Heinrich Himmler
Member
- May 20, 2013
- 71
- 151
Nilikuwa nafanyakazi tarime mgodi wa North Mara miaka ya 2009/10 kwenye kitengo cha security. Kuna kijana anaitwa John tulikuwa naye kwenye kitengo cha security. Mimi na John tulikuwa tunasimamia ugawaji wa mufuta kwenye machine zilizopo kwenye machimbo (Pit) kwa kutumia fuel boozer. Ratiba yetu kwa siku ilikuwa inaanza saa 12 asubuhi tunajaza boozer mafuta na kwenda nalo pit.
Siku moja nikaamka asubuhi pale camp nikampitia john nikakuta ameshaondoka, basi nikajua ametangulia offisini, nikaenda ofisini sikumkuta nikawa namsubiri, nilivyoona anachelewa nikaanza kumtafuta kwenye simu lakini simu yake ikawa imezima. Muda ukawa unaenda nikashangaa hata wazungu mabosi wa security hawapo, basi nikaamua kwenda kusimamia ujazaji wa mafuta mimi mwenyewe. Baada ya muda John akawa amekuja nikamuuliza ulikuwa wapi. Akanijibu siku ilivyoanza;
Alipigiwa simu kama saa 11 alfajiri na security manager (SM) aende ofisini, akaenda alipofika pale akamkuta manager na mkaburu mwingine, wakamwambia azime simu yake halafu awape, alipowapa wakamwambia aendesha gari wakaende nae camp anakokaa security superintendent (SS). Yeye akaambiwa asubiri kwenye gari, wakaingia ndani wakakaa kama dk 10, halafu wakatoka wamebeba maboksi kama ya ukubwa wa sabuni za mche, kilichomshangaza yale maboksi ni madogo lakini wameyabeba wawili, mmoja akaja kufungua mlango wa nyuma wa gari na kubakia pale, wale SS na SM wakaingia ndani kuja na boksi jingine mpaka yakafika maboksi matatu. Wakati huo walikuwa wanawasiliana na makaburu wenzao kwa simu za mkononi kwa ki-africana. Walikuwa hawatumii radio call.
Baada ya kumaliza kuyapakia SS akapanda mbele na SM na Yule kaburu mwingine wakapanda nyuma kwenye yale maboksi, akaambiwa aendeshe gari kuelekea plant. Akaendesha gari kuelekea plant akashangaa mageti yote kutokea camp kuelekea plant yapo wazi na kuna security officer mkaburu kila geti hadi geti la “high security” , alipofika plant wakayashusha yale maboksi wenyewe na kuyaingiza kwenye helicopter ambayo ilikuwa imekuja kuchukua mzigo wa dhahabu ambao unakuwa umekaguliwa na kuwekwa seal na TRA na TMAA tokea jana yake.
Ile helicopter ikaondoka. Baada ya kuondoka ndio wakamrudishia simu yake na kumruhusu aondoke. Aliponisimulia hivyo nikajua wameshatuibia dhahabu, kwa sababu kiutaratibu, dhahabu huwa haitoki gold room, maafisa wa TRA na TMAA huja siku moja kabla ya kusafirisha dhahabu na kufunga seal zao, siku inayofuata dhahabu iliyofungwa hupakizwa kwenye helicopter ambayo hutua hapohapo plant.
Nikaamua kumpigia Yule afisa wa TRA wa Musoma anayekuja kufunga seal pale mgodini nikamweleza huo mkasa mzima akampigia afisa mwingine wa TRA aliyepo mwanza aende akaiwahi ile helicopter kabla haijatua ili aone kama kuna mzigo wa dhahabu ambao haujafungwa seal. Bahati mbaya Yule afisa wa mwanza akafika uwanja wa ndege wa mwanza akakuta ile helicopter imeshatua na mzigo umeshafaulishwa. Ikwawa imekula kwetu.
USHAURI wangu kwenye kukagua haya madini maafisa wetu wawe wanakagua na kufunga seal siku hiyo hiyo ambayo dhahabu inasafirishwa ili wahakikishe dhahabu inayosafirishwa ndio ile iliyofungwa seal pekeyake. Otherwise makaburu wanatupiga sana, kwa sababu wenyewe kwa wenyewe wanazungukana na kuiba dhahabu, case za makaburu kuiba dhahabu ni nyingi tu humu migodini, wakanada wenyewe wanajuwa kuwa makaburu wanawapiga