Fbn
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 15,749
- 37,422
Sababu zenyewe ni hizi hapa zitakazokufanya usionewe
Askari akikuomba Rushwa mkamate mpeleke TAKUKURU - Kangi Lugola Waziri wa Mambo ya Ndani.
-
1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
-
2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
-
3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
-
4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
-
5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
-
6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
-
7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
-
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
-
9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
-
10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
-
11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
-
12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
-
13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
-
14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
-
15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
-
16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
-
17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
-
18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
-
19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
-
20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
-
21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
-
22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
-
Waambie na wengine wasio wana jf
soldier
hayo unayo sema mpaka ya timie utajikuta mwochwari au kesi utakayo pewa kuja kutoka si leo