Usifanye biashara kama huna yafuatayo

Usifanye biashara kama huna yafuatayo

Habari nzuri hiyo nimeipenda
Suala la ushirikina limekuwa likitumiwa na wengi sana kukwamisha maendeleo. Ninaamini kuanzisha biashara ikakwama ni kitu cha kawaida lakini wengi wakiona umeshindwa basi ndiyo kigezo cha kujaji hata wengine wanaotaka kuanzisha biashara. Utasikia utaweza wewe hapa hata fulani alishindwa.
 
Usifanye biashara pia kama huwezi kuwa mshirikina either kwa kujilinda au kufanya chochote cha kuiendeleza biashara yako, tokweni povu ila mioyoni mwenu mnajua ni kweli
siyo kweli.....biashara za kishirikina hufiki popote zaidi utakua masikini zaidi sababu hutakua na ubunifu zaidi ya kutegemea uchawi
 
USIFANYE BIASHARA KAMA HUNA YAFUATAYO.

Sipendi kukuambia nini usifanye, kwa sababu ni hasi. Napenda kukuambia ni nini ufanye, ili iwe rahisi kwako kufuata vizuri.

Msisitizo unahitajika zaidi ili kuhakikisha kwamba tunakwenda sawa. Yaani tunaelewana vizuri na unafanya maamuzi yako ukiwa unajua vizuri ni kipi unakwenda kupata.

Kuna sababu nyingi sana za kwa nini wewe usiingie kwenye biashara, ila hapa leo tutajadili sababu moja muhimu.

Kama haupo tayari kujifunza kila siku, basi usiingie kwenye biashara, endelea na mambo mengine, ambayo yanaweza kuwa muhimu zaidi kwako.

Watu wengi wanapofikiria biashara huona kama ni sehemu wao wanakuwa mabosi na kusimamia wengine.
Lakini ukweli ni kwamba biashara ina changamoto nyingi kuliko picha hiyo unayojitengenezea. Na njia ya kuvuka changamoto hizi ili uweze kufikia mafanikio ni kuwa na maarifa sahihi. Na maarifa haya utayapata kama unajifunza kila siku kuhusu biashara.

Unapoingia kwenye biashara ni lazima biashara yako iwe muhimu sana kwako kiasi kwamba una shauku ya kujua vizuri na kwa undani. Ni shauku hii ndio inayokusukuma kujifunza zaidi na hivyo kubobea zaidi kwenye biashara hiyo.

Hivyo sababu ya kwanza kabisa kwa nini usiingie kwenye biashara ni kama hujawa tayari kujifunza kila siku.

Sababu nyingine muhimu sana ni MUDA, kama huna muda wa kutosha kusimamia biashara yako, wewe mwenyewe. Usifanye biashara utakua unapoteza pesa zako.

Kama huwezi kujitoa muhanga. Biashara ni risk. Kama unaogopa usifanye biashara kwani unaweza kukata tamaa na kuacha ukawa umepoteza pesa zako. Mafanikio hayaji mapema inahitaji subira sanaa.
umeongea vizuri sana hasa kwenye utayari .risk.na muda....usishangae kuanza biashara na milion kumi halafu baada ya mwaka ukajikuta umebaki na milioni moja tu hapo usikate tamaa kazana zaidi na zaidi baada ya hapo lazima upate faida
 
Bro mi nataka nianzishe biashara nipo chuo ili nikimaliza kusoma nisirud nyumbani, vp sitatu. Ia kianzio kikubwa sana, vp unanishaurije? Will i be succesful or not?
 
Bro mi nataka nianzishe biashara nipo chuo ili nikimaliza kusoma nisirud nyumbani, vp sitatu. Ia kianzio kikubwa sana, vp unanishaurije? Will i be succesful or not?
You will be very successful. Jipange tuu...
 
umeongea vizuri sana hasa kwenye utayari .risk.na muda....usishangae kuanza biashara na milion kumi halafu baada ya mwaka ukajikuta umebaki na milioni moja tu hapo usikate tamaa kazana zaidi na zaidi baada ya hapo lazima upate faida
Ni kweli nduguuu. Asante kwa mawazo yako.
 
mkuu mimi nina mke ninaye hapa chuoni ila yeye hasomi na nina mpango mwezi wa saba nianzishe biashara duka la nafaka hapa moshi yeye ndo atasimamia, mimi nitakuwa naenda kama sina vipindi, mkuu vipi nitakuwa napoteza hela ila napenda biashara niasoma BBA kwa hiyo napenda biashara na ninajifunza biashara na nipo tayari kwa risk.
Kama ni mwaminifu na ana mapenzi ya dhati na malengo na wewe ni wise decision.. wewe ndie unaejua tabia yake..
 
Back
Top Bottom