Pombe ya mbege ni kinywaji maarufu sana katika jamii wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, haswa Wachaga, Wameru na Waarusha.
Ni pombe inayotengenezwa kwa juisi iliyosindikwj na kuchachushwa ya ndizi na unga wa ulezi.
Mbege sio pombe tu bali pia hutumika kufanyia mitambiko ya kimila. Teknolojia ya kutengeneza Mbege iligunduliwa Kibosho na ilienea taratibu maeneo mengine hasa nyakati za vita vya kiukoo vya wa Mangi na wachili.
Mbege ni kati ya vitu vilivyounganisha sana watu, kwani nyakati za kale na hata sasa kidogo, kikombe au kata moja ya mbege ilikuwa inanywewa na watu wengi kwa mstari. Mmoja akipiga gulps (nguchu) kadhaa anampasia mwingine hivyo hivyo hadi wa mwisho na kisha wa mwisho anarudisha tena kule ilitoka hadi iishe.
Mbege ni pombe inayoweza kunywewa popote na yeyote. Iko vizuri sana.