Ushuhuda wangu mimi baba kijacho

Ushuhuda wangu mimi baba kijacho

Step by step

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
1,190
Reaction score
1,324
Habarini wadau.

Nianze kwa kumshukuru Mungu na kuwashukuru wana Jf waliowahi kunipa mawazo na kunitia moyo.

Pia niwashukuru hata wale walionitumia comment za kejeli na kunicheka.Ishu iko hivi, nilioa na kuishi na wife mwaka mmoja na miezi nane bila wife kushika ujauzito. Ilinichanganya sana sana nikaomba ushauri humu na kupata majibu kibao.

Tulivyoenda hospitali wakafanya vipimo vyote wakasema tuko ok tuwe na subira nikashtukia mpaka mwaka unakufa hakuna kitu.Wife akawa mtu wa kulia na nyumba haina amani tena. Kuna wadau humu wakanishauri nikomae na maombi (sitolitaja kanisa wala mchungaji alonisaidia) manake mtasema promo at work.

Jamani Mungu anajibu tumeenda kanisani siku hiyo kumweleza pastor akacheka sana then akauliza wanangu mlikua wapi siku zote mpaka mnaumia kwa muda wote huo tukamwambia tulikua tunazunguka na hospital.

Pastor akasema mwakani mwezi wa 10 utakuwa na mtoto wako akatuombea bila kumpa hata mia tukaondoka.Baada ya wiki wife kichefu chefu na kutapika kwenda hospital kupima kitu imo am so happy.

Jamani Mungu yupo ila usije ukamsema vibaya mtu mwenye changamoto ya kukosa mtoto najua namna inavyouma. Tumelia sana na mke wangu eti leo tumepokea thanx God
 
Mmemuona Pastor, halafu ndani ya wiki mambo yakajibu?! Huh! Anyway, never mind. Hongera kwenu bro.
 
Mchungaji gani huyo Mkuu

Haisaidii kujua jina la mtumishi, Mungu ndiye atusaidiaye. Mwamini mtumishi lakini Mwamini zaidi Mungu.

"...mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa." - 2 Mambo ya Nyakati 20:20

Nampa hongera mleta mada! Imela, keep on trusting God!
 
Hata mimi ningekuwekea mikono tu mbona mngeenda kupata mtoto?
 
Mimba ya week moja inastua kidogo....

Ila natamani kujua kama Pastor aliishia kwenye maombi tu.........!!!
Hata mimi wasiwasi wangu ni kama Pastor alifanya maombi tu. Na jinsi alivyo-sound excited..."wanangu mlikuwa wapi siku zote".
 
Haisaidii kujua jina la mtumishi, Mungu ndiye atusaidiaye. Mwamini mtumishi lakini Mwamini zaidi Mungu.

"...mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa." - 2 Mambo ya Nyakati 20:20

Nampa hongera mleta mada! Imela, keep on trusting God!

nilikuaga naskia tu watu wanashuhudia miujiza leo kwangu nimejionea. Heshima yangu ilishuka sana na nilikua najiona kama sio mwanaume vile
 
Back
Top Bottom