Usiku mzito na vituko vya mauza uza

Usiku mzito na vituko vya mauza uza

Super mega

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2023
Posts
1,177
Reaction score
2,361
Habari za muda huu wakuu,

Leo muda huu nimekumbana na visa vya mauza uza wakati nipo katika usingizi ilikua kama ndoto lakini ni ndoto ya uwazi yani nikisema uwazi namaanisha matukio yaliyo kuwa yanatokea nayaona kwa uhalisia huko huko usingizini na ndotoni,

Ilikua ni mapigano makali na mazito baina yangu na mtu mmoja ambaye ni mtu mzima kwangu basi yule mzee katika kupambana kweli mimi niliona kabisa haya ni mapambano ambayo mimi inabidi nitumie Imani yangu kama siraha kwakua tayari nilioneshwa kuwa hii vita ni ya kichawi kabisa kwakweli kupitia imani yangu nilimuomba sana Mwenyezi anisaidie kweli sio jambo jepesi niliona kabisa bila maombi ya dhati na ya kweli

Nilikua sichomoki kabisa mzee huyu alikua na nia ya kunimaliza kabisa lakini kwa uwezo Mwenyezi Mungu nimetoka salama na ndio nimepata na nguvu ya kuandika kisa hiki usiku huu,niseme bado hakuja kucha hivo vita inaweza kuendelea tena au ikawa imepumzishwa hadi siku nyingine...tusiache kusali usiku ni mrefu sana na una mambo mengi sana.
 
Muwe mnafua mashuka , unapolala kuwe mzunguko mzuri wa hewa , pia punguza kushiba sana kabla ya kulala !

Ni ndoto hizo
Mkuu kwa kusema mashuka ni machafu sio kweli kabisa sipo katika hatua hizo kabisa ni hali tu ya usiku kuwa vibaya na sio ndoto au kwamba nilikula chakula kigumu hapana nimekula kias kidgo sana.
 
Kwamba ilikuwa ndoto halafu ukamuona kwenye macho ya uhalisia halafu ukanzaa kuomba mungu kwa imani yako
halufu ukamshinda HALAFU UKAPATA NGUVU ZA KUANDIKA UZI halafu umekula maknde ya degu ukavimbewa halafu tumia rungu kuangamiza hao kunguni maana nawaona hadi kwnye uzi wako
 
Kwamba ilikuwa ndoto halafu ukamuona kwenye macho ya uhalisia halafu ukanzaa kuomba mungu kwa imani yako
halufu ukamshinda HALAFU UKAPATA NGUVU ZA KUANDIKA UZI halafu umekula maknde ya degu ukavimbewa halafu tumia rungu kuangamiza hao kunguni maana nawaona hadi kwnye uzi wako
Nikifa MkeWangu Asiolewe soma taratibu tu huna haja ya kuleta dhihaka.
 
Madhara ya kushiba sana ugali mda wa kulala !

Kula kistaarabu mida ya kulala si Kula kama upo kwenye mashindano au vita .
Mkuu sikumbuki kabisa nimekula lini ugari hata kwa mchana tu
 
Itakua ulibanwa mkojo, Mara nyingi sana inakuaga hivyo
Duh kabla sijaingia kulala huwa najiweka mwili kuwa mwepesi ikiwepo kutoa haja ndogo na zingine pia huwa nanawa kabisa uso ila usiku wa leo nimelala kwa tabu sana mkuu mpaka kuna kucha sina amani.
 
Back
Top Bottom