Usalama wa Tanganyika utakua mdogo sana kama Zanzibar ikijitenga, Tuko tayari kushare nao keki ya Tanganyka kwa ajili ya maslahi mapana. Kama Zanzibar ni ndogo kwa nini ijitenge?Wewe Nape huko Zanzibar huna tofauti na Mkenya
Huwezi kumilikishwa ardhi ya aina yeyote
Huwezi kuajiriwa kwenye serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Huwezi kuomba nafasi yeyote ya kugombea huko kama ambavyo unaweza ukajaribu kwenye jimbo lolote huku Bara
Sasa kwa nini tuendelee kuwa watumwa wao?
Kwa nini hamridhiki na Tanganyika yetu?mbona Rwanda na Burundi ni nchi ndogo kama baadhi ya mikoa hapa kwetu Bara lakini wamejikubali?
Bila kuungana na Zanzibar Tanganyika haiwezi kusimama?
Hebu fungukeni zaidi mtueleze agenda za siri za Muungano huu mnaoung'ang'ania manake sidhani kama zimeshawahi kuwekwa wazi asilani
Tanganyika kwanza,Tanzania baadaye