Usikubali kubadili dini kisa mwanamke, mara nyinyi shetani huwatumia wanawake kukutenga na Mungu

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,640
4,426
Siku moja baba yangu aliniita,akanikalisha chini na kuanza kunisimulia hadithi hii; alianza hivi>
"Mwanangu kipindi mimi bado kijana,nilitokea kumpenda sana binti mmoja mzuri na mwenye kupendeza,ila nilivyomwambia kama nampenda alinikubalia kirahisi sana na kusema kuwa hata mimi alikuwa ananipenda tangu mwanzo ila alishindwa kusema tu.

Lakini alinipatia mashariti ya kuwa nae,alidai kuwa kama nataka kuanzisha mahusiano na yeye lazima kwanza nisilimu niwe muislamu,nilipoleta ubishi kuhusu kubadili dini alinikatalia kufanya nae chochote mpaka pale nitakapokubali kuwa muislamu. Kwa kuwa alikuwa mzuri na wakuvutia sikuweza kumuachia aondoke hivi hivi, bali nilibuni njia ya kumnasa kirahisi. Niliazima kanzu na kibaragashia kwa rafiki yangu, kisha ijumaa nikaenda msikitini katika msikiti aliyokuwa akiswali na yeye, nilivyofika msikitini sikuweza kuingia ndani ya msikiti ila nilibaki nje na kupanda juu ya mti wa mwembe nikisubiri wamalize kuswali.

Baada ya kumaliza kuswali na mimi niliteremka taratibu na kujichanganya na wenzangu na kuanza kushikana nao mikono huku nikiwa kama mtu aliyemaliza kuswali. Nikaanza kuelekea kule kwa wanawake nikitafuta kujionyesha kwa msichana yule ili ajue kuwa nimekubali kuwa muislamu, sikuamini msichana yule alivyofanikiwa kuniona!!!!!alifurahia sana siku hiyo na kusema kuwa jioni hiyo tungekuwa pamoja"

Sasa mimi nikamuuliza baba,kama unadai binti alikuwa mzuri na wa kupendeza kwanini ulimdanganya kwa kupanda juu ya mti wakati ulimpenda?kwanini usingerudi kuwa muislamu ili uupe moyo wako furaha?

Baba alinijibu kuwa;mwanangu wewe bado kijana mdogo nimeamua kukusimulia hadithi hii ili ujifunze kitu, katika maisha usikubali hata siku moja kuuza roho yako iende jehanam kwa ajili ya starehe ya usiku mmoja.bali tumia akili kutimiza haja za moyo wako ila usimkane Mungu wako wa kweli.

Nikamuuliza tena baba, unasema nisimkane Mungu wangu kivipi,wakati hata waislamu humuabudu Mungu yule yule.

Baba alicheka sana kisha akaniambia haya;Mwanangu lazima ujue kuwa kitu chochote kizuri, ndio huwa mtego wa shetani kuwakamata watu na kuwatenganisha na Mungu, ukikua utakuja kujua nini maana ya maneno haya. Fikiria kuhusu Eva alivyotumiwa na shetani ili kumgombanisha Adamu na Mungu, pia fikiria Delila alivyotumika na shetani kumgombanisha Samsoni na Mungu. Ndio ujifikirie ni jinsi gani yule binti alivyotaka kunigombanisha na Mungu.

Kwa umri niliyokuwa nao sikuweza kuyaelewa maneno yale ya baba,ila leo nimekuwa nimeyaelewa vizuri sana. Shetani amekuwa akiwatumia wanawake wa kiislamu ili kuwakamata wanaume wenye tamaa.maana ukimtaka tu mwanamke wa kiislamu shariti la kwanza wewe mwanaume ubadili dini na kuwa muislamu ndipo umpate na inapotokea ukakataa, ukamwambia abadili yeye dini basi jua yupo tayari uhusiano wenu ufe ila sio yeye kubadili dini.leo ndio najua kuwa kumbe Baba yangu alikuwa na haki ya kupanda juu ya mti wa mwembe kwa ajili ya mapenzi,ila hakuwa tayari kuwa adui wa Mungu kwa ajili ya mapenzi.
Instagram%20media%20-%20Bfq0E69AlRX.jpg
 
Back
Top Bottom