Ushuhuda: Nimedhulumiwa na kampuni ya Sunranch

Ushuhuda: Nimedhulumiwa na kampuni ya Sunranch

Unanunua Nyoka ili iweje ?

Hata ukipata wewe haimaanishi kitu sio Utapeli; kuna mambo hayapo sustainable and they neither make economic or logical sense....;

That said mimi naweza kuja leo kama mkulima ninafuga nikatafuta investors ili msaidie kwa fedha mimi niwekeze nguvu (ila sio kwa hio return ya 10K unless huyo mnyama bei yake ni kubwa au within a year anatoa kitu fulani kikubwa) 10,000/= x 365 = 3,650,000/= (hata kama hilo linawezekana ila sio kwa idadi ya watu ambayo ni infinity...; Hata kama kuna soko la huyo mnyama la wanyama 100,000 kwa mwaka vipi wakijiunga watu 200,000 ? Huoni hapo business itakuwa saturated ?!!!

Lakini ukienda deep biashara nyingi sasa hivi duniani ni Deci / Ponzi na Speculations without anything being produced...; Hata Mabenki yenyewe ni mwendo wa kukopesha pesa ambazo hazipo (Creating Money from Nothing);....., That is the world we live in....
 
Huwa Niko makini comred..,haya yote yalitokea kwa sababu nilipewa ushuhuda na dada yangu wa damu hambaye tunaheshimiana sana..,na dada yangu alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzoni kabisa,unaambiwa hizi kampuni za kitapeli wa mwanzoni ndio Huwa wanafaidi Ili wapate kuwavuta wengine!

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Hata kama bado ni ujinga hata kama ungeambiwa na mzazi wako kuamini tu ni ujinga.
Kwakweli wajinga wa kupiga hawawezi kuisha
 
Mngemuuliza kwanza dada yako kama ni mtumiaji wa jf ungeshakuwa na jibu kuwa dada yako nae katapeliwa

Kuna shuhuda nyingi sana zimeletwa hapa tangu

enzi za deci

enzi za walimu kuuziwa saa kwa mill 5

enzi za wale wale jamaa waliokuwa wanapiga picha na magari mazuri kukushawishi ujiunge nao ili umiliki

Enzi za kina ontario mzee wa forex watu walijaa akaunti zikaungua

Enzi za kina kalynda ulikuwa wapi dogo

Enzi zile za kilimo cha vanila kilo mill 1 baadae ikaja kugundulika kumbe bei ya vanila kilo ni 3000 watu walilia

Mambo ni mengi muda ni mchache

Pole ila umefanya makosa kutokumuuliza dada yako kama anafahqmu kama kuna watu kibao wamelia
 
Wanabodi, najua wengi mtaniita mjinga au hata mpumbavu, lakini kabla ya kufanya hivyo naomba kwanza msome andiko langu

Siku 5 zilizopita nilipandisha Uzi hapa jukwaani nikiomba kujulishwa kama ni kweli kampuni hii ya mtandaoni inaitwa sunranch Ina ukweli wowote au ni matapeli kama walivyo matapeli wengine.,nilifanya hivyo baada ya dada yangu wa damu kabisa ninayemheshimu sana kunishawishi nijiunge na kampuni hii kwa kununua mnyama na kuanza kupiga faida.,bila Shaka wote mnajua ukaribu wa mtu na dada yake hasa mkiwa mnaheshimiana

Dada yangu alikuwa miongoni mwa watu wa awali kabisa waliojiunga na kampuni hii ya kununua wanyama mtandaoni na huenda ni kweli alipata faida na kuamua kunishirikisha kama ndugu yake..,aliponiambia na kunishawishi nijiunge niliona kama nikikataa nitamvunjia heshima ,hasa ikizingatiwa ya kwamba naamini dada hawezi kunidanganya Ili nipigwe.,

Basi kilichofuatia ni kwamba alifanikiwa kunishawishi nikanunua wanyama wawili, mmoja wa laki Moja na elf thelasin,na mwingine wa elf thelasin na tano..,hao wanyama kwa mjibu wa hiyo kampuni ilitakiwa nipate faida ya sh.10000 kila siku kwa kipindi Cha mwaka mmoja. ,na Kuna wengine zaidi ya 1200 walinunua nyoka kwa laki sita ijumaa iliyopita wakitumaini kupata million 5 jumatatu hii, lakini kilichotokea mpaka muda huu .., naomba mwenye ushuhuda aongezee[emoji24][emoji24][emoji24]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app


Bei ya bata ni Tsh 25000, utapata 1000 kila siku, na mapato ya jumla ni 60000 ( halali kwa siku 60)

Bei ya sungura ni Tsh 75000, utapata Tsh 3100 kila siku, na mapato ya jumla ni 279,000(halali kwa siku 90)

Bei ya mbuni ni 190000, utapata Tsh 7600 kila siku, mapato ya jumla ni Tsh 1,368,000( halali kwa siku 180)

Bei ya mamba ni 500000, utapata Tsh 20000 kila siku, mapato ya jumla ni Tsh 3600000( halali kwa siku 180)

Bei ya ng'ombe ni Tsh 1500000, utapata Tsh 60000 kila siku, mapato ya jumla ni Tsh 12600000( halali kwa siku 210)

Bei ya farasi ni 2900000, utapata Tsh 116000 kila siku, mapato ya jumla ni Tsh 34800000 ( halali kwa siku 300)

Bei ya sika kulungu ni Tsh 68000000, utapata Tsh 280000 kila siku, mapato ya jumla ni Tsh 102200000 ( halali kwa siku 365)

Bei ya bata bukini(goose) ni Tsh 50000, utapata Tsh 2000 kila siku, mapato ya jumla ni Tsh 180000 ( halali kwa siku 90).
 
Wewe ni MPUMBAVU tu, tena chizi kabisa.

Juzi tu hapa umeleta uzi, mimi ni mmoja wao nikakwambia hao ni wajanja wajanja tu, pumbavu kabisa, wapumbavu kama nyie mnaotumia hisia badala ya uhalisia ni wa kupigwa risasi au kutolewa kwenye kundi la wanaume. 😠😠😠😡😡😡
 
Huwa Niko makini comred..,haya yote yalitokea kwa sababu nilipewa ushuhuda na dada yangu wa damu hambaye tunaheshimiana sana..,na dada yangu alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzoni kabisa,unaambiwa hizi kampuni za kitapeli wa mwanzoni ndio Huwa wanafaidi Ili wapate kuwavuta wengine!

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Kweny Hela hata wewe mwenyew usijiamin...nyie wenyew akili za kishikiwa ndo mnafanya watanzania tunaonekana wajinga hata kwa majirani zetu hapo Kei
 
Back
Top Bottom