Usikate tamaa

Usikate tamaa

Katika maisha , unapoanza kufanikiwa katika kila nyanja,
Nakuhakikishia shetani atakuja na kila aina ya uharibifu, Hasa kupitia kwa watu wako wa karibu.

Ataleta majaribu kutoka pande zote,
Kila mtu atakuzungumzia vibaya, wapo watakao kukatisha tamaa, kukudhalilisha, kukufanya ujihisi mwenye hatia, kukufedhehesha na wengine watakuonea wivu, . . . . etc.
Ni kawaida kujisikia vibaya kwa sababu wewe ni binadamu kama mimi, na kila binadamu ana hisia.

Katika kipindi hiki unaweza hata kumsahau Mungu nakuhisi Mungu hayupo kwakuwa unaona kila unacho Muomba hakuna majibu.

Sikia nikwambie, hilo ni suala la muda tu na kila mtu anapitia, mambo yote yatakuwa sawa.

Ni kipindi kigumu sana kwakuwa katika kipindi hichi utasalitiwa, utaonewa, utahukumiwa, na kusingiziwa. Lakini Mungu atawafichua na kuwaondoa rafiki wabaya wanaokuzuia usisonge mbele.

Wakati umekata tamaa kabisa kwa hayo unayopitia ndipo Mungu atakapokushangaza kwa Ukuu wake, atakubariki kuliko vile ulivyomuomba. Atakufungulia milango ya Baraka na Neema kila kona, Atawaaibisha adui zako. Hapo waliokudharau watatamani wawe hata vijakazi wako. Watakuamkia hata kama una umri mdogo kuliko wao.

Kazana kupambana, usikate tamaa Mungu yupo na wewe. Wewe ni mshindi , Pambana hadi ingwe ya mwisho, ndiyo unaweza. Kwa sababu una Mungu na Mungu ndio kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Barikiwa sana Soja p, ujumbe mzuri sana hasa "kwangu mie kwa kipindi hiki"blessed much!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta uzi umelenga mimi dah, Haya maisha aiseeh Mungu tusaidie unajitahid kuitafuta hata buku unakosa
 
Back
Top Bottom