'Usifanye Mchezo na Binti Yangu' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Usifanye Mchezo na Binti Yangu'

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Sep 27, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  <table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  </td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Monday, September 27, 2010 3:14 AM
  Polisi wa nchini Marekani ambaye alitumia kazi yake ya upolisi kumtishia kumtia mbaroni kijana aliyemfumania akila uroda na binti yake ameingia matatani baada ya video ya tukio hilo kutolewa.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> "Si jambo zuri kufanya mapenzi na mtoto wa polisi", alisema afisa huyo wa polisi wakati akitishia kumtia mbaroni kijana mwenye umri wa miaka 15 aliyemfumania akifanya mapenzi na binti yake mwenye umri wa miaka 14.

  Afisa huyo wa polisi akiwa na unifomu zake alienda kwenye nyumba ya kijana huyo na kuwaeleza wazazi wake kuwa ameenda kumtia mbaroni mtoto wao kwa kosa la shambulizi la kijinsia.

  Alimfunga pingu kijana huyo mbele ya wazazi wake na kisha kuanza kumsomea risala kuwa ni jambo baya sana kufanya mapenzi na mtoto wa polisi huku akiuliza imekuwaje afanye mapenzi na binti yake ambaye kwa umri wake mdogo hajui hata kujitunza kama mwanamke.

  Baada ya kupiga mkwara mzito, afisa huyo wa polisi alimvua pingu kijana huyo na kisha kuwaambia wazazi wake kuwa alikuwa akimtisha kijana huyo kwa kitendo chake cha kutembea na binti yake wa kambo.

  Alimpa kadi ya kuonyesha amekamatwa na polisi na kumwambia aibandike kwenye friji iwe onyo kwake.

  Tukio hilo lililotokea wiki tatu zilizopita limeingia sura nyingine baada ya kijana aliyetiwa mshikemshike na polisi kuamua kulipiza kisasi akitaka afisa huyo wa polisi na yeye apate mshtuko kama alioupata yeye wakati akitishiwa kutiwa mbaroni.

  Uchunguzi dhidi ya afisa huyo wa polisi umeanzishwa kuhusiana na tukio hilo.

  Video ya tukio hilo imezua mjadala mkubwa nchini Marekani watu wakijadili kama afisa huyo wa polisi alifanya kitendo hicho kama mzazi mwenye uchungu na mwanae au kama afisa wa polisi ambaye alitumia vibaya magwanda yake ya kazi.

  Angalia VIDEO ya tukio hilo chini.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; text-align: center; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;">
  Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  </td></tr></tbody></table>
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  sioni kosa alilofanya, hata ingekuwa mimi ningemtishia hivyo hivyo pengine zaidi ya hiyo na ingekuwa hapa bongo polisi amfumanie mtu anam do na bentiye wa umri huo ujue ndiyo mauti yake kama si kum-babu seya.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nimeipenda hiyo signature yako!
   
Loading...