Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
USIFANYE BIASHARA KAMA HUNA YAFUATAYO.
Sipendi kukuambia nini usifanye, kwa sababu ni hasi. Napenda kukuambia ni nini ufanye, ili iwe rahisi kwako kufuata vizuri.
Msisitizo unahitajika zaidi ili kuhakikisha kwamba tunakwenda sawa. Yaani tunaelewana vizuri na unafanya maamuzi yako ukiwa unajua vizuri ni kipi unakwenda kupata.
Kuna sababu nyingi sana za kwa nini wewe usiingie kwenye biashara, ila hapa leo tutajadili sababu moja muhimu.
Kama haupo tayari kujifunza kila siku, basi usiingie kwenye biashara, endelea na mambo mengine, ambayo yanaweza kuwa muhimu zaidi kwako.
Watu wengi wanapofikiria biashara huona kama ni sehemu wao wanakuwa mabosi na kusimamia wengine.
Lakini ukweli ni kwamba biashara ina changamoto nyingi kuliko picha hiyo unayojitengenezea. Na njia ya kuvuka changamoto hizi ili uweze kufikia mafanikio ni kuwa na maarifa sahihi. Na maarifa haya utayapata kama unajifunza kila siku kuhusu biashara.
Unapoingia kwenye biashara ni lazima biashara yako iwe muhimu sana kwako kiasi kwamba una shauku ya kujua vizuri na kwa undani. Ni shauku hii ndio inayokusukuma kujifunza zaidi na hivyo kubobea zaidi kwenye biashara hiyo.
Hivyo sababu ya kwanza kabisa kwa nini usiingie kwenye biashara ni kama hujawa tayari kujifunza kila siku.
Sababu nyingine muhimu sana ni MUDA, kama huna muda wa kutosha kusimamia biashara yako, wewe mwenyewe. Usifanye biashara utakua unapoteza pesa zako.
Kama huwezi kujitoa muhanga. Biashara ni risk. Kama unaogopa usifanye biashara kwani unaweza kukata tamaa na kuacha ukawa umepoteza pesa zako. Mafanikio hayaji mapema inahitaji subira sanaa.