Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,791
- 31,803
USIA WA MAREHEMU KITWANA SELEMANI KONDO KWA WATANZANIA
Mohamed Said May 24, 2017 0
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999
Mohamed Said February 17, 2015 0
Annur Na.187- Feb.5-11, 1999
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma
Kitwana Selemani Kondo
Mh. Kitwana S. Kondo: Mheshimiwa Spika, naomba nikushuru sana.
Mheshimiwa Spika, naomba na mimi nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa hotuba yake aliyoitoa tarehe 4 Novemba, 1998 hapa Bungeni. Hotuba hii Mheshimiwa Spika ina ukweli, ina usahihi na pia ina uungwana. (Makofi).
Mimi nataka ninukuu vifungu viwili katika hotuba hii, navyo ni vifungu vya mwisho. Lakini kabla sijafanya hivyo, nataka nimwambie rafiki yangu, mpenzi wangu Dr. Msina kwa manung’uniko yake ya mambo aliyofanyiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, mimi ninazo habari na sio mimi tu, watu wengi wanazo habari kwamba Wasukuma na Mkuu wa Mkoa wa Tabora ni Msukuma na Wanyamwezi na kidogo Wadigo wana tabia ya wizi. Kwa hiyo yaliyomkuta ni mahali pake. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ningependa sasa niende kwenye vile vifungu nilivyosema kuwa nitavinukuu. Katika hotuba hii ya Mheshimiwa Rais, mwisho inasema hivi, "Mheshimiwa Spika, baada ya miaka mitatu ya Urais, nathubutu kubadili maneno ya msanii mashuhuri wa visiwani, Siti bint Said na kusema Tanzania ni njema atakaye na aje. Nchi yetu Mwenyezi Mungu ameibariki sana. Ni nchi ya umoja, amani, upendo, bashasha, ukarimu uliopindukia. Ni nchi ya wapenda usawa na haki. Umoja wetu wa Kitaifa unatokana na imani yetu ya dhati juu ya usawa wa binadamu mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya sheria. Umoja unaoimarishwa na sera sahihi za kujenga jamii na kuandaa mazingira ya maendeleo ya haki, amani na utulivu kwa wote". (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya hapo, Mheshimiwa Rais anaendelea. Anasema hivi, "Umoja unaotahadhari sera, kauli, tabia na vitendo vinavyoweza kupanda mbegu za mfarakano, chuki na kutoaminiana miongoni mwa Watanzania". Ningependa niyarudie maneno haya. "Umoja unaotahadhari sera, kauli, tabia na vitendo vinavyoweza kupanda mbegu za mfarakano, chuki na kutoaminiana miongoni mwa Watanzania. Umoja unaolindwa kwa vita vya kudumu dhidi ya ukabila, udini, ubaguzi wa rangi, jinsia au majimbo".
Mheshimiwa Spika, miaka mingi iliyopita, kwenye 1658 A.D. Mtu mmoja Galileo alisema, "Dunia ni mviringo". Makuhani wakamwambia huyu anakufuru, akashitakiwa akahukumiwa kuuawa na akachomwa moto. Leo Galileo amekuwa Vindicated. Kwa bahati mbaya Galileo mwenyewe hayupo kujua kwamba amepata Vindication. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninachotaka kusema ni hiki cha umoja unaotadhari sera, kauli, tabia na vitendo vinavyoweza kupanda mbegu za mfarakano. Nimesema mara nyingi hapa kwako. Mheshimiwa Rais, hivi karibuni aliwahutubia Waislamu kwenye Baraza la Idd, akawaambia kwamba manung’uniko yao na malalamiko yao yote atayatazama na atayashughulikia akishirikiana na Baraza lake la Mawaziri.
Sasa nina mambo mawili au matatu ambayo nataka kuyasema ambayo yanaweza kuleta mfarakano. Yanapandwa na serikali. Moja, karibuni hivi katika mwezi wa Ramadhani, mwezi wa Ramadhani kwa Waislamu ni mwezi Mtukufu, ni mwezi wa toba.
Wale jamaa zangu wasiojua toba ni mwezi wa kurudi kwa Mungu. Wakati wa ukoloni na mimi nilisoma wakati wa Ukoloni mwezi wa Ramadhani shughuli zote zinafungwa, baadaye kwenye serikali yetu wenyewe shule hazifungwi. Lakini baada ya muda wanaachiwa watoto kurudi majumbani kwao au kwenda kwenye mabweni. Lakini mwaka jana na mwaka huu serikali ikaamua kuwa mitihani ya watoto wa kidato cha nne ifanywe mwezi wa Ramadhani na iendelee mpaka siku za Idd. Hiyo ni moja ya cheche za mifarakano.
Kwa Rehema ya Mungu Alhamdulillah, baada ya kunung’unika Waislamu, Waziri wa Elimu na Utamaduni alitoa maelezo. Maelezo yale yakawaridhisha Waislamu na Mheshimiwa Rais akakubali kwa siku za Iddi, watoto wasifanye mitihani na haikufanywa mitihani. (Makofi)
Lakini mimi ninalouliza ile sababu ya kuamua mwezi wa Ramadhani ifanywe mitihani ni nini? Ni Insensitivity, ni jeuri, ni kiburi, kwa sababu kuna wengine ambao ni wazito tuliwasikia wakisema, wakitaka kufanya mtihani na wafanye hawataki basi. Mimi nasema watu kama hao ndiyo watu wasioitakia kheri nchi hii. Siyo sisi tunakuja kusema hapa hadharani. Hao wanaosema wakitaka kufanya na wafanye na hawataki kufanya basi. Hao ndio wasioitakia kheri nchi hii. (Makofi)
La pili, linaloweza kuleta mfarakano ni tabia ya serikali ya kuchelewesha makusudi kuandikisha taasisi za Kiislamu. Taasisi yoyote ya Kiislamu ikitaka kuandikishwa serikalini itachukua miaka miwili au mitatu. Sababu hazitolewi, hata kama kuna uchunguzi, watu waende wakatafute habari kwa nini inachukua miaka miwili, miaka mitatu?
