USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

Bravo, watanzania tuamke na tufanye, utafiti mkubwa umefanywa juu ya huyu kuku hapa Tanzania, ni aibu kufanya mazoea
 
Tukiendekeza ukisasa tutaharibu uumbaji wa Mungu halisi. Waone watoto siku hizi walivyonenepeana kwa sababu ya haya mayai ya kisasa! Daima huwa nafurahia kuwaona wanangu wakiwa na maumbo mazuri bila kufutuka miili. Kuleni hayo mayai ya kisasa majibu mtayajua.
 


Hii kasumba ya watafiti wetu kufanya reaserch za kinadharia na kuzifungia kwenye makabati ndio kama hizi, Profesa wa Poultry anafungua bar badala ya kuwa na banda la kuku kufanya kwa vitendo. Mkuu nakubaliana na hoja zako, ziko sahihi katika level ya kitafiti, ila kibiashara mambo hayako hivyo. Umetoa mfano wa kuchi etc, kwa wafugaji wa kuchi wanaweza kusema neno hapa, kuchi ni kati ya kuku asilia wanaofanya vyema sana sokoni hasa kwa ukubwa wa maumbo yao, ila ni breed ngumu Zaidi katika kuzaliana. Majogoo ya kuchi hudominate matetea mengi Zaidi na kuwapiga majogoo mengine yasikaribie matetea, ila mating kwa kuchi ni tatizo. hata matetea wa kuchi hutaga mayai machache Zaidi kuliko aina nyingine za kuku asilia na hii ndio maana population ya kuchi huwa ni ndogo na haiongezeki kwa kasi.

Pia ifahamike, si jambo rahisi kufanya breed selection kama mtaalamu anavyodai hapa. Kuna baadhi ya breeds mfano kuroiller ya india, Imewagharimu miaka Zaidi ya 50 kwa KEGG FARM, wengineni mpaka miaka mia kupata pure breed ya kuku wanaohimili mazingira magumu, kuwa na maumbo makubwa na kiwango cha juu cha utagaji. na kwa vile kampuni hutumia gharama kubwa sana katika hili, formula la kufanya breed selection hubakia siri ya kampuni, wao huuza parents tu kwa dealers na dealers wao wanauza commercial breeds. Selection inahitaji utaalamu wa juu sana kuweza kubaini dominant na recessive genes ili kupata aina ya kuku unayohitaji. Uzuri wenzetu waliofanikiwa wameshatusaidia kwenye hili la breed selection na izo breeds zipo mtaani ikiwamo wale wanaoitwa wamalawi pamoja na kwamba crosses wengi ni third to tenth generation huwa hawafanyi vyema sana.

Kweli kupeleka mayai mabovu sokoni ni aibu, ila kwa kiasi kikubwa mayai huaribikia yakiwa sokoni tayari na si kwa mkulima.Na sababu hii imefanya supermarket nyingi kutonunua mayai ya kienyeji bali wanakupa supplier a shelf ndani ya supermarket ili uweze kulihudumia. wao hukupa sehemu ya kuweka bidhaa zako, wao wanauza kwa niaba unakuja kuchukua mapato mzigo ukitoka, ila pia jukumu la supplier ni pamoja na kwenda mara kwa mara kubadili mayai yaliyopita muda wake na kuyaweka mapya kwa gharama zako mwenyewe. yale yaliyoharibila/kupita muda ni hasara yako supplier.

'' kauli ya mleta mada kuwa yai LA kienyeji (lililorutubishwa) huharibika haraka viz aviz lisilorutubishwa ni ulongo mtupu, the fact is yai lolote ukilitunza kwenye shelf temperature kama ya pwani huharibika haraka.''

Kunituhumu kusema uongo kwa mambo usiyoyajua ni si sahihi, kwa wale wanaofanya hatching wanaweza kuwa wanajua hili, yai lisilo na mbegu, hata likikaa kwenye incubator kwa siku 21, kwa joto kubwa Zaidi ya lile pwani la nyuzi joto 37.8 bado hubaki vile vile bila kubadilika wakati yale yenye mbegu huwa vifaranga. Na mara nyingi haya masalia ya mayai yasiyo na mbegu toka kwenye incubators / hatcheries baada ya siku ya 18 au 21 ndiyo yanayotumika sana kutengenezea baadhi bidhaa ikiwemo half cakes, chapatti, cakes etc.

Tafiti mnazofanya ni kati ya mambo bora sana kwaajili ya kuendeleza tasnia hii ya ufugaji hapa nchini, ila ni vyema mnavyofanya tafiti hizi angalieni tija ya tafiti zenu katika kufanya mapinduzi ya kibiashara ya ufugaji. kama findings za tafiti haziwezi kuwa na commercial impact basi naweza sema zina tija ndogo sana kibiashara.
 
