Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,712
- 830,745
Ukipita mitaa ya kariakoo hasa Congo, na mitaa yote karibu na shule ya Uhuru mpaka msimbazi polisi ni kawaida kukuta matangazo ya kununua simu na saa mbovu
Tahadhari: usijaribu kuuza kitu chako kibovu kwakuwa hakitanunuliwa! Sana sana kitaongezewa ubovu kwa kuchomolewa vifaa ambavyo bado ni vizima
Kinachofanyika ni hiki: wengi wanaoweka haya matangazo ni mafundi hivyo unapeleka kitu chako kikiuza hukuambia rudi baada ya muda fulani, kinachofanyika huku nyuma ukiondoka hufungua na kutoa vifaa vyote vizima na kukuwekea vibovu kabisa
Muda uliopewa ukirudi unaambia kitu chako hakiuziki hivyo kichukue tu, kwakuwa ni kibovu hutaweza kumbana kwa lolote lile lakini tayari utakuwa umeshamfaidisha kwa kuchukua vifaa vilivyo vizima na kuwekewa vibovu kabisa
Ushauri: muulizie tena kwa fedha tasilimu yeyote anayehitaji tena bila kupeana muda wa kurudi kuchukua pesa yako! Wajanja ni wengi siku hizi na wezi ndio wametamalaki kila kona