Ushuhuda wa kweli wa kilichonipata

Ushuhuda wa kweli wa kilichonipata

Bujibuji we ni rafiki yangu kuanzia leo, coz akili zimekulejea Mie nilikua nakushangaa Kumbe hukuwa wewe

Jaman kwa yeyote aliekosewa na bujibuji kwa comments zake amsamehe coz akili hazikua zake.

Ila kuanzia leo yupo timamu,tumshukuru MUNGU!!! KARIBU JF BUJIBUJI NA AKILI MPYA!!!
 
Bujibuji we ni rafiki yangu kuanzia leo, coz akili zimekulejea Mie nilikua nakushangaa Kumbe hukuwa wewe

Jaman kwa yeyote aliekosewa na bujibuji kwa comments zake amsamehe coz akili hazikua zake.

Ila kuanzia leo yupo timamu,tumshukuru MUNGU!!! KARIBU JF BUJIBUJI NA AKILI MPYA!!!
 
Sikutaka nisimulie kisa hiki hapa JamiiForums , ila kuna msukumo ndani yangu unaniskuma kushuhudia ili mtu mmoja aweze kupokea uponyaji wake kupitia ushuhuda huu.

Mimi Bujibuji Nilikuwa na msichana wangu, hakika tulipendana naye sana. Msichana alikuwa ni mcha Mungu, mzuri, anajiheshimu, msomi na kipato anacho.
Mapenzi yetu yalikuwa motomoto kama mikwara ya USA na North Korea.
Nilienda nyumbani kwa huyu dada na kumposa, nikalipa na mahari tukapanga na tarehe ya harusi.

Nyumba jirani na nilipoishi alikuwa amepanga jamaa mmoja mishen town, yeye na mkewe walikuwa hawana kazi lakini walikuwa wakiishi vizuri kabisa.
Mke wa huyu jamaa alianza kujipendekeza kwangu na kuonesha dalili za kunitaka, kwa kweli sikuwa interested nae kabisa, nilimpenda sana mchumba wangu.
Siku moja nikiwa natoka kwenye matembezi ya jioni, nikakutana na huyu mke wa mtu, akanipiga na leso yake nyeupe usoni, nikashanga sana kwani sikuwa na mazoea naye ki hivyo.

Nikaanza kukifikiria na kukitafakari kile kitendo, kwa kadiri nilivyokuwa nikitafakari, ndivyo hisia za kimapenzi zilivyokuwa zikiongezeka kwa huyu mdada ambaye ni mke wa jirani.

Kwa kweli usiku huo sikulala, nilimfikiria na kuwaza penzi la huyo Mrs. jirani.

Kesho yake asubuhi nikiwa natoa gari nje ili niende kwenye mishe zangu, nikakuta amesimama nje ya gate, eti ana hamu ya kuiona sura yangu.

Nilifurahi sana nikajiona mwenye bahati kuliko kakakuona. Hofu ya mke wa mtu ikapotea, sikumuogopa tena mumewe, na upendo kwa Miss Lady wangu ukapotea na kuyeyuka kama moshi wa njiti ya kiberiti. Chuki, dharau, kiburi, jeuri na roho mbaya viliwaka moyoni mwangu kila iliponijia sura ya mchumba wangu, nilimchukia sana na nikatamani hata WATU WASIOJULIKANA WAMPELEKE KUSIKOJULIKANA kama walimvyomfanyia ndugu yangu mpendwa Ben Saanane.

To make a long story short, mshahara wangu wote, allowances na kila nilichokuwa nikipata nikawa nakabidhi kwa huyo mke wa mtu, nikawa sina pesa, sikuweza kumtunza tena mama yangu wala wadogo zangu, mshahara wangu wote, ambao kwa kweli ulikuwa ni MNONO SANA uliishia kwa mke wa mtu.

