Ushuhuda: Bila uvumilivu biashara, ujasiriamali vitakushinda

ELAFU

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
410
150
Siku za mwanzo za kuanza kujitegemea na kufanya shughuli binafsi (Biashara, Ujasiriamali nk) ni ngumu sana. Hili nimelishuhudia mimi mwenyewe "personally".

Changamoto ni nyingi na mambo mengi ambayo mtu uliyapanga au uliyatarajia hayatokei. Inaweza ikakuchukua siku, wiki, miezi, mwaka nk.

Lengo sio kukwamisha wanadamu. Bali ni kuchuja wanaojaribu na wasio serious na kuacha walio serious. Baadae ndipo mambo yanaanza kuwa sawa.

Wavumilivu na wenye juhudi ndo huona kipindi cha mafanikio, waliokuwa wanajaribu na kuacha wanakuwa wameachwa.

[HASHTAG]#Juhudi[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Imani[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Uvumilivu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Tathmini[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Maarifa[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Moyo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Malengo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Mpango[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Kiu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Shauku[/HASHTAG]

Mafanikio huhitaji muda. Ukishindwa kuyasubiri hautayaona, kwa kuwa wakati wake wa kuja wewe utakuwa umeshaondoka..
 
Nashukuru kwa kulieleza hili..Kuna siku nilifikiria kuanzisha uzi kama huu!Vijana wengi tunadanganywa kwenye ujasriamali au biashara na wengi wamejikuta wakitumbukia kisa wamesikiliza success stories kadhaa za watu mashuhuri au wanamuziki..

Ujasiriamali au kuamua kuanzisha biashara ni kama vita no retreat and if u have decided to do it u have to do it!

Ni lazima ujitoe ufahamu na si rahisi kama tunavodhani au kusikia kwa watu maarufu..Changamoto zake ni ngumu na kuna kipindi unahisi kujichimbia kaburi kwa madeni,kuonekana tapeli na kukimbiwa na washkaji kwa kukopa!

Nini ufanye haya yote yanapotokea..

1.Kama ni vita lazima maana yake usikubali kurudi nyuma,endelea kupambana kwa kuji evaluate ili uweze kujua ni sehemu gani unaanguka..kama shida ipo kwenye uendeshaji basi jitahidi kukaa na timu yako muone ni kwa jinsi gani mnaweza kuendesha kwa ufanisi zaidi na kuvutia wateja..Pia jitahidi kufanya biashara kisasa kama kutumia kompyuta softawares kwenye kutunza mahesabu na inventory

2. Jitahidi kuwekeza zaidi kwenye kuongeza mtaji wako kwa kupunguza maisha ya kifahari..jishushe kwa kuishi maisha ya kawaida au epuka anasa kama mabia na kwenda kumbi za starehe pasipo ulazima..unaweza fanya hivyo tu kama kuna faida ya msingi unaipata kwa mfano kunanmtu muhimu unahitaji kuonana naye kwa ushauri lakini ni mtu wa bia badi unaweza kuweka naye apointment bar au club

3. Mtangulize mungu na usjali maneno ya watu
 
True brother.
Mimi mwenyewe baada ya kusoma sana vitabu na semina mbalimbali za ujasiriamali nikajitumbukiza, uhalisia ile nadharia niliyopewa ambayo iko kwenye handout ni tofauti kabisa na real life experience. Sometimes unapata kizunguzungu aisee.
Ila mimi sijakata tamaa na nikiangalia soon nitatoka kimaisha, maana ninapokutana na situation inayokatisha tamaa mimi ndo hapo nafocus mbele zaidi.

Ushauri:
Pale unapoona unakata tamaa, au unaexperience failure, ndipo hapo hapo unatakiwa uone success ahead. Ukikata tamaa imekula kwako aisee.
 
Bonge la point mkuu!!!,safi kweli JF ni shule tosha.
 
Kweli kabisa,hata wahenga walisema baada ya dhiki faraja.
 
Back
Top Bottom