USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

Nahitaji jogoo kwaajil ya mbegu.. (ni PM Kama upo mkoa wa KAGERA/Mwanza) Nataka nianze kufuga kuku wa kienyeji! Banda tayari ninalo na mitetea 20 ninayo
 
Kuna ukweli katika maelezo ila pia kuna mistakes ulizofanya kama kuwaacha matetea na vifaranga..!

Na kutochanganya chakula chako mwenyewe chenye ubora.

Vifaranga ungevitenga vyenyewe nakuwekea bulb au chemli hata kama viko 300 na kuwapa chick mash...unamwacha mama yao awahi kutaga tena akiwa na majogoo.
 
Doh..kuna mdau alinambia nianze na kuku kumi tu baada ya mwaka ntakua bilionea
 
Mkuu Mimi Nina kuku 2 wanataga simchezo yaani mayai 30 na Kitu kila mmoja
 
Mkuu Nimekusomaa vizurii, natumaini naweza pata mengi zaidi kutoka kwako

Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
 
Uko sahihi mkuu. Kama unataka pressure tegemea kuku.
Kuna shida mbili au tatu katika ufugaji wa kuku.
1.Kuna magonjwamengi sana, hata ukichanja, kuna dawa za chanjo ambazo ni fake (feki) kwenye soko letu. Hivyo unaweza kuchanja na bado wakafa.wakati mwingine unapata vifaranga ambao wana maambukizi toka kwa msambazaji wa vifaranga Ukifanikiwa katika hatua hii, unapata shida ya pili
2.Masoko. Kuna matapeli wengi sana wanajipangia bei ya kuku na mazao yake. wataomba uwape kuku wakauze kisha ukachuke hela, hapo imekula kwako
3.Kuna hawa watu wenye mashine za kutotolesha vifaranga wa kienyeji nao ni hatari. unapeleka mayai 100 unapata vifaranga 30 ,mengine yoote unaambiwa viza
 
Asante sana mtoa mada daah 2016 nilikua siwaz haya kabisa kumbe kuna watu wanapeana madini tu uku, hongereni sana wachangiaji nimejitahidi sana kusoma comments

Kwa ufupi najiandaa kufanya ufugaji wa kuku, na mm nilikua nawaza kuku wa kienyeji na hao chotara, mpaka napata uzi huu ilikua katika kutafuta maarifa
Natarajia kuoata eneo kama heka moja hivi lipo mbali na makazi ya watu

Naomba kupata a be che kuanzia kwenye structure ya eneo hili pia mabanda ndani yakaaje, nilisikia kuku wanapenda kuning'inia
Hapa mm najua mtaji ni iyo heka moja nafasi nafasi nafasi ni muhimu sana

Je, hamna shida kuweka chotara na kuku wa kienyeji sehemu moja?

Jinsi ya kutafuta masoko nifanyeje?

Jinsi ya kuandaa chakula cha kuku, kuna mdau pale alitoa website lakini chini nikaja kuona kuna mtu akasema iyo website haifunguki

La mwisho hao kuku wa kienyeji nawapataje kwa hapa dar na pia chotara nawapataje na bei zake pia

Natanguliza shukrani zangu na mbarikiwe sana ndugu zangu
Ginner
mfuga kuku
@
 
black austrolop nimetembelea kwenye blogs na web za wabongo naona wanamterm kama ni kuku wa malawi, je ni kweli kuku weusi maarufu kama wa malawi ndio breed ya black austrolop?
 
Nami pia nakubaliana na michango chanya iliyomo kwenye uzi huu.
Mwanzilishi wa uzi ni mfugaji, ambaye anafuga kuku chotara.
Nakubaliana na hoja za Ginner.
Mimi nafuga Kuku wa kienyeji kwa sasa.
Huko nyuma, nimefuga Kuku wa mayai, 'layers', Kuku wa nyama, 'broilers', Kuku chotara, 'black Australop', aka Kuku wa Malawi.
Hivi sasa nafuga Kuku wa kienyeji, ambao binafsi nawaita "Shombe".
Siyo Chotara.
Kuku wangu ni 'Shombe' kwa sababu 'Mitetea' ni kuku wetu wa kawaida, wa kienyeji, lakini 'Majogoo' ninayotumia ni 'Kuku wa Kisukuma', maarufu kwa jina la 'Kuchi'.
Kwa hali hii, watoto wanaozaliwa wanakua haraka, (grows faster) ingawa napata tatizo la idadi kubwa ya 'Vilema', maana miguu yao ni mirefu sana.
Shombe hawa wanakua haraka, lakini miguu yao mirefu inashindwa kubeba uzito wao.
Baadhi, kama asilimia 5 hivi, wanakuwa vilema.
Asilimia 5 ni kubwa sana kwa Mfugaji.
Inanibidi kuongeza kiasi cha Madini na Mifupa na DCP kwenye chakula cha vifaranga ili kupunguza viwete.
Nafugia Wilaya ya Mvomero, Tarafa ya Mkindo, Kijiji cha Mkindo.
Kuhusu soko la kuku, mpaka sasa, mahitaji ya Wakaangaji wa chips na kuku katika eneo ninaloishi pamoja na maeneo jirani ni zaidi ya kuku 200 kwa wiki.
Soko lipo.
 
Bei elekezi ya kuuza hawa chotara ni shilingi ngapi?
 
Bei elekezi ya kuuza hawa chotara ni shilingi ngapi?
Ginner atusaidie katika hili la bei elekezi ya kuku chotara.
Bei ya kuku wa kienyeji huku Kijijini ni kati ya Sh. 10,000/= na 15,000/=.
Majike yana bei ya chini huku majogoo yakiuzwa bei ya juu kidogo.
Nilienda kwa Mfugaji Dar, eneo la Goba, kutafuta mbegu ya Kuchi, nikakuta majogoo chotara aina ya 'Kroiler' yanauzwa Sh. 25,000/= kila moja.
 
Okay kama bei zipo ivyo, soko lake ni mahotelin tu na migahawa mikubwa labda, maana vibanda vya chips kuku wao ni hawa wa 7000/=
au nipe somo kidogo kwenye masoko kama hautojali ndugu yangu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…