G
guest-1787677877
Guest
Nikutie moyo kijana unayepita katika majaribu.
Inawezekana umemaliza chuo na huna ajira. Nikutie Moyo, kuna jamaa yangu kapata ajira akiwa na miaka 41 na sasa ni mtu mkubwa tu. We bado sana kwa umri wako.
Mungu yupo atakukumbuka na kuna majira ya kila jambo chini ya jua. Majira yako hayajafika, yakifika hata muende interview watu 100,000 kwa nafasi 1. Utapata wewe.
Inawezekana unapita kwenye msongo na msoto mkubwa wa kimaisha tokana na hali ya kiuchumi. Songa mbele Milango yako itafunguka.
Nikutie moyo, usikate tamaa kijana Songa mbele. Binafsi nilipita katika hali ngumu nikawa nauza sigara za kutembeza mikononi miaka ya nyuma, sasa ni mtu mwingine. Endelea na Mapambano. Simama imara, muombe Mungu, tunza afya yako, fanya kazi kwa bidii na Mungu atakusaidia na kukuvusha.
Inawezekana una changamoto katika kazi yako, muamini Mungu kiwa nalo litapita. Aliyekuvusha mwanzo hata sasa atakuvusha.
Angalia hiyo picha ya PM hpo. Ikutie nguvu katika mapambano yako ya kila siku ya kutafuta mkate. Kuwa na subira, muaminifu na Mtazame Mungu tu utavuka.
Mungu awasaidie na akutane na haya za mioyo yenu. Kwa mgonjwa, yeye atakuponya mtegemee yeye tu.
Mungu awabariki na kuwatia nguvu wapambanaji wa JF.