Nimelelewa katika
familia ya kumcha Mungu. Sijawahi kumuona baba, mama, bibi, babu, au
mjomba akienda kwa mganga. Ila dunia ilinifikisha na kunifundisha kwenda
kwa mganga.
Katika kukabiliana na matatizo ya dunia aliyoniusia mama kwamba "Naka
kua uyaone ya dunia" nilijikuta nimekabiliwa na tatizo la kimapenzi
ambalo lilinikondesha kwa siku 3 kila nipitapo watu walikuwa
wananishangaa. mama yangu alilia sana asijue ni kipi kilinisibu ila
kamwe sikufungua mdomo kuelezea nini tatizo. Nilisugua kichwa bila jibu.
Asubuhi ,moja shetani akanipa wazo la kwenda bagamoyo kutafuta mganga
(ilitokana na maelezo ya watu kuhusu uganga na bagamoyo) .Sikujua hata
ni wapi kuna mganga ila nilielekea mwenge kupanda gari nisijue hata
nitashukia wapi. Nikapata wazo la kumuuliza conductor kama anajua mganga
yeyote huko bagamoyo. Alisema nisiwe na tabu.
Tulifika bagamoyo akanielekeza kwenye mganga. niliefika nikaambiwa
nianda 40,000 kwa ajili ya vifaa kama nazi, kuku ubani, kitambaa cheupe,
n.k. nilishuhudia nazi zikivunjwa na kuokotwa kwa ajili ya kitoweo.
Kuku alichinjwa bila kuchelewa mke wa mganga akaja kumchukua huku akiita
watoto wachemshe maji tayari kwa kunyonyonyolewa. Wakati wa kuondoka
nilipewa dawa inaitwa mlipu na maandishi ya kiarabu eti nikachome nikiwa
naongea yale nitakayo.
Nilirudi mtaani badala ya tatizo kupungua ndio lilizidi mara 20 zaidi.
Nikakata tamaa, ikabidi nimpigie tena yule kondakta (nilichukua namba
yake). Alinielekeza mganga mwingine karibu na kawe beach. Mambo yakawa
ni yale yale mwisho nikaagizwa mwingine wa kunduchi ambae na makalio
huwa anashika (wengine hadi wameliwa papuchi) yakawa ni yale yale.
Katika mishe nilipatamarafiki wenye matatizo mbali mbali team ikaundwa .
Tulipata twende kunduchi beach yupo mganga mwingine ila mafanikio
yalikuwa ni sifuri.
Kote huko hela zinaliwa tena hadi laki 2 kwa mganga mmoja.
Safari ya mwisho ilikuwa ya tandika ambapo nilijiambia nisipofanikiwa
bhaaaaaasss. Huko nilikutana na waganga 2 mwanamke na mwanaume dawa
walizotoa ni zile zile ila waliongezea nipeleke nywele za mhusika,
nguo/uzi wa nguo yake, na mabaki ya chakula kwenye sahani aliyokula. Pia
nilkipewa maji ya kumuwekea kwenye chakula na mengine niweke kwenye
maji yangu ya kuoga. Mafanikio hayakuwepo pia.
Mwisho nilijuta sana na kumrudia Mungu kwani niligundua uganga ni
utapeli. Toka nilipoamua kumrudia Mungu nilipata amani ya kweli na afya
yangu ilirudi. Niliamua kupotezea lile tatizo na nililikubali.
Ni kipi ninataka kuwausia:
1. Waganga wengi ni wezi na waganga njaa hivyo kwenda kwao ni kutafuta
kuibiwa
2. Asilimia kubwa dawa ni zile zile hivyo kupita kuzunguka ni
kujichosha.
3. Nilikutana na wachaga na watu mbali mbali. shida ya mchaga ilikuwa
kuvuta wateja , kupata hela ila wenzangu na mimi tulipelekwa na ishu za
mapenzi. angalau mchaga alienda kimaendeleo
4. Wanawake wengi huenda kwa waganga tatizo kubwa likiwa mapenzi. kote
nilikopita 99% ya wateja ni wanake tatizo kubwa mapenzi. wenye sura
nzuri shepu na walio kawaida. hili ni fundisho kwamba shida ya mapenzi
ni kwa wote mapenzi hayana ufundi wala mwenyewe. kama unaoa muombe Mungu
sana.
5. Hakuna jipya chini ya jua. ni ubatili na kulilisha upepo. nimemrudia
Mungu ni baraka kwa kwenda mbele na amani ya kweli
6. Waganga wengi wa darisalam wana bei kuliko mikoani hii ni kwamba dar
kuna hela ndefu ni kama bei za nyumba dar zilivyo juu kuliko mikoani.
7. Never say never. kabla hujafa lolote linaweza kukufika na ukajikuta
unafanya usilotegemea.
Mwisho usidanganywe ni wizi mtupu.
Mungu anatosha