Viatu viliisha, nguo ziliisha, gari sikuweza kulimudu tena, mchumba wangu kwa huruma na upendo wake alikuwa akininunulia ngua na viatu na kumpatia jamaa yangu aniletee, huku akitaka nisijue kuwa vimetoka kwake , kwani nilimchukia sana na nilimuona ni mchawi kabisa kama walivyo jichawi , MziziMkavu na Mtu mzito

Kila mtu aliyenifahamu alinionea huruma kwa ufukara ulionivaa, mimi sikuuona huo ufukara, na kwa kipindi chote mke wa mtu alikuwa hajawahi kunipa unyumba, nikiwa nae niliridhika sana kiasi kwamba sikukumbuka kumuomba tendo adhimu la kupeana raha duniani.

Afya yangu ya akili ilitetereka, kazini nikasimamishwa ili nikatibiwe, ndugu zangu wakanipeleka hospitalini, baada ya vipimo vingi na kuzunguka hospitali nyingi za magonjwa ya akili ikiwemo MIREMBE, sikuonekana nina tatizo lolote la kiakili. Ndugu zangu wakaamua kunipeleka kwenye maombi, huko kwenye maombi nilipelekwa nikiwa sijitambui wala sijielewi. Niliombewa sana aina ya maombi yanayoitwa "MAOMBI YA UKOMBOZI"".
Baada ya siku tano kuanzia nipelekwe mombini nilirejewa na ufahamu, maombi yaliendelea.
Siku ya tisa nikiwa hapo maombini nikiombea, mapepo yalifumuka, yalinirusha juu na kunibwaga chini, mapepo yaliongea mengi, yalielezea kisa kizima cha jirani yangu na mkewe kuwa huwa wanatumia nguvu za giza kuwavagaa watu wenye uwezo kidogo wa kipesa (WENYE UNAFUU WA MAISHA) kuwatupia hayo mapepo kwa mke kujidai anakutaka, na ukiingia kwenye kumi na mbili zake wanakukwangua kila kitu.
Hivyo ndivyo namna wanavyoishi hapa mjini.

Nikafanyiwa maombi na kisha nikapona kabisa, nilirudiana na mchumba wangu, tukafunga ndoa na niko nae mpaka sasa. Nilirudi kazini na baada ya miezi mitatu nikapata promotion.
Mke wa mtu alinitesa kwa muda wa miaka mitano, huku yeye na mumewe wakila jasho langu kiulainiiiiiii.
Uchawi upo na pia nguvu za MUNGU zipo na zinatenda kazi kupitia kwa watumishi wake.
Tusiache kumuomba Mungu atulinde na uchawi ni kila hila za muovu ibilisi shetani.
Hv story yako isingenoga mpaka umemuingiza mpenzi wangu Ben?
Unajua nina uchungu kiasi gani kupotelewa nae?
Next time tafuta wa kuwatolea mifano, si Ben Saanane wangu.
Maumivu yalipona na nilisahau, unayatonesha upya.
Nimemaliza.
 
Hv story yako isingenoga mpaka umemuingiza mpenzi wangu Ben?
Unajua nina uchungu kiasi gani kupotelewa nae?
Next time tafuta wa kuwatolea mifano, si Ben Saanane wangu.
Maumivu yalipona na nilisahau, unayatonesha upya.
Nimemaliza.
Wataalam wa limbwata utawajua tu, yaaani hujaumizwa kwa ishu ya sir8 umeumizwa na kukusema wewe na yule Mkurya wako hapa jukwaani.
 
Bujibuji we ni rafiki yangu kuanzia leo, coz akili zimekulejea Mie nilikua nakushangaa Kumbe hukuwa wewe

Jaman kwa yeyote aliekosewa na bujibuji kwa comments zake amsamehe coz akili hazikua zake.

Ila kuanzia leo yupo timamu,tumshukuru MUNGU!!! KARIBU JF BUJIBUJI NA AKILI MPYA!!!
Nimeipenda hiii.
Hebu sikiliza hii album kali kuliko.....
 
Back
Top Bottom