Mheshimiwa Spika, nilipata kusema hapa kwamba mimi ni mlezi wa Baraza la Maimamu Tanzania. Tumeomba Baraza la Maimamu kuandikishwa, sasa ni miaka mitatu, sababu haijulikani. Wengine kila wakiomba wanasema lazima kipatikane kibali toka BAKWATA. Leo ningependa nijue ipo sheria inayosema hivyo? Au ni matakwa tu ya wakubwa? Hilo la pili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la tatu, Sura ya 33 Aya ya 30 na ya 31 ya Qur’an inamtaka mwanamke akifika umri wa miaka 9 avae hijabu. Hijab maana yake avae nguo ya mikono mirefu, avae shungi, avae gwanda zuri na avae suruali inayoficha mapaja na mpaka magoti. Mimi najua ya kwamba serikali imetoa agizo kwa watoto wa shule kwamba wafanyiwe hivyo wale wa Kiislamu wanaotaka, sheria zote zinavunjwa. Dini ya Kiislamu inakataza pombe, Waislamu wanakunywa pombe. Sasa hilo anafanya mwenyewe.
Lakini ninajua pia ya kwamba kuna shule nchini huku, kuna viongozi wa Idara ya elimu ambao wanakataa kutekeleza sheria hii au agizo hili na serikali imekaa kimya, nataka nijue ni kwa sababu gani? Tujue ni kwa nini. Hii ni amri ya Mwenyezi Mungu na serikali, Rais anasema tusifanye chochote kinachoweza kuleta mifarakano.
Mheshimiwa Spika, lingine ni kwamba huu mwaka wa 30 wa uhuru. Siku ya Ijumaa ni siku muhimu kwa Waislamu kama ilivyo kwa siku ya Jumamosi ni siku muhimu kwa Wasabato kama ilivyokuwa siku ya Jumapili ni siku muhimu kwa Wakristo wengine. Lakini siku ya Ijumaa ingawa kuna agizo la serikali kwamba Waislamu waachiwe waende wakasali. Kuna viongozi siku ile ndiyo siku ya kufanya Board Meeting, ili kumzuia Mkurugenzi ambaye ni Muislamu ambaye anapenda kazi yake aogope. Shule zinafungwa saa 7. Jumapili vitoto vidogo vidogo vya Kikristo vinakwenda kusali. Jumamosi vitoto vidogo vidogo vya Kikristo vinakwenda kusali. Siku hizi vitoto vidogo vidogo vya Kiislamu vinataka kwenda na wazazi wao. Naomba utaratibu ufanywe wa dhamiri kabisa kwamba Ijumaa saa 6 kazi basi kwa Waislamu. Wale wanaofanya Board Meeting waache wafanye saa 8, wafanye saa 9 na shule zote za Primary na Secondary zifungwe saa 6 ili kuwapa nafasi watoto wa Kiislamu waende wakasali.
Mheshimiwa Spika, nina mengi lakini nitakuambia mwisho. La mwisho, Rais aliwaambia Waislamu wote pale Dar es Salaam kwamba atalishughulikia suala la elimu. Lakini akawashauri kwamba wale wafadhili ambao hivi sasa wanatujengea Misikiti wajenge pia shule. Hilo jambo zuri, na Waislamu wamelisikia na ninajua ya kwamba Waislamu wanataka hivi karibuni kumwendea Rais kwenda kumshukuru. Ila nina jambo moja, natoa mfano wa Dar es Salaam, Waislamu wanafikia asilimia 70 au zaidi. Kwenye magereza Dar es Salaam wengi kuliko Wakristo au watu wengine. Hawa wengi, hawana kazi, jela watakuwa wengi. (Kicheko)
Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu. Asilimia 29 ni wengine. Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21. Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe. Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.
Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu. Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga. Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha. Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini.
Mheshimiwa Spika, Rais Mkapa anawasaidia Waislamu. Tulimwendea, mimi mmojawapo kwa mambo mengi ambayo ameyashughulikia. Nina hakika ya kwamba mambo haya tuliyoyasema na aliyoambiwa na viongozi wa Kiislamu kule bungeni atayashughulikia. Lakini ninaamini kabisa ya kwamba hataweza peke yake bila ya msaada wa viongozi wangu hao walioko hapa. Wakisema hawa kwamba ndiyo kawaida yao hiyo. Atapata tabu Rais wangu.
Mheshimiwa Spika, kengele ya pili imelia. Nashukuru sana. Lakini nataka niseme kwamba haya niliyoyasema, nasema kwa sababu najua mimi kwamba suala hili la mfarakano ni suala kubwa. Penye mfarakano hakuna maendeleo. Penye mfarakano hakuna cha uchumi. Kwenye mfarakano kuna ghasia. Kwa kuwa Rais ameomba tufanye kila jambo mfarakano usiwepo, basi serikali imsaidie Rais katika kutekeleza wajibu wake kwa makundi yote ili pawepo na usawa. (Makofi)
Kitwana Selemani Kondo akifanya kipindi cha televisheni (TV Imaan) ''Walioacha Alama Katika Historia,'' nyumbani kwake Upanga tarehe 12 Septemba, 2012 akihojiwa na Mohamed Said