Kijana kijana
JF-Expert Member
- Mar 11, 2018
- 2,546
- 2,624
Habari wakuu natumai ni wazima
Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya wale ndugu zetu wa damu ambao hawana dini na wanaeneza taarifa ambazo zinakataliwa na dini zote na akili salama za mtu. Wanasema hakuna maisha(moto au pepo)baada ya kifo. Wanakusudia eti ukifa wewe unapotea tu hewani kama kuku, mbuzi au mnyama mwingine.
Hii akili sio salama kabisa ndugu zanguni kwa sababu kwanza dini zote kuu(uislamu na ukiristo)zinathibitisha kuwepo kwa maisha baada ya kifo tena motoni au peponi. Kwa maana ukifa unafanya madhambi utaenda motoni na ukifa unafanya mema utaenda peponi.
Hii kuamini hivi ndio salama kabisa kiakili na ndio usahihi kwa sababu hawa wenye madai haya wanasema hivi vitabu vya dini vimeandikwa na watu kama sisi ili tuheshimu tu tawala za dunia. Yani kwamba eti ukienda kanisani au msikitini unapewa mawaidha na kuambiwa acha pombe acha kuiba acha wizi acha wake za watu n.k eti pale unaheshimu falme za dunia.
Sasa ukijizuia kuzini, kuiba, kutapeli, kupora na dhambi zinginezo hivi unakuwa unatii ufalme wa nchi gani hapa duniani?
Ufalme wa nchi unafahamika sheria zake ni za katiba na hata hao wanaosema hakuna maisha baada ya kifo wanatii katiba za nchi kwa heshima kabisa, lakini wanawabeza wale ambao wanafuata Katiba ya Mungu kiimani.
Sasa hawa hawaoni kwamba wao ndo wanatii falme za nchi kwa kutii na kufata katiba za nchi?
Ajabu zaidi wanasema hivi vitabu vinavyoitwa vya Mungu vimeandikwa na watu tu yani mfano taurati kaiandika mtu tu au injili au quran kwa hivyo wanatuambia kwa kuwa kaandika mtu basi haina haja ya kutii na kuziamini kwa kudai ni uongo.
Tujiulizeni sasa, hawataki kutii vitabu vya Mungu kwa kuwa eti vimeandikwa na watu, sasa mbona wanazitii katiba ambazo zimetungwa na watu ambao wanawalalamikia ni walevi, mafisadi au madikteta au wana mapungufu fulani huko Bungeni?
Mbona wanazitii zilizotungwa Bungeni na watu vile vile? Kuna tofauti gani kati ya watu hao wanaowatii sheria zao (katiba)na watu wale walioandika vitabu vya Mungu?
Kwa sababu ikiwa wanakataa kiukweli kutii vilivyoandikwa na watu basi WAWE WAKWELI MBONA WANATII KATIBA ILIYOANDIKWA NA WATU VILE VILE?
Mfano katika kununua bidhaa kuna taratibu unafuata kama risiti au viwanja lazima ufuate taratibu za nchi, enhee hamzifati kwa kuwa zimetungwa na watu?
Hawa watu ni waongo kabisa na akili zao kidogo zina pepo mchafu amewachezea wanajikoroga tu. Kwa sababu kwa akili ya kawaida tu tunajua kuzini ni madhambi au kuiba au kuchukua mke wa mtu n.k. Sasa jiulize akilini tu kwamba ikiwa kuna maisha baada ya kifo hivi kweli kuna ambae ataadhibiwa na Mungu kwa kuwa tu eti hakuiba au hakuzini au hakulewa?
Nadhani akili haikubali jambo hilo, sasa ikiwa wewe unaamini kwamba tukifa ndo tumekufa alafu ukawa hapa duniani ushakula wake za watu, umeiba, umelewa na kufanya ufisadi kisha ukafa na hali hiyo ukakutana na maisha mengine hivi huoni utakuwa imekula kwako?
Na yule ambae hakufanya hayo uliyofanya wewe na akafa akakuta hali hiyo ya maisha ya milele huoni kama atakuwa amekula donge nono? Na ikiwa huyu hakukuta maisha baada ya kifo na wakati duniani alijizuia na madhambi atapata hasara gani huko?
Sasa ndugu we jifanye huamini ukaenda huko ukayakuta utajuta si utakuwa ueingia cha kike?
Wanasema tena eti sisi ni kama wanyama wakifa ndo wameshakufa kabisa,sasa tujiulize jamani hivi kweli sisi ni sawa na wanyama? Hawa wanyama si wanaingilia mama zao jamani na dada zao, sasa na sisi tunaishi hivyo?
Halafu hawa wanyama wanaongozwa na katiba gani? Ni kwa sababu wanyama hata kiakili wako tofauti na binadamu kabisa kimaumbile na vinginevyo, sasa hawa watu wenye itikadi hizi hamuoni kama wanajifananisha na wanyama tu?
MWISHO NISEME TU WEWE ENDELEA KUMTII MUNGU WAKO HATA UKIFA UKAKUTA NI FAIDA NA USIPOKUTA HAUTAADHIBIWA ETI KWA KUWA HUKUNYWA ULEVI WALA KUZINI WALA KUIBA N.K.
LAKINI NI HAKIKA YAPO MAISHA BAADA YA KIFO