Usihofie kile ambacho utapoteza, fikiria kile ambacho utakikosa kwa kutofanya

Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,323
3,353
Badala ya KUHOFIA kile ambacho UTAPOTEZA kama ukiamua KUFANYA,fikiria kile ambacho UNAKIKOSA kwa KUTOFANYA.

Tafiti zinaonyesha kuwa watu wengi wanapokuwa wazee HAWAJAILAUMU KWA MAMBO WALIYOFANYA bali wanajilaumu sana kwa MAMBO AMBAYO WALITAKIWA KUFANYA ila HAWAKUFANYA(Nakushauri usome tena sentensi hii na uielewe).

Majuto makubwa ambayo utakuwa nayo kwenye maisha yako,sio yale uliyoyafanya na UKAKOSEA bali yale ambayo hukuyafanya na UKAKOSA fursa za KUWA na KUPATA ulichostahili.

Hivi leo ungekuwa wapi kama yale mambo ulisema mwaka huu utayafanya ungekuwa umeshayafanya?Hivi maisha yako yangekuwaje kama ungeweka hofu pembeni na kuchukua maamuzi ambayo umekuwa unayaghairisha kila siku?Si unakumbuka ulivyokuwa umekuwa nadhiri ya kuwa wa tofauti na ukajiwekea muda kabisa,lakini hadi leo hakuna hatua uliyochukua?

Kumbuka kuna mambo mengi ambayo unayaghairisha,maamuzi mengi amabyo unayaogopa na hatua nyingi ambazo unazihofia:NDIO ZIMEBEBA MABADILIKO YAKO MAKUBWA.

Kila unapoghairsha,kumbuka unapunguza uwezekano wako wa kufanikiwa.Kila unapohofia kuchukua hatua unakuwa umefanya maamuzi ya kuwa mtu mdogo kwenye maisha yako.

KAMA SI LEO NI LINI?
ALAMSIK
download%20(1).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom