Nawahurumia sana viumbe hai ninapowakuta kwenye matatizo

emmarki

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
503
535
Habari wanajamvi,

Nina hali ambayo sijui niiterm kama tatizo au ya kufurahisha.

Ninajikuta navionea huruma sana viumbe hivi visivyokuwa na hatia wanyama, ndege na wadudu wa aina zote (kufugwa na wasiofugwa), ninapokutana navyo vikiwa kwenye hali yoyote itakayohatarisha uhai wao.
Nikupe scenarios ninazokutana nazo au ambazo nimewakuta hawa viumbe nikajikuta nawasaidia bila kujali aina ya kiumbe.

1: Kuwasaidia kuvuka barabara/njia. Vinyonga na konokono nikikutana nao anajitahaidi kuvuka njia kuelekea upande wa pili, najikuta nasimama na kuwasaidia kuvuka kwa kuwabeba kwa kijiti au kushika na mikono yangu. Nafanya hivyo coz najua mpita njia/boda zitakanyaga na kuwau.

2: Mende, nzi, mbu na wadudu wengine warukao nawanasua wanapokuwa wamenasa kwenye maji au kushindwa kuruka. Niliwahi ishi mabibo, choo kilikuwa na mende wengi hivyo nikikuta wale wanaoshindwa kutembea nakuwa na kazi ya kuwabinua na kuwanasua ili watembee. Nzi nkiwaona wamenasa kwenye ndoo za maji nawatoa na kuwaacha waende zao. Siui mbu wa mchana.

3: Mbwa, paka nanwanyama wengine wadogo wanaofanana na hao. Nikiwa nimepanda boda au daladala mwenye akili mbovu waopenda kugonga hawa viumbe huwa nahamaki kwa kelele huku nmeshika kende zangu nkiamini hatagogwa. Asipogongwa nafurahi sana, mimi ni introvert lkn kwa hilo huwa nakuwa mkali gafla. Inapotokea nkaona mbwa au paka kafa njiani kwa kugongwa ninaumia sana.

4: Nkikuta kuku na vifaranga wake wako barabarani nawafukuza ili wasigongwe.

5: Ni mfugaji mzuri, changamoto inapokuja kwenye kuuza naumia moyoni sana. Sichinji kuku....lkn nyama nakula

6: Nyoka na wadudu hatari, nikiitwa niue endapo kakutwa kwenye mazingira ya watu nitawazuga na kumtengenezea mazingira mpk nyoka akimbie.

Hali ya kutaka kusaidia hutokea gafla sana akilini, kiasi kwamba siangalii niko mazingira gani na kiumbe huyo ana hatari gani kwangu.

Kwa sehemu ninaposhindwa either nmekuta kafa au hali hairuhusu kumsaidia naumia sana. Najikuta najiuliza ni tatizo la akili au lkn nakumbuka mwenye tatizo la akili hawezi jitambua kama ana tatizo
 

Southern Highland

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
10,348
15,010
Wewe umepitiliza yan hadi mende na nzi? Mimi nikiona mtu ana mtreat mbwa vibaya ndio huwa najisikia vibaya ila paka pia siwezi kukaa nao nitawafukuza tu.

Unawezaje kula kuku na kuchinja unashindwa? Utakua na psychological problem

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
8,759
5,742
Mshirikishe Mungu umuulize kwa nini aliamua kuweka kitu hicho ndani yako. Siyo wewe, ni Mungu
 

emmarki

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
503
535
Huo ni ugonjwa wa akili

Hata baba angu huwa anao,ni afisa mifugo,ng'ombe akiwa anaumwa akili ya baba haitulii na atamtibu hata kama mkulima hana hela
upendo wa kujaribu kuokoa kila kitu, japokuwa haiwezekani tunabaki kuumia tu
 

emmarki

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
503
535
Ohooooo sasa ndo naamini zile tafiti kumbe n za kweLiAFYA YA AKILI
AFYA YA AKILI
AFYA YA AKILI
AFYA YA AKILI
mzee, you're wrong. wazungu wanaongoza kwa kuown pets, kuna tasisi za haki za wanyama na shelters around the world...na wenyewe wana tatizo la akili mkuu!
 

emmarki

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
503
535
Wewe ni mtu uliyestaarabika
wangu umepitiliza, siku moja niko na mamdii wangu tuko njiani taratibu tunaelekea mahali, mara paap konokono mbele yangu anajikongoja taratibu kuelekea upande wa pili. Nlichofanya nilizuga naokota kitu, kumbe namuokota konokono ili asikanyagwe na shubaamiti bodaboda. Nikimaliza hilo zoezi nahisi kama vile nimeokoa dunia 😂
 
7 Reactions
Reply
Top Bottom