Ginner
Nimekuelewa Mkuu vizur sana
Ila napenda kukusahihisha kidogo kwenye utagaji mayai kwa kuku wa kienyeji
Kwa uzoefu wangu wa miaka mitano kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji, kuku mmoja jike kwa mwaka anaweza kutaga mayai 150.
Ninachokifanya mimi kuku akianza kutaga huwa nampunguzia mayai hadi idadi ninayoitaka ikamilike ndo nampatia mayai yote tayari kwa kuatamia.
Then akitotoa ninamwacha wiki moja akilea vifaranga baada ya hapo namtoa kwenye chumba cha kulelea vifaranga [namwacha huru] akitoka nje hukaa wiki moja kisha huanza kutaga tena.
Ina maana ukizungusha hivyo kwa mwaka kuku mmoja anaweza kukupa vifaranga 150~ 200
Sema Changamoto Iko Kwenye Soko

Nawasilisha...
 
Makala yako ni nzuri, lakini kitaaluma na uandishi wa kitaaluma inaonekana kuegemea upande. Mimi naona kwa kuwa wewe tayari unafuga kuku chotala tayari ni mshindan wa kuku wa kienyeji hivyo huwezi kuwa neutral lazima utakuwa biased. Ningekuona umeandika kiasi juu ya uzuri wa kuku wa kienyeji, lakini umeandika changamoto tu, kuanzia kuwafuga, mayai kiasi kidogo, uatamiaji hafifu muda mrefu wa kuwafuga nk nk. Kuku wowote iwe wa kienyeji au wa kisasa utagaji wake unategemea lishe. Kuku wa kienyeji wa Tabora ni tofauti na wale wa Moshi. Hujatuambia inakuwaje ukichanganya mbegu hizi mbili ingawaje wapo wa Malawi na Zimbabwe hawa nao ukichanganya inakuwaje. Inakuwaje ukitumia mashine kutotolesha mayai, kwa sababu hata hao chotara ukiwafuga lazima utachanganya mbinu za kienyeji na za kisasa.
Nadhani, pamoja na andiko lako zuri unahitaji kwenda zaidi ya hapo ulipofikia.
Mimi nimewahi kuanza kufuga kuku mmoja wa kienyeji. Akataga mayai 11 na akatotoa vifaranga 11. Kwa bahati mzuri vifaranga wote wakakua kufikia kuanza kuataga. Nikawauza kwa bei ya shs 2500 kwa wakati huo. 2500x10= 25000. Nikanunua nguruwe. Baada ya miezi 6 nikampandisha na baada miezi minne nguruwe akazaa piglets 11 @ 10, 000 maana bei ilikwisha panda nikapata 110,000 nikanunua ngombe crossbreed na Mpwapwa na Fresian. Binafsi niona hayo ni maendeleo kuanzia na kuku mmoja wa kienyeji.
Mtandaoni hatudanganyani ila tunachosema ni kuwa ukiwa mtaji mdogo unaweza kufanya kitu. Development by definition means change. Change from one inferior stage to another a bit supperior stage. Tunataka kila mtu ajione anaweza hata yule aliyekuwa anafikiria everything is imposible aone angalao hili kwa kiasi hiki anaweza
 
bantulile
Ahsante sana, kuna watu humu wanabeza watu wanaofanya vitu vidogo, hawajui kuwa hata vikubwa msingi wake ni kuanzia vidogo! Wewe ulinunua kuku mmoja ukafanya majaribio ukapata faida - SAFI SANA!
Mtu anakurupuka hajafanya jaribio kwa vitendo anakurupuka kuanza na kundi kubwa la kuku, wanakufa wote - anaingia mtandani kulalama eti kadanganywa!
 

Nakubaliana na hoja yako mkuu, na nikupongeze kwa mafanikio. hakika hiki ndicho nachozungumzia pale naposisitiza ufugaji wa kibiashara. business model inaweza isiwe sawa kwa kila mfugaji ila ni vyema tukapeana mbinu kama hizi za namna ya kufanya ufugaji wa kibiashara. umetoa mwongozo mzuri na mbinu uliyotumia kwa hakika itawafumbua wengi Zaidi.
 
nimefuga kuku wa kienyeji kwa muda mrefu, kuku akilalia na kulea kwa wiki hawezi kufika idadi ya mayai 100 kwa mwaka. labda useme vifaranga hivyo ni pamoja na mayai ya nyongeza toka kuku wemgine.
 
Vitu viwili nahisi ni muhimu kwenye huu ufugaji wa kuku wa kienyeji. Mbinu mbadala za ufugaji wa kuku na elimu kwa watumiaji kiubora ukilinganisha na kuku wengine (quality is better than quantity). Bado tuko nyuma kuelimishana.
 
Miezi 10 tu unalalamika khaaa ni mfanyabiashara gn kafanikiwa kwa kipindi kifupi.

