Usikubali kuonewa na Askari yeyote yule

Usikubali kuonewa na Askari yeyote yule

SMART PASSENGER

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
1,361
Reaction score
2,139
Sababu zenyewe ni hizi hapa zitakazokufanya usionewe

Askari akikuomba Rushwa mkamate mpeleke TAKUKURU - Kangi Lugola Waziri wa Mambo ya Ndani.
-
1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
-
2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
-
3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
-
4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
-
5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
-
6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
-
7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
-
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
-
9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
-
10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
-
11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
-
12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
-
13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
-
14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
-
15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
-
16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
-
17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
-
18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
-
19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
-
20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
-
21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
-
22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
-
Waambie na wengine wasio wana jf

soldier
 
Kwa nchi hii ambayo askari anaua mchana kweupe ndani ya kituo cha polisi na Waziri wa mambo ya ndani anasema ni kawaida raia kufia polisi kama ilivyo kufia guest, hospital n.k usitarajie sharia kuheshimiwa

Askari wa kibongo hawatumiagi akili kwenye utendaji kazi wao zaidi ya misuli
 
Ijapokuwa umeandika 'askali' ila ngoja nikubaliane nawe huenda ulitaka kuandika neno 'askari'.

Icho kipengele no 12 nashauri wangekifanyia marekebisho au kifutwe mazima.
 
Raisi aliwahi kutamka akiwa ziarani huko kwao kuwa serikali yake inakomesha kabisa mtu kumtukana na kumdharau mtu mwingine kwasababu ya cheo chako au mali yako. daaaalakini najua mheshimiwa sana Makondakta mara nnyingi tu amekuwa akiwatukana watu haddharani tena waliomzidi umri. Utamsikia kkichaa mwingine huyu mbele ya media ambayo inasikilizwa mpaka na watoto wa muhanga jamaniii halafu hachukuliwi hatua mmmh nasema hivi MANENO YAO HAWA WATAKATIFU USIJE UKAYAAMINI HATA SIKU MOJA YATAKUJA KUKULETEA SHIDA
 
Utakubali vp kuonewa
tapatalk_1536381753382.jpeg
 
Kwa nchi hii ambayo askari anaua mchana kweupe ndani ya kituo cha polisi na Waziri wa mambo ya ndani anasema ni kawaida raia kufia polisi kama ilivyo kufia guest, hospital n.k usitarajie sharia kuheshimiwa

Askari wa kibongo hawatumiagi akili kwenye utendaji kazi wao zaidi ya misuli
Askari wa kibongo hawatumiagi akili kwenye utendaji kazi wao zaidi ya misuli.

Hii ilinisaidia sana, nilikuwaga na kesi,

baada ya kukamatwa wakakusanya ushaidi kwa nguvu mno! Wakapata ushaidi mzito sana!

Pamoja na vitu vingine walipata video ya tukio.

Niliweka wakili...kesi ilikuwa ngumu sana"

Baada ya kuwasilisha ushaidi wao wote
Tukaanzisha kesi ndogo ya kukataa ushaidi wao wote! Kwamba hawakufuata sheria ktk kukusanya ushaidi. Pamoja na kukata.

Hukumu ilivotoka wakashinda wao na hivo Hakim akaamua kesi ya msingi iendelee"

Mwisho wa kesi nilishinda kwa kukataa kwamba ushaidi waliouleta hauhusiani na Mimi na hivo vitu sio vyakwangu!

Walishindwa kuthibitisha kwamba vitu vilikuwa vyangu kwa sababu ktk ukamataji na ukusanyaji wa ushaidi hawakufuata sheria. Nikashinda!!"
 
Pole sana mkuu na hongera sana kwa kuwashinda hao jamaa walinda usalama wa raia na mali zao waliogeuka kufanya kazi kinyume na wajibu wa majukumu yao
 
aiseeeeeeeh hujanishawishi kabisa askari wa kibongo usijifanye unajua sana sheria mambo hayo labda ulaya sio tz
Tena askari wa kibongo wanaumoja uliopitiliza. Maana ukimletea ujuaji mmoja watakuchenjia kikosi kizima na watakupa tuhuma usiozitegemea.
Kumbuka wao wana mamlaka makubwa ikiwemo kupeleleza kosa na kuwa waendesha mashtaka.
 
Mkuu mleta uzi unaishi bongo kweli? Nna wasiwasi unaishi Marekani na utakuwa unaongelea Police wa huko maana huku sisi tuna maafande na hatuna kabisa hao ulowaongelea hapa.
 
Sababu zenyewe ni hizi hapa zitakazokufanya usionewe

Askari akikuomba Rushwa mkamate mpeleke TAKUKURU - Kangi Lugola Waziri wa Mambo ya Ndani.
-
1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
-
2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
-
3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
-
4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
-
5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
-
6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
-
7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
-
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
-
9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
-
10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
-
11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
-
12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
-
13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
-
14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
-
15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
-
16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
-
17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
-
18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
-
19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
-
20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
-
21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
-
22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
-
Waambie na wengine wasio wana jf

soldier
Hiki ni kinyume chake
 
Mleta uzi umeshindwa kutoa ufafanuzi wa haki huku ukihusisha ukweli wa taifa la Tanzania Hapo ukijiloga Kufuata sheria hizi unakifa faster polisi wanalindwa zaidi nchi hii na wanatetewa kwa kila aina ya uovu wanaoufanya
 
Back
Top Bottom