Usifosi tufanane

Usifosi tufanane

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,705
Aliamka asubuhi na mapema kufagia Uwanja wa nyumba. Jirani na nyumba yake akamuona mwanaume akifagia.

Hakuamini. "Mwanaume, muda kama huu aamke na kufagia, oh mke wake ana raha kweli."

Akampungia mkono, nae akapunga huku akitabasamu. Ndani ya moyo wake akawaza, "Hakika huyu ndio mwanaume bora, sio hili ambalo naishi nalo mimi."

Ingawa alikuwa akifagia, kwa chini chini alikuwa akimtazama mwanaume yule na kutamani kama angekuwa ndio mume wake.

Kwa hasira akaacha kufanya usafi na kumfuata mumewe chumbani. Muda huo mume wake alikuwa kwenye usingizi mzito huku akikoroma utafikiri kakanyaga 'clutch' na kuingiza gia namba tano.

Akamtazama mumewe na kusonya msonyo mkali kama ule wa muigizaji Riyama Ally. Moyoni akajitamkia, "Hili jitu pumbavu kweli, unalala unakoroma wakati mwanaume mwenzako wa jirani anamsaidia mkewe kufagia."

Muda kidogo, mume akaamka. Mke hakusubiri, 'akamchana live', "Hivi wewe baba James, unalala na kukoroma tu wakati Jirani yetu rafiki yako Baba Devotha anamsaidia mkewe kufagia nyumba."

Akaendelea ..

"Baba Devotha ni mwanaume Bora kabisa, kwanini usiwe kama yeye? Yaani wewe unataka kila kitu niwe nafanya peke yangu"

Ooh, maneno yale yalimchoma mno Baba James. Hakuna kitu kinachomuudhi na kumghafirisha mwanaume kama kufananishwa na mwanaume mwingine na kumwambia yeye sio Bora.

Hata hivyo, Baba James hakutaka ugomvi. Hivyo akakaa kimya na kupotezea.

Siku iliyofuata, Yule jirani utafikiri alitumwa na shetani kuivunja ndoa yake, alikuwa akifagia tena. Mara hii Mke hakuvumilia, akaenda kumuamsha mumewe aliyekuwa akikoroma lengo ili aje amuone mwanaume mwenzake akifagia.

Kama kawaida yake, hakusema lolote. Aliamka, akashuhudia na akaelewa somo.

Siku ya tatu, Baba James akaamka asubuhi na mapema kabisa. Akahakikisha anafanya usafi bila ya mtu yeyote kumuona. Siku ya nne vivyo hivyo. Mke akafurahi, moyoni akajisemea, "Yes, nimeweza kumtawala. Hiki ndicho nilichokitaka."

Labda hukufahamu. Kwa sababu haikuwa kama alivyojifikiria.

Siku hiyo ilikuwa ijumaa. Baba James ambae alikuwa akirudi nyumbani kabla ya saa moja jioni ambapo akichelewa sana ni saa moja na nusu, hakuwahi kurudi nyumbani saa nne na kuendelea, labda kama alikuwa na shughuri maalumu kazini.

Siku hiyo mpaka saa sita usiku hakuwa amerudi nyumbani. Mama James tokea saa moja alikuwa akimpigia simu lakini haikupokelewa.

Hatimae saa saba usiku akasikia mlio wa gari, akaamka haraka haraka huku akiwa na hasira tayari kwa ugomvi.

Baba James akaingia ndani ya nyumba, huku akiwa na harufu ya pombe wakati hajawahi kunywa pombe. Alionekana dhahiri amelewa.

"Oh! Nini kimemtokea mume wangu" Hakuelewa kabisa. Mama James akashindwa kuvumilia, akambwatukia mumewe.."Hivi umekuwaje wewe, hii ndio maana yake nini?"

Baba James akamwekea kidole kwenye mdomo wake akimaanisha akae kimya, kisha akaongea,

"Shiiii, tulia. Wanaume bora huamka asubuhi kufagia nyumba, na kila Weekend hurudi nyumbani kwa kuchelewa huku wakiwa wamelewa. Mimi ni mwanaume bora kabisa".

Bila kutegemea, muda huo huo na yule jirani yao alikuwa akirudi nyumbani kwake. Yule jirani alikuwa amelewa hovyo akitukana matusi ya nguoni na huku akiwa na mwanamke mwingine tofauti na mkewe.

Baba James akamchukua mkewe mpaka dirishani, akafungua pazia na kumwambia, "Angalia kule, huu ndio muda ambao wanaume bora tunarudi nyumbani. Kisha asubuhi tunaamka na kufagia uwanja.

Mama James alielewa somo lile kwa haraka. Hivyo akaenda kumuandalia chakula mumewe na kwenda kulala.

Siku iliyofuata Baba James, mapema kabisa akaamka aende kufagia, wakati akitaka kuondoka kitandani Mama James akamvuta kumzuia huku akimwambia, "Achana na hayo masuala ya mwanaume bora, njoo tuendelee kulala...sitaki mwanaume bora."

Baba James akatabasamu na kisha akarudi kulala. Akaamka muda wake wa kawaida na kwenda zake katika kibarua chake.

Asubuhi ile Mama James alijisikia vibaya kwa kuwa alikuwa ametazama upande mmoja tu wa yule jirani yao na kumuona kama ni mume bora bila kujua upande wa pili yupoje. Kumbe ni mlevi na mtu wa wanawake pia.

Baadae akaja kusikia kuwa yule 'Bwana' alikuwa akifanya vile kwa sababu mkewe alikuwa amesafiri, hivyo mara moja moja alikuwa akifagia nyumba mwenyewe.

Ooh kosa gani alikiwa amelifanya?

Na huyu sio mwanamke pekee anaekosea hivi. Wapo wanawake wengi sana wanawaambia wanaume zao kwanini usiwe kama yule au kama huyu bila kujua upande wa pili wa shilingi ukoje.

Hata wanaume pia, wanatamani wanawake wengine, bila kujua upande wa pili wa shilingi ukoje.

Ndio. Ni vizuri kupenda namna ya maisha ya watu fulani na kutaka na ya kwako yawe vile, lakini utambue haufahamu upande wa pili ukoje.

Wanandoa wengine wanaweza kuwa wote ni walevi na wanaenda Bar pamoja miaka na miaka. Ila ndoa yao iko vizuri tu. Sasa wewe jaribu kumpeleka mke wako Bar, my Brother utarudi nyumbani peke yako.

Wengine wanaweza kuwa wanahudhuria kanisani kila siku na wanakaa pamoja, lakini nyumbani ni vita ya Dunia isiyoisha.

Usijaribu kufananisha maisha yako na ya wengine. Endapo mtu uliyenaye anajitahidi kutimiza majukumu yake huna haja ya kuanza kuhitaji mengine zaidi. Hakuna binadamu atakayekuwa 'perfect' kwa asilimia zote.

Hata kwenye mambo mengine, iwe kiuchumi hata mahusiano ya kawaida Hebu kimbia mbio zako, Kisha watakie wengine kila la kheri katika mbio zao. Njia yetu inaweza kuwa ni moja ila Destination ni tofauti.

Wenyebusara washawahi kusema kwamba,

"Usiitamani nyumba kwa bati lake, kama huishi ndani ya nyumba hiyo"

Stay in your lane!!!
 
Ujumbe mujarabu kabisa. Kwa lugha nyingine tunasema usikihukumu kitabu kwa mwonekano wake (jarada lake).
 
Sawa sawa mkuu, hii ndo ile quote ya usemi usemao tuishi na wanawake kwa akili.
 
Back
Top Bottom