Mjasiriamali1
JF-Expert Member
- Jun 8, 2009
- 891
- 237
Dah yamenikuta, tiketi kuelekea Arusha nimekata saa 12 gari linaondoka saa 3. Usije ukakata hili basi kama unaharaka zako utajuta. Yasije kukuta yaliyonikuta mimi. Lakini najiuliza ile spidi ya Sumatra iko wapi kukagua magari! Kupiga fine walikuwa njiani kila mahali. Wakatoa simu matangazo mpaka kwenye mabasi. Je ilikuwa ni nguvu ya soda. Ni kama vile wametulizwa, kwishiney kabisa, vitu vingi serikali inakuja spidi alafu inatulia kabisa kama vile wamepigwa mute. Najiulizaga kwanini uanze kitu kama unajua huwezi kukifuatilia mpaka mwisho? Ningejua ningekata gari langu la kila siku.