Mfano muasisi wa Kali Linux ilimchukua miaka 10 mpk aka release tool hyo ,

Hakuna mjasiria Mali aliyetajirika kwa miezi 10

Hoja yako naipinga mkuu na ni invalid
 
nimefuga kuku wa kienyeji kwa muda mrefu, kuku akilalia na kulea kwa wiki hawezi kufika idadi ya mayai 100 kwa mwaka. labda useme vifaranga hivyo ni pamoja na mayai ya nyongeza toka kuku wemgine.
Samahani kuu naomba nitoe uzoefu wangu kwa hili la mayai.
Mm kuku wangu naofuga hua na stani wa kutaga mayai 15-17. Na kumchukua miezi miwili kutaga tena.haoa ipo hv namuwekea mayai analalia mpaka anatotoa.baada ya kutotoa tu,mm humnyang'anya vifaranga ck ya kwanza anayotoka na vifaranga ndani.hivo baada ya wiki mbili huanza tena kutaga.huu ndo mtindo natumia kwa kuku wng woote.
 
nimefuga kuku wa kienyeji kwa muda mrefu, kuku akilalia na kulea kwa wiki hawezi kufika idadi ya mayai 100 kwa mwaka. labda useme vifaranga hivyo ni pamoja na mayai ya nyongeza toka kuku wemgine.
Mwaka una wiki ngapi? 52
Kawaida ya kuku wa kienyeji ...
Anataga wiki 2
Anahatamia wiki 3
Analea wiki 1
Anapumzika wiki 1
Hizo ni jumla ya wiki 7
Chukua 52 gawia 7 = 7
Mizunguko 7 x vifaranga 12 = 84
JIBU LIKO WAZI, NA HAYA MAHESABU NIMEISHAYAFANYIA KAZI, CHANGAMOTO NI KWENYE KULEA VIFARANGA JAMANI.
 
Ndugu zanguni,
mimi pia nafuga hawa kuku wa kienyeji na ninao hawa kuku 142,wakati nawanunua nilikua namatarajio makubwa sana yaani niwalishe vizuri wakue nipate mayai lakini haikua hivyo badala yake wakawa wanataka kwa kusua sua na hapo tayari nimetumia pesa nyingi kuwatunza ikabidi niwauze tu kwani wamenitia hasara sana ,hivyo nimebakiwa na hao 142 ambao nao nimeamua niwaachie tu sasa wajitafutie coz nina eneo kubwa.Sasa hivi nimebahatikakupata kuku 42 wa mayai yaani wanataga mpaka najiuliza hivi nilikua wapi siku zote.Hivyo kibiashara fuga kuku wa kisasa ila kiafya fuga wa kienyeji
 

Mkuu unaweza nisaidia formula ya kuchanganya msosi wa kuku ili watage vizuri?
 
Jamani nahitaji mayai ya kanga, please
Mayai ya kanga mimi ndiye mzalishaji mkubwa na nakaa Dodoma. Kwa uzoefu wangu kanga hutaga kuanzia mwezi wa kumi mpaka may maka unaofuata. Kwa sasa kanga wamenipungua sana ninao kama mia mbili na ushee. Katika msimu wa utagaji huwa sikosi trei tatu kwa siku na yai moja nauza mia tano. Ukipenda vifaranga pia utapata kwani ninayo mashine ndogo ya kutotoresha yenye uwezo wa mayai 96, na kifaranga kimoja nauza sh 1500 cha siku moja. Kikifika kipindi hicho tuwasiliane kwa simu na 0786775663 /0757284076 /0715557342 . Pia ninafuga kuku wa kienyeji ( crosbreed) kwa sasa ninao zaidi ya mia tatu na pia nafuga bata mzinga ila soko linanishawishi kuacha kuwafuga.
 
aiseee... umeongea sana nimependa... sio mfugaji... ila tatizo hapa mi nililo liona halipo kwa kuku hawa wa kienyeji... tatizo lipo kwako mfugaji, ni kusema kua kuku hawa hawana tija kibiashara nimekataa kidogo kwa sababu hizi.

1. ubunifu kwako ndio imekua tatizo... kama kuku wa kienyeji hawawezi kutaga mayai mengi kwa mwaka maana yake unatakiwa uangalie njia gani ufanye ili waweze kutaga mayai mengi... kuanzia lishe mpaka ufugaji... kwanini huyu kuku akitaga kama ulivyosema anataga siku 10 kumaliza... akimaliza ukiyachukua... ili akae mda kidogo aje kutaga tena itakuaje..? au ata susa kutaga tena.?
na kama utunzaji wake hayatakiwi kuwekwa sehemu yenye joto, firdge zimejengwa za nini, supermarkets gani hizo zisizo na A/C kufanya mazingira yawe ya baridi?
2. nyama... usishindanishe nyama ya kuku na samaki... kwani kila mteja ana ladha anayopenda... wateja wa nyama hugawana, unataka kuniambia hawa kuku wakilishwa vizuri hawa nawiri na kuongezeka kilo, kama ni kutaka kuku wengi... na kimsingi kuku hawa ni lazima warutubishwe na jogoo... tetea wakisha taga na na mayai yakatotoleshwe na mashine ili tetea watage tena haiwezekani?

kila biashara ina tija endapo utakua mbunifu... na hakuna biashara isiyo na changamoto... na kuku hawa ndio kuku wanaotoa nyama na mayai yenye virutubisho vingi ukilinganisha na hao kuku wengine... sio busara kusema hii biashara sio ya kufanya... cha msingi ni kuangalia na kutafakari njia gani zitumike kurahisisha na kuipa tija biashara ya kuku wa kienyeji.
 
ni kweli kabisa... ni ubunifu na kufata taratibu za ufugaji... hawa kuku hawawezi kua na hasara.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…