Usia kwa viongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usia kwa viongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lusajo, Apr 1, 2009.

 1. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimeiwaza hii kitu baada ya kukumbuka maneno ya Mheshimiwa, Mtukufu wetu wa zamani, aliyekuwa Raisi bwana B.W Mkapa ya kwamba Watanzania ni wajinga. Yaani nikawaza mimi, baba na mama, babu na bibi na watoto wangu ni wajinga! Kweli!?
  Lakini kwa upande mwingine nikawaza kwamba ilimchukua Mandela miaka 27 jela, lakini alikuja kuwa Raisi wa SA, Iliwachukua wamarekani miaka 40+ baada ya kifo cha MLK kuja kumchagua Raisi mweusi na mpaka leo bado nasubiri kurudi kwa Yesu, kwa hiyo subira ninayo kwa sababu najua yote haya yana mwisho.
  • Kwako B. W Mkapa najua Soon and very soon yoote haya yatakwisha na wezi na mliofanya uhujumu uchumi woote kuanzia ambao mnajiona mna kinga (Mkapa) na wasio nayo watawekwa ndani tuu. Na najua hii kitu itatokea in my life time. Ni viongozi wengi sanasana wa Afrika ambao wanajiona wenyewe ni invisible na wanaona wananchi wao ni wajinga, lakini poaa tu acha niwe mjinga sasa hivi ila hapo baadae tutajua mjinga ni nani kati ya mimi na wewe.Nadhani umewaona ndugu zako ambao kuna mmoja alikuwa analazimisha ufisadi hata kama wananchi watakula nyasi! najua siku si nyingi tutaona nani atakula nyasi, hata kama safari hii ni danganya toto kwa ajili ya uongozi wa sasa kushinda uchaguzi wa 2010, lakini najua itafika siku itakayokuwa sio danganya toto, itakuwa reality kwa sababu it just a matter of time wataona ukweli. Maana kuna watu hawakuamini kama itatokea hivyo na haya mambo mengine ya uhuru wa vyombo vya habari na blogs na internet kwamba vimeletwa na Kikwete, inawezekana ni Raisi Kikwete ndio lakini na yeye hana choice kwa sababu ni suala la muda, sio Rocket Science haya mambo yanakuja na muda.
  • Kwako Mama A. Mkapa mengi yamezungumzwa juu yako (Ufisadi wako) kama ni ya kweli shauri yako nadhani umemuona Mama Chiluba na yeye aliwekwa na mumewe na kama wewe umeiba za mwizi 40 mama.
  • Kwako Mhe Raisi J. Kikwete kama wewe sio fisadi (keep it that way) najua ukisimama tena 2010 utashinda tuu (tutake tusitake) na wengi wenu (viongozi) huwa mnajisahau katika kipindi cha mwisho na huwa manafanya mambo ya kuiba au kuruhusu rafiki zenu kuiba kwa niaba yenu. Please please usifanye ufisadi kwa sababu wewe sio invisible na utakuja kukamatwa kumbuka "Za Mwizi _____"
  • Kwako Mama S. Kikwete sijawahi kusikia usisadi wowote ambao umeufanya zaidi ya ile safari uliyotumia ndege yetu (walipa kodi), naomba uendelee hivyohivyo na kumbuka huna haja ya kuiba kwa sababu inaeleweka wewe na familia yako kama mke wa raisi mtaendelea kuangaliwa na hela za walipa kodi, cha kufanya ni sisitiza elimu kwa wanao woote maana ndio itakuwa mkombozi wao. Ila ukiiba Mama utakamatwa tuu.
  • Kwako Rostam Azizi, Lowasa and the like. RA unaweza ukawa "Kingmaker" sasa hivi lakini shauri yako (Nadhani umewahi kusoma history kwamba kuna falme nyingi tuu ziliangushwa), angalia soon usije ukawa kingmaker wa Keko au Ukonga. Nitakachokushauri kama uliiba hela zetu (walipa kodi) na bado unazo bora uanze kujenga magereza vizuri kwa sababu najua utakuja kuishia huko, sidhani kama vilio vya wananchi vitaishia njiani (siku itafika tuu)
  • Kwako Mhe. Mwakyembe, Mhe. Mama Kilango and the like. Kama mko upande wa wananchi (Keep it that way). Lakini mkiiba kwa kujidai nyie ni wazalendo na kujificha huku mkijidai ni watetezi wa wananchi kwamba mnapinga ufisadi ila mnaiba, ole wenu, kumbukeni ni suala la muda tuu, kama mmeiba muda wa kukamatwa utafika tuu. Endeleeni kutetea wananchi ila msije kufanya ufisadi.
  • Kwako Mhe. Masha, Zitto na kuna wengine ambao ndio mnaitwa vijana. Muda utafika mtashikana mashati kwa hiyo msijisahau hata kidogo na kama hamjafanya ufisadi nawashauri msije fanya hata siku moja. hapa kwa Mhe. Masha hata siku moja sijawahi kusikia habari yoyote nzuri uliyoifanya ukiwa kama waziri wa mambo ya ndani. Unaweza ukasema una haters na vyombo vya fulani vinakuonea, ila kuna magazeti mengi tuu na kama utafanya kazi yako ipasavyo tutasikia habari nzuri kutoka kwako, nadhani unamuona Mhe Pinda na unaweza kujifunza kwa Waziri wa mambo ya ndani wa zamani A.L Mrema enzi zake tulikuwa tunasikia mengi mazuri aliyoyafanya kwa hiyo yalikuwa yana offset mabaya yake. Tunaokulipa (Walipa kodi) tungependa kuona unafanya kazi sio kutetea mashirika fulani fulani tuu.
  Nimejaribu kutokumuita mtu yoyote fisadi kwa sababu wanasema bado hamjapelekwa mahakamani kama kweli mmefanya makosa, lakini kama nilivyosema kwamba msijali muda utafika tuu. Kwa sababu mafisadi manajijua tuu na mambo mengi yameshasemwa juu yenu na kumbukeni za mwizi ni 40 (kuna mifano Chiluba, Mobutu, na kuna wengine wamefanya ufisadi wa aina tofauti lakini wanakamatwa mmoja baada ya mwingine)
  Niliwahi kuambiwa Jamii Forums ni watu walio nyuma ya Computer wanapiga kelele tuu (usiku wanalala), lakini kumbukeni kwamba hapa kuna watu wa aina mbalimbali wazee kwa vijana, na kuna kizazi kijacho na viongozi wajao wanaosoma mengi juu yenu na ufisadi wenu na najua watakuwa na machungu kwamba hamjawaachia kitu na mnawaita wazazi wao "wajinga" sasa sidhani kama watakubali hilo.
  Niliwahi kuambiwa Internet inafikia wa-Tanzania wachache sana lakini mkumbuke kwamba haiitaji watu 100 kuanza kupambana, wale wachache wanaojua what is going on ndio watakaokuwa viongozi wa kuinua mawazo ya wale wasio na internet.
  Wana JF naomba muendelee kutoa usia, maonyo kwa kiongozi yeyote yule unayedhani atahitaji hilo.

  Ni mimi, Mtoto wenu, mdogo wenu, kaka yenu, baba yenu, rafiki yenu LUSAJO
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .......keep it up Lusajo......ni vema kuwaambia.......tusije laumiana mbele ya safari..........
   
Loading...