Usichojua kuhusu pombe ya Mbege

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Pombe ya mbege ni kinywaji maarufu sana katika jamii wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, haswa Wachaga, Wameru na Waarusha.

Ni pombe inayotengenezwa kwa juisi iliyosindikwj na kuchachushwa ya ndizi na unga wa ulezi.
Mbege sio pombe tu bali pia hutumika kufanyia mitambiko ya kimila. Teknolojia ya kutengeneza Mbege iligunduliwa Kibosho na ilienea taratibu maeneo mengine hasa nyakati za vita vya kiukoo vya wa Mangi na wachili.

Mbege ni kati ya vitu vilivyounganisha sana watu, kwani nyakati za kale na hata sasa kidogo, kikombe au kata moja ya mbege ilikuwa inanywewa na watu wengi kwa mstari. Mmoja akipiga gulps (nguchu) kadhaa anampasia mwingine hivyo hivyo hadi wa mwisho na kisha wa mwisho anarudisha tena kule ilitoka hadi iishe.

Mbege ni pombe inayoweza kunywewa popote na yeyote. Iko vizuri sana.
 
Basi sawa nimeijua
 
Kwa ufupi ni mataputapu kama kindi, komoni na wanzuki.
Uliposema wanzuki umenikumbusha mbali sana. Morogoro waligundua pombe moja hivi wakaipa jina la LUKANGE WINE kutoka na eneo husika hujulikana kma lukange, hiyo pombe kabla hujanywa lazima uwe na kamba kwa ajiri ya kufu ga kwenye suruali, kwenye kifundo cha chini cha mguu.
Principle za hizo pombe unapokunywa lazima ujinyeee, basi mtaaani ikifika mida jioni utaona watu wameshikilia kamba wanakwenda kunywa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah hii pombe nimewahi kunywa kwa pupa wakati nilikuwa sijawahi kuitumia na nilikuwa dogo sana.....huyo mtengenezaji alikuwa mchaga na mkewe na ilitokea alinipenda sana,sasa nilikunywa ya kutosha nililala kwake tangu around saa tisa hadi kesho yake na walishindwa kuniamsha
 
Uchagani kulikuwa hakuna vita vya kiukoo..Mangi atapiganaje vita na Mchili!!?
Hapo umechanganya madesa.
 
Uliposema wanzuki umenikumbusha mbali sana. Morogoro waligundua pombe moja hivi wakaipa jina la LUKANGE WINE kutoka na eneo husika hujulikana kma lukange, hiyo pombe kabla hujanywa lazima uwe na kamba kwa ajiri ya kufu ga kwenye suruali, kwenye kifundo cha chini cha mguu.
Principle za hizo pombe unapokunywa lazima ujinyeee, basi mtaaani ikifika mida jioni utaona watu wameshikilia kamba wanakwenda kunywa

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona unazungumzia pombe iitwayo PINGU?
 
Back
Top Bottom