BALIMI CASTLE
Member
- Aug 2, 2017
- 33
- 47
Miezi 9 iliyopita katika pita pita zangu nilifanikiwa kukutana na binti mmoja mrembo muhudumu wa afya.
Nikaanza kuchombeza chombeza na hatimaye tukazama kwenye dimbwi zito la mapenzi.
Penzi likamea, tukawa tunatembeleana Mara kwa mara,yeye akija kwangu napoishi na Mimi kwenda kwake napoishi.
Kipindi chote hiko tulichokuwa tunatembeleana hatukuwahi kuvunja amri ya sita.
Bila kujua hili wala lile siku moja nikajikuta na hamu sana na mgegedo.
Nilikwenda kwake siku ile visa vya hapa na pale vilianza ili tu,tunda tamu liliwe.
Lakini kilichonishtua,ni pale nilipoona mwenzangu mwitikio wake ni mdogo mno,kadri nilivyokuwa najitahidi kumuhamasisha.
Nikajikuta nakuwa "bored" sana,baada ya kugundua kuwa amenifanya kuwa "bored" akaniambia kuwa kuna kitu anataka kuniambia.
Nikamwambia niambie,akawa anasitasita,basi nikamwambia kama huwezi kunitamkia kwa mdomo nitumie sms nikurahisishie kazi.
Kweli akakubali,akanitumia sms aliyoniambia kuwa ana H.I.V ,alivyoniambia hivyo nikamfariji na nikawa siamini,nikahisi labda anataka kuninyima papuchi.
Mwisho tukavunja amri ya sita bila kinga.Maana kwa muonekano wake aliyokuwa nao yule binti huwezi amini,
Ameumbwa akaumbika kisawasawa.
Siku zilizofuata nikahitaji nithibitishe kauli yake ya kusema kuwa ameathirika,
Nikamshauri tukapime,akaniambia kuwa haitabadilisha majibu,lakini alikubali tukaenda kupima na majibu yakasoma kuwa ni positive kwake na Mimi negative.
Nikajikaza kiume baada ya yale majibu na kutokumuonesha kuwa nimestushwa sana.
Na nikawaza sana kuhusu hali yangu,endapo nikienda kucheki baada ya siku 90 nikawa positive na Mimi.
Kiufupi nilichanganyikiwa sana,kila jambo niliona sina uwezo wa kulifanya,
Nikamuuliza yule binti anaishije,akaniambia anatumia dawa za ARV mwaka wa tano sasa.na kila siku ana Meza dawa.kwa kuwa ni muhudumu wa afya anazingatia masharti ipasavyo za matumizi ya ARV.
Nikawaza sana kupanga foleni ya kupata vidonge vya ARV na kumeza kila siku.
Nikakubali matokeo litakalokuwa na liwe,nikasubiria siku 90 zipite nikaenda kupima nikaonekana sina maambukizi,nikasubiria siku 90 tena nikaenda kupima nikajikuta sina maambukizi.
Kutoka pale nikamrudia mungu,nikaanza mchakato wa kuoa kabisa.
SOMO NILILOPATA
1-Kweli ARV zinasaidia kupunguza maambukizi ya v.v.u,kama asingekuwa mtumiaji mzuri wa ARV ningekuwa nimeshanasa sasa.
2-Huwezi kumjua mwenye v.v.u kwa kumtazama.
3-Kama una uwezo wa kuoa au kuolewa ni heri ukafanya hivyo mapema kuliko kurukaruka,utajikuta unarukia waya wa umeme.
4-ukishindwa kabisa kuoa,kaa mbali na ngono kabisa hadi utakapo oa au kuoelewa.
5-Ukitumia kondomu basi piga vigoli wiwili au kimoja cha kawaida,maana huwa zinapasuka.
6- Ni heri kupima afya kabla ya kugegedana.