Usiku wa mauzauza ya CHADEMA

Usiku wa mauzauza ya CHADEMA

Sijapiga kampeni ya aina yoyote.
Hata kama kuna jambo lilimpata mawazo hakuna uhalaliwa kuhalalisha yaliyotokea siha
Kama uliweza kushuhudia uhalifu kisha kuukalia kimya mpaka leo, ukaona wahalifu ukawakalia kimya mpaka leo, basi wewe ulikuwa mmojawapo. Jitokeze uhojiwe
 
Sikumbuki tarehe ila nakumbuka ilikuwa ni karibu kabisa na uchaguzi mkuu 2015, nikiwa nimelala chumba cha upande wa mbele wa nyumba yetu huko kijijini katika jimbo alilokuwa anawania Dkt Mollel kwa tiketi ya CHADEMA.Ghafla kama kimondo nilisikia jiwe kubwa limepiga kioo likatoa sauti kubwa sana ya mpasuko wa kioo.

Niliogopa na kufikiri ni ndoto lakini kabla sijang'amua kama ile ilikuwa ni ndoto au ni kweli, nilisikia watu wanatembea kwa vishindo na hali ya kuogofya huku wakiulizana maneno ambayo sikuyaelewa - ni kama fujo fulani. Watu wengine wakaamka ila kwa tahadhari sana.

Nikaenda sebuleni kuungana nao ndipo nilipowasikia wakitafuta sehemu ya kupanda ili washushe bendera ya CCM iliyoko juu ya bati letu. Ndipo wote tulijua hawa ni CHADEMA hofu ilitanda

Tuliogopa na kukimbilia jikoni huko ambako ni upande wa nyuma wa nyumba.
Hofu ilitujaa ukizingatia siku mbili zilizopita mwanachama mmoja kindaki ndaki wa CCM alilawitiwa na kutupwa maeneo ya makaburini na CHADEMA walijigamba baada ya tukio lile kwamba watakomesha na wengine.

Walifanikiwa kupanda juu wakashusha bendera kama baada ya dakika 10 pakawa kimya.

Ndipo baba akapigiwa simu na mlinzi wa maeneo ya maduka ambako na sisi tunaduka pale kwamba jamaa wamepanda juu ya bati la duka wanatoa bendera na pia wanachana picha za wagombea wa CCM zilizobandikwa kwenye kuta za duka letu.

Nikiri baba alikua mpenzi kindakindaki wa CCM na alitupa mifano mingi kwa nini tunapaswa kuienzi CCM.
Sikuwahi muelewa ila usiku ule nilimuelewa. Sikulala usiku kucha nikiwaza kama kweli hawa jamaa wakiingia ikulu itakuwaje?

Joto la uchaguzi lilipanda sana na kampeni za CHADEMA zilihusisha kuvamiavamia maeneo ya biashara za wanachama wa CCM na vitisho vingi matusi ya waziwazi niliyashuhudia.

CHADEMA walifanya uvunjifu mkubwa wa haki za kibinadamu na pia amani kipindi cha uchaguzi wa 2015 na kama kuna mwanahabari anayetaka kutengeneza habari nitampa evidence zote

Maana hata huyo jamaa aliyelawitiwa na CHADEMA aliwaona na anawajua sema alienda mafichoni na eneo alipo ninalifahamu.

CHADEMA wanaimba haki,utawala bora na usawa lakini vitendo walivyofanya wakati wa uchaguzi viliumiza watu wengi sana.

Naamini uchaguzi wa mwakani na huu wa Serikali za Mitaa mtaufanya kwa amani maana kwa staili ile hamkutakiwa kupata hata kitongoji kimoja.
Dada unaficha ficha Nini kwanini usiwe mkweli, vp unaona aibu kusema kuwa wewe ndio ulie lawitiwa?

Kama siyo wewe muhanga watukio Hilo Leo Nini kimekusibu hata uo umbea uulete leo,?! sikuzote ulikuwa wapi kutuletea umbea
 
sifa ya kuwa mwachadema uwe mfanya vurugu na mchochezi wa hali ya juu sisi siyo utamaduni wetu
 
Afadhali wewe kioo kilipgwa jiwe. Fikiria Mwenyekiti wa CHADEMA kule Arusha alikatwa shingo kwa chainsew. Mawazo alikatwakatwa kwa mapanga. Ben Saanane njia aliyoipitia Mungu tu ndiyo anajua.

Lazima uwe mpumbavu sana kuamini kuwa kuna uungwana ndani ya CCM. Ndani ya CCM kuna majitu ni mauaji na maharamia ya kiwango ambacho ni nadra kushuhudiwa hata huko kwenye udikteta uliokomaa, kama Korea Kaskazini.

Ndani ya CCM na serikali kuna majitu ambayo japo ni mafuasi ya shetani lakini kwa uovu yanamzidi hata shetani mwenyewe.

Mara nyingi watu wa CCM na serikali wamekuja kunishawishi kujiunga na CCM eti ili nigombee ubunge. Naliapia jina la Mwenyezi Mungu sitathubutu kujiunga na CCM au chama chochote ambacho kipo tayari kuua kwa sababu ya madaraka. Sijakosa roho ya Mungu kiasi cha kujichangamanisha na wauaji. Namwomba Mungu daima, isitokee hata siku moja nikajiunga na uovu dhidi ya mwanadamu mwenzangu, katika maisha yangu yote ya kuwepo hapa Duniani.
dahaa hatari sana
 
Back
Top Bottom