Usidanganywe na Miguu ya Tembo...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usidanganywe na Miguu ya Tembo...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Aug 28, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Inakaribia saa sita za usiku hapa Iringa. Kabla sijafunga kazi zangu za usiku huu nimeona niseme japo neno fupi la usiku huu.

  Ndio, nimelipitia jarida la kila wiki ( Pichani) . Limesheheni vichwa vya watarajiwa Urais 2015. Inahusu Urais 2015. Si mnajua, Watanzania hatuna ndoto ya taifa, nyingi ni za vyeo tu, ikiwamo Urais.

  Na Urais Bongo ni vita, tena si ya mchezo. Na kwenye vita kuna ya muhimu haya; Uwanja wa vita kwa maana ya uwanja wa kupigania. Kuna mikakati, kuna makamanda wa vita na wapiganaji. Lakini, vita pia ni sharti iwe na malengo.

  Ndio, babu yangu alipata kuniambia; porini usidanganywe na miguu ya tembo. Tembo ni mnyama makini sana. Unaweza kuifuata miguu ya tembo ardhini ukadhani unayemfuatilia ni tembo mmoja. Hapana, tembo hukanyaga nyayo za tembo aliyemtangulia. Nyuma ya tembo mmoja yumkini kuna tembo mia moja.

  Inahusu Uongozi pia, leadership. Nyuma ya kiongozi mmoja yaweza kukawa na kumi wanaomfuatia nyuma yako. Mzee Kenyatta alitamka; " Fuata Nyayo!"- Na kwa tembo ni " Kanyaga Unyayo!"

  Naam, usidanganywe na miguu ya tembo, ukadhani ni mmoja, kumbe wako mia moja.

  Na hilo ni Neno Fupi La Usiku Huu.

  Alamsiki.
  Maggid,
  Iringa.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  haya kaka tumekupata sana kwa neno la leo usiku...:israel::israel::israel:
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 4. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo hakuna rais labda RAHISI.ni pombe mpya kwenye viriba vya zamani.kwa kujipendelea hao!!!!!!
   
 5. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hayo ni maoni yako ni jinsi ya utashi wa kibinadamu, lakini nataka kukuhakikishia safari hii watanzania wamechoshwa na hali hii inavyoendelea katika nchi yetu.

  Kila kukicha hali ya maisha ni ngumu afadhali ya jana viongozi wakiingia madarakani wanabadilishwa na mfumo mbovu wanaoukuta na wanalazimika kuufuata hata kama ni wa upotoshaji. Sidhani kama kiongozi yeyote anayewania uongozi kwa nguvu na uwezo wake bila kumtegemea Mungu anaweza kuenenda kwa njia sahihi bila kuwafuata wale aliowakuta.

  Imefika mahali ambapo watanzania wameelekeza kilio chao kwa Mwenyezi Mungu naye ametenda kazi, leo tunashuhudia viongozi walioko madarakani wanashikana uchawi, wewe ulifanya hivi wewe ulifanya vile,wewe ukimwaga mboga mimi namwaga ugali nk nk. kwa hiyo wameendelea kuwa na malumbano ya jinsi hii hata wanapokuwa katika ukumbi wa bunge letu tukufu, wanaendeleza malumbano yasiyokuwa na mashiko kwa wananchi kiasi kwamba sisi wananchi tumekata tamaa.

  Wakiwa huko bungeni wanapayuka payuka tu wamemsahau mtanzania, wameshau makundi yanayotaabika katika jamii kama walemavu,watoto wa mitaani, wamesahau wafanyakazi wanaoteswa na waajiri wadhalimu wanaoitwa wawekezaji kama sio makabaila, wamewasahau walimu wanaotusomeshea watoto wetu walalahoi,wamewasahau wauguzi wanaotutibu sisi walalahoi.

  Wanajipendelea wao kwa kujiongezea maslahi yasiyo halali kwa kutumia kodi zetu, wanajitibia wao na familia zao katika hospitali bora kama sio hapa basi ulaya kwa kutumia kodi zetu, wanasomesha watoto wao kwenye shule bora na hata ulaya kwa kutumia kodi zetu, wananunua na kutumia magari ya kifahari kwa kodi zetu.

  Nionavyo raisi ajaye ni yule atakayepatikana kwa msaada wa Mungu, kilio cha mtazania kimejibiwa.Tayari wenye macho ya rohoni tumeshajua, hao wengine watabaki kuwa wakosoaji wasio na tija.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 6. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,371
  Likes Received: 630
  Trophy Points: 280
  Kina kajura na sheikh yahya wako na huyo jamaa aloandika newspapers. Liwalo na liwe, rais bora atachaguliwa kwenye ballot box na watanganyika walio majority ila tumtangulize mungu tumpate walau mcha mungu anayejua taabu za wa2 wa kawaida.
   
 7. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nawashauri kila mtanzania atakayekwenda kupiga kura mwaka 2015 awaze yafuatayo kichwani mwake ndipo akachague CCM na serikali yake au Chadema na M4C yake.

  1.Maisha magumu kwa walala hoi
  2.Mbwa wa mwekezaji pale kahama alipofanyishwa mapenzi na mwanafunzi wa darasa la tatu chini ya uangalizi wa polisi
  3.Dhuluma na kashfa ya serikali kwa wananchi wa nyamongo
  4.Mauaji ya watu kwenye mkutano wa CDM pale Arusha,Morogoro,Mwanza,Iringa na Mbeya
  5.Walimu kufutwa kwenye sensa eti kwasababu ya mgomo
  6.Vifo vya watu mahospitalini kwasababu ya mgomo huku wabunge wa CCM wakifurahia Bungeni na chadema wakilaani
  7.Kupigwa ulimboka na Serikali kufurahia na Nape kuukejeli umma wa wawatanzania
  8.Wizi wa kina lowasa,Chenge,Rosta,JK,Ridhiwani,Ngeleja,Maige na wizi wakutisha pale Tanesco
  9.Wizi wa wanyapori uliofanywa pale KIA
  10.Wizi EPA
  11.Utoaji Ajira serikalini kwa kufahamiana kwa familia za viongozi tu
  12.Bomoabomoa nyumba za watu kwa kubeba wawekezaji kama pale njedengwa Dodoma
  13.Kuuza Ardhi ya madini ya watanzania kwa wawekezaji unaofanywa na Chama na Serikali ya CCM
  14.Kutoa mikopo kwa upendeleo wa familia za viongozi wa CCM na kuwatupa walalahoi wa nchi hii
  15.Rushwa ktk ugawaji vitalu vya uwindaji kwa wazawa na kuwapa wageni
  16.Kuwapa wahindi na warabu uongozi ktk tanzania kupitia tiketi za CCM ambapo hakuna mwafrika mwenye uwezo wa kuwa hata mjumbe wa nyumba mbili india au uarabuni na kwamba wote hawa wapo CCM na sio chadema
  17.Ajira kukosekana kutokana na kuua viwanda na kuwapa wahindi na waraabu na kugeuza watz kuwa manamba wao
  18.Kufeli watoto wetu na watoto wa wakubwa wa CCM na serikali wakienda Ulaya na kurudi kutuongoza watz.
  19.Udini uliopandizwa na JK na serikali yake unavyotishia maendeleo ya Taifa hili,,,,
  CHAGUENI HII LEO NINYI MTACHAGUA CHAMA GANI...MIMI NA NYUMBA YANGU YOTE TUTAICHAGUA CHADEMA....
   
Loading...