Usikubali kutoka hapo ulipoajiriwa jinsi ulivyoingia

Bado sana mkuu. Am still young na ndiyo kwanza na hustle.

Hii kitu nimekuja igundua nikiwa field chuo. Nimekutana na wengi wafanyakazi na nimejifunza mengi kwa wale ambao walikuwa wazi kunieleza ukweli.

Kuna kampuni moja hapa DSM (sitotaja jina) nimekutana na production manager ana miaka zaidi ya thelathini kwenye ajira na kazi ni hiyohiyo anayoifanya miaka yote. Ni mzee ambaye tuliendana na aliona nina nia ya kujifunza vitu hivyo aliniambia ukweli bila kujali nyadhifa na umri wake.

Kiufupi miaka hiyo yote yupo kazini hajawahi ona utofauti katika maisha yake, furaha yake, uchumi na hata mahusiano yake kijamii na yote kwasababu ya ajira yake, japo wengi walikuwa wanamuheshimu sana kutokana na uzoefu wake na ujuzi aliokuwa nao.

Aliongea mengi sana ya kusikitisha, na ndiye aliyenipa hilo wazo.

Sikumuelewa mwanzo ila kwasasa nimeweza kumuelewa vema.

Umeajiriwa, fanya juu chini usiwepo kwenye kampuni kwasababu ya pesa ya kula na kuishi. Kuwepo pale kupata mbinu na namna bora za kutengeneza pesa.

Jitume sana ujenge uaminifu wa kutosha.

Kuna wengine makazini kwao bila wao kazi haziendi, ila mpka hapo hawajagundua uwezo walio nao na waanzishe chao.

Wewe haupo kazi hazifanyiki, unategemewa wewe tu, na ukitaka kuacha kazi boss anakuomba tena hata kwa kukuongezea mshahara, ila bado tu hujagundua thamani yako na uwezo ulionao. Shtuka mapema, tayari unao uwezo wa kutosha kuanzisha chako ndiyo maana bosi anakubembeleza.
Hizi point umezi cement vyemaa....

Jitume sana ujenge uaminifu wa kutosha.

"Kuna wengine makazini kwao bila wao kazi haziendi, ila mpka hapo hawajagundua uwezo walio nao na waanzishe chao.

Wewe haupo kazi hazifanyiki, unategemewa wewe tu, na ukitaka kuacha kazi boss anakuomba tena hata kwa kukuongezea mshahara, ila bado tu hujagundua thamani yako na uwezo ulionao. Shtuka mapema, tayari unao uwezo wa kutosha kuanzisha chako ndiyo maana bosi anakubembeleza"

Ulicho zungumza Ni ukwel ulio uchi....

Nina mengi ya kuwa ambia vijana......Mwaka huu mwezi wa December niliwahaidi na naendelea ku ahidi...... inshallah

Hizo point zako nimezifanyia research.....zipo valid

Aluta continue Kwa VIJANA wote wanao make it happen...
 
Ulimwengu unabadilika mkuu, inabidi kwasasa kila mmoja amuone mwingine kama fursa.

Muajiri aonekane fursa kutokan na uelewa alionao na experience yake mpaka kusimamisha kampuni.

Muajiri aone fursa ya wewe kumfanyia kazi ili kampuni izidi kukua.

Tusikae kulipwa mishaara tu kisha kustaafu au kufukuzwa kazi bila kutoka na chochote cha ziada.
 
Back
Top Bottom