Mr. Purpose
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 1,439
- 2,690
Wakuu habari?
Nimekuwa mtu wa kutoa comments sana na kuanzisha threads kutegemeana na uhitaji wangu. Ila nimeona ni wakati muafaka kuanza ku-share kile nilichojaaliwa na Mungu.
Twende kwenye point ya msingi. Ipo hivi, wewe uliyeajiriwa kwenye hiyo kampuni usikubali kutoka hapo jinsi ulivyoingia.
Katika kampuni yoyote ukiwepo jifunze jinsi gani inavyofanya kazi na wahusika wamewezaje kusimamisha hiyo kampuni mpaka kufika hapo ilipo. Hapa nazungumza na wewe mwenye lengo la kuja kuacha kazi ili kujiajiri, au wewe ambaye hutopenda mwanao kupitia mfumo ambao ulipitia katika harakati za utafutaji.
Ni kweli kuna watu wa aina tofauti, yupo anayefanya kazi fulani kwasababu ya kupata pesa ila wapo waliopo sehemu fulani ili kujifunza jinsi gani ya kutengeneza pesa.
Jitahidi kuingia katika kundi hili la pili. Usiwe sehemu fulani kwa lengo la kupata pesa, ila kuwa sehemu hiyo kwa lengo la kujifunza jinsi ya kutengeneza pesa.
Ukiona wewe ofisini ni kushughulika tu na majukumu yako tu unayokabidhiwa na ukishamaliza ndo imetoka, aisee unakosea.
Acha tabia ya kuijua kampuni ili usifeli interview. Fuatailia misingi ya kampuni, ujue ilianza vipi na nani, na ilikuaje mpaka ikawa hivi. Kutokana na ufuatiliaji huo unaweza gundua vitu vingi vya msingi ambavyo vinaweza kusaidia kuanzisha jambo lako na kufanikiwa pia.
Siyo jambo jepesi, lakini unapokuwa ofisi yoyote, jifunze na kuielewa kampuni husika, utajikuta una knowledge pana sana na unaweza kuwa msaada kwa wewe mwenyewe au hata kwa kizazi kingine pia.
Usikae kutumika tu.
Karibu tujadili.