a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 1,966
- 2,200
ushuhuda
Miaka ya 1960's ilitokea mkoa wa Mbeya eneo linaloitwa Mwakaleli
Alipokuwa anaishi mwinjilist huyu mwanamume kijana wa miaka 22 akiwa pia ni muajiriwa wa serikali kama meneja wa shirika la umma .Akiwa amefunga ndoa ya kanisani na mkewe wa miaka 20 ,maisha yalikuwa mazuri na kila kitu kilikuwa sawa.
Pamoja na kuwa mtumishi wa umma pia alikuwa ana huduma ya uinjilisti akihudumu madhabahuni kuhubiri katika kanisa moja la kiinjili katika kijiji hicho cha mwakaleli mkoani Mbeya.
Anakiri kuwa pamoja na kuwa mwinjilist ila pia alikuwa na tabia ya kunywa pombe kwa siri kwa kificho.
Anaendelea kueleza kuwa yeye na mkeweu walifanikiwa kupata mtoto wa kwanza wa lakini alipofikisha umri wa miezi 2 aliugua ghafla kama kifafa degedege hivi siku ya 2 akafa.
tatizo hili liliendelea akapoteza watoto wengine watatu kwa namna hiyo hiyo baada ya kuzaliwa hawafikishi umri wa mwaka mmoja,wanaugua ghafla kama kifafa wanakufa dhafla .
mwinjilisti akaongeza kuendelea kunywa pombe kwa siri
Pia akapata wazo la lutafuta waganga wa kienyeji akazunguka ndani ya nchi ,na nje ya nchi KONGO,Malawi na Zambia
Akatumia pesa nyingi na dawa nyingi za waganga wa kienyeji,ikiwemo hirizi zinazopumua.
Lakini ile hali ya kila mtoto anayezaliwa haishi kufikisha umri wa mwaka mmoja wote waliendelea kufa kwa kuugua ghafla kifafa na kufa gafla kabla ya kutimiza umri wa mwaka mmoja.Jumla watoto alliozika waliofariki walifikia 8 wote walikufa kwa staili hiyo hiyo
na umri wake ulisogea na kufika umri wa mika 42 ,aliteseka na tatizo hili kwa zaidi ya mika 20 la watoto wake kufa ghafla baada ya kuzaliwa kwa kuugua kifafa cha siku moja kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja.
Lakini pamoja na kwenda kwa waganga wa kienyeji na kunywa pombe ,ambavyo hivi vyote alivifanya kwa siri ,bado aliendelea kuhudumu madhabahuni kama mwinjilist akihuburi neno la Mungu katika kanisa la kiinjili mwakaleli.
Siku moja kanisa lao la kiinjili mwakaleli mbeya lilipokea wanakwaya wageni kutoka Arusha kikundi cha UWATA uamsho wa wakristo Tanzania.Walikuja kuwasalimia na kujumuika kuimba kwaya na kudumisha urafiki wa kikristo.
kile kikundi kilihudumu kuimba kwaya hapo kanisani.
wakati kile kikundi cha kwaya kinaimba huyu mwinjilisti alijisikia amani na furaha na kuguswa na kuwapenda sana kile kikundi na ile huduma ya ile kwaya na kuifurahia sana moyoni.
Baada ya kumaliza kuimba kwaya mwinjilisti akaenda kuwasalimia na kitakiana amani na kuwapongeza,
Mmoja wa waimba kwaya kutoka katika ile kwaya wageni akamwambia Roho wa Bwana ananielekeza nikuambie UACHE DHAMBI mtumishi.
mwinjilisti akajibu mimi mbona sina dhambi?,unaniambia niache dhambi gani? mana nasali ,nahudumu madhabahuni nahubiri ,n.k
basi kile kikundi kiliendelea kuhudumu hapo kanisani kwa siku ya pili
Lakini yule mwinjilisti bado alitokea kufurahishwa sana na kuvutiwa sana na ile kwaya wageni,na kusikia amani moyoni juu ya uwepo wa ile kwaya
walipomaliza kuimba mwinjilisti akawafuata akamwambia ,nikiri tu ni kweli mimi nina dhambi huwa naenda kwa WAGANGA wa kienyeji ,huwa nina tatizo kila nikipata mtoto anakufa ghafla nimeshazika watoto wanafika nane sasa.
Akaambiwa ni adui michezo ya nguvu za giza wachawi wanakula watoto wako kishirikina
akatubu akaongozwa sala ya toba ,akatubu na kuleta hirizi zote alizopewa na waganga wa kienyeji na manyanganga yote yakachomwa moto.
Akaambiwa kwa JINA la Yesu ,hatakufa tena mtoto .
mwaka mmoja baadae akiwa na umri wa miaka 43 akampata mtoto tena wa kiume,akakua vizuri kwa mara ya kwanza akashuhudia ametimiza mwaka mmoja na kuendelea bila kufa.
akapata na wadogo zake wawili wa kike.
watoto wote wakiwa wazima mpaka sasa yule wa kiume na dada zake wawili wote wameajiriwa na wanafamilia zao ni wazima wa afya.
Wanaishi maisha mazuri ya furaha na amani ndani ya Yesu.
Tunajifunza nini.
ACHA DHAMBI
usiwe na michanganyo kwa mganga wa kienyeji kidogo,pombe kidogo,uzinzi kidogo,kutambika mizimu ya kwenu kidogo changanya na kanisani kidogo..
yani kanisani upo kwa Yesu kidogo na kwa shetani kidogo
Siyo moto wala sio baridi yani upo vuguvugu.
unakuta kila jumapili unaombewa pepo linalopuka linatoka
jumapili ijayo pepo hilo hilo linalipuka tena
mwaka mzima ,kila siku unaombewa pepo linalipuka linatoka linarudi tena,mwaka kesho ,mwaka kesho kutwa pepo linakuganda linatoka linarudi.
Haitakiwi pepo likishakutoka likurudie tena,kila siku unaombewa pepo tu haitakiwi iwe hivyo..ACHA DHAMBI
Yn 5:14
Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
nakuacha na neno
Mit 28:13-14
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara.
Isa 59:2
lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
Mit 28:9
Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo.
Sam 15:22
Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
Tit 2:11-12
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa
Rum 6:1-7
Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.(UTAKATIFU)
1 Pet 1:15-16
bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Yn 14:23
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Yakobo 1:22-24
Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo. Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo. Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo.
1 Petro 3:12
Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza maombi yao. Bali uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu.”
Zaburi 34:15
Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.