampuni zingine tofauti na shule, hili jambo siyo kweli.

Engineer anaweza Fanya kazi kwenye kampuni ya magari na yeye siyo kwamba kile atakachojifunza pale ndicho atakachohitaji ili kuanzisha kampuni yake. Kuna masuala ya sheria hili halichagui mwalimu wala doctor ni lazima kufuata sheria hitajika ili uweze kufanya shughuli husika.

Hivyo niseme tu, kila mmoja katika kampuni husika ana nafasi ya kujifunza namna ya uendeshaji na background ya kampuni husika SIYO kwa lengo la kuandaa kampuni kama hiyo, hapana. Ila kwa lengo la kupata uelewa wa namna jinsi watu wanavyoanza mpaka kufanikiwa sasa kuanzia hapo unaweza amua nianzishe kampuni kama hiyo au nyingine tofauti.

Lakini faida inakuja kiujumla kuwa unayo basic knowledge ya uendeshaji wa biashara, tahisisi au kampuni ya aina fulani kwasababu umekuwa sehemu ya kampuni hiyo na umeshuhudia na kujifunza.

Dhana ya waalimu kuwa na uwanja mdogo siyo kweli. Wapo watu kama akina MSUKUMA wanamiliki kampuni za mabasi na ni darasa la saba, inakuaje wewe mtu was degree unalalamikia field yako?

Hapo ndipo nguvu ya mtazamo inapokuja kuwa na athari katika maisha yako kiujumla na kujitengenezea dhana kuwa haiwezekani na kweli haitowezekana.
 
Date20210317

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
3,860
2,000
Huu pia ni ukweli. Na ni uamuzi wa mtu mwenyewe apindue meza au aendelee kuvumilia, maana ni kweli kupindua meza siyo kazi ndogo. Ndiyo maana wapo risk takers wachache wenye ubavu wa kuamua.
Kabisaa. Nilipindua meza ila katika kupambana kuna time unataman kama upindue tena meza irud kama awali 😂😂😂
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Kabisaa. Nilipindua meza ila katika kupambana kuna time unataman kama upindue tena meza irud kama awali
Ni kweli mkuu, kuna moments ambazo unaweza jilaumu kwanini ulifanya maamuzi hayo. Ila nyakati ngumu huwa hazidumu milele na ni sehemu ya kukuamsha kifikra kutafuta majibu ya wapi nimekosea.

Nakumbuka kuna mwalimu wangu wa kiingereza primary alishawahi niambia

"Mr. Purpose, katika maisha yako hakuna maamuzi ambayo hutokaa bila kujuta kwanini uliamua, yawe ni maamuzi mazuri au mabaya, lazima kuna siku utayajutia"

Ila kikubwa ni msimamo na kujitoa hata wakati wa nyakati ngumu uwe imara kuendelea kusimamia kile unachokiamini.
 
Well said
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,480
2,000
Nimekuelewa vuzuri sana.

Sasa naomba nikupe ushauri mmoja. Hata siku moja huwezi ukayalazimisha maji yapande mlima.

Kama una ajira ya kudumu (permanent pensionable), tulia, fanya kazi.

Najua, sehemu nyingi kupata promotion is an issue. Tulia fanya kazi zote kwa weledi bila kinyongo, na mambo ya promotion yape kama added advantage.

Usipende sana kuangalia angalia mafanikio ya wenzako. Mshukuru Mungu kwa ule mkate wako wa kila siku anaokupatia.
Ishi maisha ya low profile, usipende makubwa. Achana na kutaka watu wakuone, live as you and not like John.
Kasome career development theory, umachana na ushauri was kubaki stagnant.Career theories zinapingana na ushauri wako.
 
kissa anyigulile

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
727
1,000
Kasome career development theory, umachana na ushauri was kubaki stagnant.Career theories zinapingana na ushauri wako.
Kasome career development theory, umachana na ushauri was kubaki stagnant.Career theories zinapingana na ushauri wako.
"Career development theory" I am interested in the word "theory".
About 95% of the theories cannot be practiced. Remember Darwin's theories. They are known as "utopian" theories.
Never rely on theories, you will end cramming steps and ultimately a total collapse.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom