Ushuhuda: Nimedhulumiwa na kampuni ya Sunranch

Ushuhuda: Nimedhulumiwa na kampuni ya Sunranch

lakini kilichotokea mpaka muda huu, naomba mwenye ushuhuda aongezee[emoji24][emoji24][emoji24]

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]pole sana kwenye ile post yako nilikwambia ukiona unaitiwa fursa basi huyo fursa ni wewe!

Wewe mshukuru Manani anua Tanga maisha yasonge! Na huna haja ya kumlaumu dadaako kwakuwa naye alishawishiwa na mtu aliyemuamini sana na huenda naye kabamizwa ila hawezi kukuambia.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23]
 
Wanabodi, najua wengi mtaniita mjinga au hata mpumbavu, lakini kabla ya kufanya hivyo naomba kwanza msome andiko langu.

Siku 5 zilizopita nilipandisha Uzi hapa jukwaani nikiomba kujulishwa kama ni kweli kampuni hii ya mtandaoni inaitwa sunranch Ina ukweli wowote au ni matapeli kama walivyo matapeli wengine.,nilifanya hivyo baada ya dada yangu wa damu kabisa ninayemheshimu sana kunishawishi nijiunge na kampuni hii kwa kununua mnyama na kuanza kupiga faida, bila Shaka wote mnajua ukaribu wa mtu na dada yake hasa mkiwa mnaheshimiana.

Dada yangu alikuwa miongoni mwa watu wa awali kabisa waliojiunga na kampuni hii ya kununua wanyama mtandaoni na huenda ni kweli alipata faida na kuamua kunishirikisha kama ndugu yake, aliponiambia na kunishawishi nijiunge niliona kama nikikataa nitamvunjia heshima ,hasa ikizingatiwa ya kwamba naamini dada hawezi kunidanganya Ili nipigwe.

Basi kilichofuatia ni kwamba alifanikiwa kunishawishi nikanunua wanyama wawili, mmoja wa laki Moja na elf thelasin, na mwingine wa elf thelasin na tano, hao wanyama kwa mjibu wa hiyo kampuni ilitakiwa nipate faida ya Sh. 10000 kila siku kwa kipindi cha mwaka mmoja, na Kuna wengine zaidi ya 1200 walinunua nyoka kwa laki sita ijumaa iliyopita wakitumaini kupata million 5 jumatatu hii, lakini kilichotokea mpaka muda huu, naomba mwenye ushuhuda aongezee[emoji24][emoji24][emoji24]
Sijaelewa samahani; unanunuaje mnyama? unanunua mnyama hai yani unaweza kumchinja au unanunua symbol ya mnyama fulani.
 
Back
Top Bottom