Ushuru wa magari yalitumika na fire fee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushuru wa magari yalitumika na fire fee

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by dkn, Aug 5, 2012.

 1. d

  dkn Senior Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sheria mpya iliyopitishwa wakati wa bajeti ya Wizara ya Fedha, serikali ilibadilisha mfumo wa ulipaji kodi kwa magari chakavu yanayoagizwa nje ya nchi. Ili kuwa sambamba na East Africa Community kwa suala hili, Kenya ilishinikiza nchi wanachama kufuata mfumo wa Kenya ambapo Tanzania iliridhia wakati Uganda ikiwa haikubaliani na hilo. Jambo la kushangaza Serikali ya Kenya inazuia uingizaji wa magari chakavu yaliyo na umri wa miaka 8 na Tanzania imekubaliana na hili ingawa bado inaruhusu magari yenye chini ya miaka 8 kwa kutoza kodi zaidi wakati Kenya HAIRUHISIWI kabisa na hakuna kodi za namna hiyo. Tanzania itakuwa dumping ya magari chakavu kwa tamaa ya pesa ya ushuru ambayo haikidhi maana ya kuweka miaka 8. Anayenunua gari ya mwaka 2004 kwa mfano analipa depreciation ya 60% na gari lenyewe litakuwa na gharama zaidi kulinganisha na gari ya 2002 ambayo depreciation ni 80% hata kama atalipa ushuru wa uchakavu. Mantiki ya kuweka miaka 8 na kuendelea kukubali kuingiza magari chakavu kwa ushuru haina maana kama tulitaka kufuata mfumo wa Kenya ambao maana kubwa ni kuzuia nchi zetu zisiwe dumping countries za mataifa ya nje na pia kuzuia ajali za magari yaliyotumika kwa muda mrefu, carbon emission kwa magari ya kizamani na kuwa na magari efficient kwenye fuel na less in carbon emissions.
  Magari chakavu yasiwe classified kama commercial on non-commercial inapokuja kwenye safety, mfano saloon car iwe miaka 8 na hata malori na magari ya abiria hakuna sababu ya kuingiza gari la 1990 kubeba wanafunzi au abiria kupewa leseni kwakuwa umelipa kodi ya uchakavu. Mara nyingine tunasema watu wa uwezo wa chini hawataweza kununua magari kama haitaruhusiwa kuingiza magari yenye umri mkubwa, hili halina mantiki kwa mtumiaji ukiangalia mbali. Gari chakavu itakuwa na gharama nyingi mfano upatikanaji wa spare parts, matumizi makubwa ya mafuta, gharama kubwa za utengenezaji, uchafuzi wa hali ya hewa. Tutakuwa na uwezo pale ambapo tutaweza kutengeneza magari yetu wenyewe, nchi kama Sudan wana magari yao pia wana contracts za kutengeneza magari ya bei nafuu kutoka China ambayo ni efficient na ya kisasa kulinganisha na magari chakavu kutoka Japan.
  Utaona kwamba serikali yetu wamekaa kutafuta vyanzo vya mapato bila kuangalia matatizo na hatuwezi kushangaa fee ya fire imetokea wapi na hivyo viwango vinalenga wenye magari pekee? Fire extinguisher zingekaguliwa kwa kipindi cha matumizi kama ina expire 2015 na haijatumia (seal kutolewa) basi hizi kodi za kila mwaka zina maana gani? Kama ni kulipa wafanyakazi then zingekuwa absorbed mfano kwenye mafuta au sehemu nyingine, hii inakaribisha rushwa na ningetegemea serikali kuhakikisha kila Wilaya au Kata ina gari la zimamoto kwa majanga ya moto, sijui takwimu zinasemaje kuhusu ajali ya moto kwa magari ukilinganisha na majengo au misitu.. focus kubwa imekuwa ni wapi kwa kuchota hela za haraka wanakimbilia kwenye magari. Serikali wimbo ni ule ule, mapato haya ya magari si sustainable na asilimia ngapi ya watanzania wenye magari, tuangalie vyanzo vingine vya mapato tulivyonavyo na tuondoe rushwa. Rais amesema kuna gesi, hivyo ndiyo vyanzo muhimu vya mapato na misamaha ya kodi iondolewe.
   
 2. mito

  mito JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,646
  Likes Received: 2,033
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama una experience na ununuzi wa magari utakubaliana na mimi kuwa kuna magari kibao tu ambayo yana umri mkubwa (above 8 yrs) lakini ni bora kuliko yaliyo chini ya miaka 8. So to me, bado hatujawa realistic, hata huko kenya haiwasaidii sana barabarani, isipokuwa kwenye makaratasi inaonekana ni nzuri
   
 3. CONSULT

  CONSULT JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  nakubaliana na wewe 100% maelezo ya mkuu hapo juu dkn yanafanana sana na ya kisiasa theoretical aspects, lakini kwenye working ground especially kwenye mazingara yetu kwa maana barabara, mafundi, hata spare parts(thailand,India,China), magari ya zamani ni more efficient-cost effective mbali sana kuliko ya kisasa yenye body za fibre, electronically sophiscated technology,,, nawashauri kabla ya maamuzi ni vema kufanya research, na ndio maana kwa mfano wa daladala dar bado watu wana pendelea kutumia DCM- TOYOTA model ya 20 yrs back sababu kubwa anapata exactly value for money, durable, alot of spares used and new, repairable with simple materials and mafundi, na tangu hapo zamani they dominate about 65% ya service za daladala, hata sumatra hawathubutu kuzizuia NO replacement at all...
   
 4. Kamanda Moshi

  Kamanda Moshi JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,419
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu umeongea point sana, haiwezekan kila mwaka ukakague fire extinguisher ile ile,tena kwa bei ya sh 30,000! Hivi huu upuuzi mpaka lin jaman?zaid hapo ni pesa zinazokusanywa na si zaidi!hebu tutafakari huu wizi, gari moja unalipia Road License , hilo hilo ulipie fire, hapo hawajaja watu wa wiki ya nenda kwa usalama,unalipa tena,halafu kuna mafuta kila ukinunua unalipia,haitoshi barabara kama mahandaki,gari likiharibika juu yako kutengeneza,na mbaya zaid mafuta ya kuchakachua ambayo kila baada ya miez 6 yatakupeleka garage!!aah ukiwa na gar lazima rangi uone kudadeki!
   
Loading...