Usije ukaoa au kuolewa Kwa sababu unampenda na hutaki kumpoteza

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
"Usije kukimbilia kuoa/Kuolewa kwa sababu unampenda na hutaki kumpoteza"

Vijana wenzangu leo tukumbashane mambo machache tu hapa kwenye mahusiano,

Katika pita pita zako unaweza kujikuta tu umetokea kupendana na mtu flani Me au Ke, na katika hali hii kwa kuwa unampenda sana utatamani kumuoa/Kuolewa nae kwa sababu tu hutaki kumpoteza,

Ndugu yangu fikiria sana Ndoa sio swala la mchezo mchezo unaitaji muda wa kukaa na kujipanga, unahitaji muda wa kukaa na kuangalia lipi chaguo lako sahihi,

Mihemko ya muda mchache inaweza kukufanya ujute katika maisha yako yote, jipe muda wa kukaa na kufikiri, jijue na kuamua kwamba kwa sasa kweli naitaji mtu wa kuoa /Kuolewa, Angalia chaguo lako sahihi usitazame cheo, pesa, Elimu, uzuri, wala mali tazama ule upendo wa dhati ulio moyoni mwake,

Kumbuka kwamba unapoamua kuoa utakuwa umekubali kwamba kile kipande kilichobaki cha maisha yako baada ya kuishi kipande kingine kutoka kwa wazazi wako utakiishi pamoja na huyo mwenza wako mpaka pale umauti utakapofika kwa mmoja wenu,

Usije kukimbilia kuoa/kuolewa kwa sababu unampenda na hutaki kumpoteza jua una muda mchache sana wa kufurahia mahusiano nae ila mwisho huja majuto makubwa na Majuto yake ni ya Umilele.

Nb.
Wale wazee wa kucopy na kwenda kupaste kwenye blog/Website zenu tafadhari sana msisahau kutaja mwandishi wa Andiko mr Zero IQ.

Cc Zero IQ
 
Nimekunyaka vilivyo mkuu... Mara nyingi upendo ni mihemuko ya muda mchache.. Unahitaji commitment ya hali ya juu kufikia maamuzi ya kuoa au kuolewa na huyo mtu.
 
"Usije kukimbilia kuoa/Kuolewa kwa sababu unampenda na hutaki kumpoteza"

Vijana wenzangu leo tukumbashane mambo machache tu hapa kwenye mahusiano,

Katika pita pita zako unaweza kujikuta tu umetokea kupendana na mtu flani Me au Ke, na katika hali hii kwa kuwa unampenda sana utatamani kumuoa/Kuolewa nae kwa sababu tu hutaki kumpoteza,

Ndugu yangu fikiria sana Ndoa sio swala la mchezo mchezo unaitaji muda wa kukaa na kujipanga, unahitaji muda wa kukaa na kuangalia lipi chaguo lako sahihi,

Mihemko ya muda mchache inaweza kukufanya ujute katika maisha yako yote, jipe muda wa kukaa na kufikiri, jijue na kuamua kwamba kwa sasa kweli naitaji mtu wa kuoa /Kuolewa, Angalia chaguo lako sahihi usitazame cheo, pesa, Elimu, uzuri, wala mali tazama ule upendo wa dhati ulio moyoni mwake,

Kumbuka kwamba unapoamua kuoa utakuwa umekubali kwamba kile kipande kilichobaki cha maisha yako baada ya kuishi kipande kingine kutoka kwa wazazi wako utakiishi pamoja na huyo mwenza wako mpaka pale umauti utakapofika kwa mmoja wenu,

Usije kukimbilia kuoa/kuolewa kwa sababu unampenda na hutaki kumpoteza jua una muda mchache sana wa kufurahia mahusiano nae ila mwisho huja majuto makubwa na Majuto yake ni ya Umilele.

Nb.
Wale wazee wa kucopy na kwenda kupaste kwenye blog/Website zenu tafadhari sana msisahau kutaja mwandishi wa Andiko mr Zero IQ.

Cc Zero IQ
Dah! Kuna mtu ameihack na anatumia ID ya Zero IQ
 
Back
Top Bottom