Habari zenu wapendwa ?
Ni miezi 6 sasa tangu nilipofanya transfer ya chuo mwaka ulioisha
Nilikua napata mkopo kama kawaida lakini tangu nimehama mpaka sasa sijasaini hata shilingi tano
.
Tumekua tukifuatili suala hili loan board kwa muda wote Huu lakini cha kushangaza kila siku tunapigwa tarehe
.
NAOMBA niseme ili kama nyie wahusika mpo humu mjionee MADUDU mnayoyafanya
.
Nimefuata utaratibu wote wa transfer kupitia TCU,barua copy ya ukubali wa transfer kutoka TCU ikatumwa kwenu na TCU kututambulisha tumehama chuo na ivo mikopo yetu mnapaswa kuihamisha
.
Lakini jambo la kushangaza mkapeleka boom la kwanza tulipohama
Tukawafuata tena kuwaulizia mkasema tuandike barua ya kusitisha mkopo usiende chuo cha zamani - tukaandika na kuwaleteeni lakini kama kawaida yenu boom la pili mkalipekeka kulekule
.
Tukaja tena kuwaambieni kwa nn mmelipeleka mkadai tuandike barua tena YA kusitisha tukaandika lakini cha ajabu boom la tatu mkalipeleka tena
.
Hivi nyinyi loan board mnadhani watu wanaishije kwa muda wote huo ama m nataka wakajiuze?
mSivo na huruma kila siku mnatupiga tarehe kwani mnataka nini hasa?
.
Kama tu wanaopata boom wanalalamika maisha magumu vipi kuhusu sisi mliokaa na pesa zetu kama za kwenu?
.
Tumeshindwa kusoma sasa tunawaza tutaishije
Tunakosa chakula,tunalala kwa marafiki mpaka wameshatuchoka ,tunakula mara 4 kwa week kusave budget lakini nyie hamuyaoni yote haya kila tukija mnatupa tarehe
.
Hivi kuna ugumu gani kutuingizia pesa zetu?
Nyumbani penyewe washatuchoka sasa kila siku mzazi unamlilia pesa
MAISHA yenyewe ndoo hayo ya kubangaiza
Mzazi ahudumie timu ya watoto nyumbani bado akupe na wewe ,kweli?
Tumekopa mpaka visivyokopeka lakin nyie hamuyaoni yote haya jibu lenu ni moja tu --TUNAWASHUGHULIKIA,MITAMBO INASUMBUA-WAKUU WANAYAPITIA mara WANAYAPITISHA
.
KILA ukija hapo kuna utaratibu mpya
Leo huyu anakuambia pesa zenu zipo tayari
Ukija tena mwingine anakuambia mitambo INASUMBUA
Mwingine andika barua
Yaani mnakera mnakera mnakera
.
Kila mara tunakuja kuwatembelea mnatuchora tu
Kwa uzembe na makusudi mnayofanya ipo siku MUNGU atatulipia
Inaendelea.....
Narudi na namba za ofisi zenu soon