Usiku wa leo wanaitaka roho yako!

Usiku wa leo wanaitaka roho yako!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Usiku wa leo wanaitaka roho yako! Leo usiku roho yako itachukuliwa! Leo usiku maisha yako yatafikia mwisho, utaondoka duniani...

Usishtuke wala usiogope; sio wewe! Maneno hayo aliambiwa mtu fulani tajiri. Shamba lake lilizaa sana. Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Sina mahali pa kuhifadhi mavuno yangu.’ Ndipo huyo tajiri akasema, ‘Nitafanya hivi: Nitabomoa maghala yangu ya nafaka na kujenga mengine makubwa zaidi nihifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu. Kisha nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, unavyo vitu vingi vizuri ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi. Pumzika; kula, kunywa, ufurahi.”'

Lakini Mungu akamwambia, ‘Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?’

Habari hiyo inapatikana katika Luka 12. Ni habari inayotuhusu sisi sote. Inawezekana hata wewe umetafuta pesa, umeweka akiba ya kutosha, sasa unapanga mipango ya kwenda mahali kula, kunywa na kustarehe, bila kujua kwamba usiku wa leo maadui zako wanataka kukuangamiza. Sasa, hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?’

Mungu atusaidie kukumbuka hilo. Kwamba wakati tusiodhani, maisha yetu yanaweza kukatika. Hivyo tujitajirishe pia kwa Mungu, ili tukiondoka, tuweze kupumzika na kustarehe mbinguni.
 
Hilo ni fundisho kwa kila mtu anayehangaikia tu mambo ya dunia hii, bila kukumbuka kwamba kuna maisha baada ya kifo.

Jiulize sasa: je, umejiandaa kwa siku yako ya mwisho? Je, ukiitwa uondoke duniani usiku wa leo, uko tayari?

Yesu hakutoa habari hiyo kututisha. Anatuwazia mema. Hapendi tupate hasara. Maana itamfaidi nini mtu akiupata ulimwengu wote, kisha akayapoteza maisha yake?(Marko 8:36). Mtu atapata faida gani akila na kunywa na kustarehe hapa duniani kwa miaka 20, kisha akateseka milele na milele katika moto wa jehanam?
 
Jiandae basi ndugu, usingoje mpaka giza likushukie. Leo ndio siku ya wokovu. Tubu leo, mpokee Yesu na kumkabidhi maisha yako, maana hakuna mtu aijuaye siku yake ya kutoweka duniani. Ukifanya hivyo, hata wakiitaka roho yako, itakuwa faida tu kwako kama Mtume Paulo alivyosema: "...kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi."(Wafilipi 1:21-27)
 
Waruhusu waichukue roho yako kwa vile umeridhia 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀
"Kwangu, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi. Lakini, kama kwa kuishi nitaweza kufanya kazi yenye faida zaidi, basi, sijui nichague lipi! Nakabiliwa na haya mawili yaliyo sawa. Natamani kuyaacha maisha haya nikakae pamoja na Kristo, jambo ambalo ni bora zaidi; lakini ni jambo la maana zaidi kwenu kama nikiendelea kuishi. Nina hakika ya jambo hili, na hivyo najua kwamba nitaendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili nipate kuongeza maendeleo yenu na furaha katika imani"(Wafilipi 1:21-27 BHN)
 
"Kwangu, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi. Lakini, kama kwa kuishi nitaweza kufanya kazi yenye faida zaidi, basi, sijui nichague lipi! Nakabiliwa na haya mawili yaliyo sawa. Natamani kuyaacha maisha haya nikakae pamoja na Kristo, jambo ambalo ni bora zaidi; lakini ni jambo la maana zaidi kwenu kama nikiendelea kuishi. Nina hakika ya jambo hili, na hivyo najua kwamba nitaendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili nipate kuongeza maendeleo yenu na furaha katika imani"(Wafilipi 1:21-27 BHN)
Kama ni kweli, basi kufa ili 'ukutane' na huyo bwana wako. Enjoy your marriage.
 
Karibi nusu saa nzima bundi analia juu ya nyumba. Toka jumanne niko hoi kitandani. Inaogopesha kiasi🥺
Ndugu yangu Da'Vinci , usiogope. Katika Kristo tuna ulinzi mkuu. Bundi ni ndege tu kama wengine; hana mamlaka juu ya maisha yetu. Na hofu haitoki kwa Mungu. Nataka nikuongoze sala ya imani ili upokee ulinzi na amani ya Mungu.

Kwanza omba sala hii ya Toba. Fuatisha maneno haya:

"Ee Mungu nakushukuru kwa kunipenda na kunitafuta hata sasa. Ninatubu dhambi zangu zote—nilizotenda kwa maneno, kwa matendo, na kwa mawazo. Naomba unisamehe, unitakase, na unioshe kwa damu ya Yesu. Ee Yesu, leo nakukubali uwe Mwokozi wangu na Bwana wa maisha yangu. Tawala moyo wangu na unijaze kwa Roho Mtakatifu. Katika Jina la Yesu, Amen."

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wa dhati, tayari umeokoka, na uko salama sasa katika mikono ya Yesu. Shetani, mapepo na wachawi hawawezi kukuangamiza. Mipango yao tayari imesambaratika kwa Jina la Yesu.

Sasa, fuatisha tena sala hii ya kuomba ulinzi wa Mungu:

"Baba wa mbinguni, nakuja mbele zako kwa jina la Yesu Kristo. Ninaikataa kila hofu na kila roho ya giza inayojaribu kunitisha. Ninajifunika kwa damu ya Yesu na ninatangaza kwamba mimi ni wako Mungu na ninalindwa na mkono wako. Iwe ni usiku au mchana, sitatetemeka tena wala sitaogopa, kwa maana Bwana Yesu ndiye Mchungaji wangu. Naomba Ee Mungu uniponye, unilinde siku zote na unijaze amani yako. Nijalie sasa kulala usingizi mzuri wa amani.
Kwa Jina la Yesu, nakukemea shetani. Toka hapa na vitisho vyako. Umeshindwa kwa Jina la Yesu Kristo. Asante Mungu kwa kunilinda na kunifariji, katika Jina la Yesu Kristo, Amina."


Mungu atakuwa pamoja nawe. Usitishike tena. Kumbuka: Usimwogope shetani wala maajenti wake, kwa kuwa Yesu aliye ndani yako sasa ni Mkuu kuliko shetani na mapepo yote na wachawi (1 Yohana 4:4).

Ukisikia bundi analia, kiri maneno haya:
Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA(Zaburi 118:17)

Malaika wa Bwana wakulinde, na neema ya Mungu ikufunike. Ulale unono 😴
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom