Umuhimu wa "Mentor" katika biashara

Simbamteme

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
784
2,063
NIMEITOA MAHALI,SIMJUI MWANDISHI
(imenigusa sana)

Nimekuwa nikipokea messages na calls kutoka kwa watu wengi mno wanaotaka kuanza biashara au waliokwishaanza biashara ila zimekwama. Utasikia akijieleza changamoto anazopitia na alivyojaribu kuikwamua biashara yake lakini hali inazidi kuwa mbaya nk nk.

Swali langu la kwanza kabisa huwa namuuliza mhusika ni hili:

"WHO IS YOUR MENTOR?"
Kwa wasiojua maana ya mentor huwa hawana jibu zaidi ya kuuliza namaanisha nini nami hufafanua. Na wakishaelewa maana ya mentor jibu lao huwa ni kuwa "SINA HUYO MENTOR NA SIJUI NAMPATAJE". Kwa wanaojua pia maana ya neno mentor huwa jibu ni lile lile KIONGOZI KWA KWELI SINA MENTOR.

Na mimi huwa najiuliza kichwani:

SASA HUYU MTU ANATEGEMEA KUFANIKIWAJE?

So naweza kukwambia kwa uhakika kabisa kuwa sababu moja KUBWA MNO ya watu wengi kufeli katika biashara ni kutokuwa na mentor. Kukosa guidance.

Mentor ni mtu ambaye ameshapita njia unayotaka kuipita wewe na ana UZOEFU, UWEZO na UTAYARI wa kukushika mkono na kukuongoza kuipita njia hiyo pia kwa ufanisi. Mfano ni kama tour guide anayekusaidia kupanda mlima Kilimanjaro hadi ufike kileleni kwa ufanisi maana ana uzoefu, uwezo na UTAYARI wa kukuongoza.

Watu wote waliofanikiwa kibiashara wana mentors. Mtu aliyewasaidia walipofika mahali pa kukwama. Mtu aliyewaambia cha kufanya. Msaada siyo lazima uwe pesa. Mawazo na maarifa ni msaada mkubwa zaidi kuliko pesa. Kama shida yako ni kwamba wateja hawaji then msaada wa kukupa siyo pesa ila maarifa ya kweli ya kwa nini wateja hawaji kwako au kwa nini wakija hawarudi.

UTAJIFUNZA MENGI MNO KUPITIA KUWA NA MENTOR.

MAMBO 6 NILIYOJIFUNZA KUPITIA KWA MENTOR WANGU AMBAYO SIKUWAHI EITHER KUYAJUA AU KUYATILIA MAANANI

Ni hivi, zamani kidogo nilikuwa nashangaa kwa nini Bill Gates alisema
'Kama ulizaliwa maskini hilo si kosa lako ila ukifa maskini basi hilo ni kosa lako"
Niliendelea kubaki na ujinga wa kutokumwelewa mpaka kupitia mentor wangu nilipojua makosa mengi ambayo watu maskini hufanya day in day out.

Nimekuwekea mambo 6 ya kutazama ili kubaini makosa ambayo watu maskini hufanya.

Haya nilijifunza kwa muda mrefu kupitia mentorship program na kwa kusikiliza vizuri mambo ambayo mentor wangu alikuwa akinifundisha.

Yapitie kwa umakini kisha utafakari na kuchukua hatua:

1. KUNA MTI WENYE MZIZI MMOJA?
Ulishawahi kuona mti wowote wenye mzizi mmoja? Hili NILIFUNDISHWA miaka kadhaa iliyopita na my mentor.

Hakuna mti wenye mzizi mmoja.

Sasa maskini wengi wameshikilia ajira (au kibarua, au labda ana kakitu anauza) kama njia PEKEE ya kuwaingizia kipato wakati hata mti wa mwembe tu au mpapai au mti wowote ule una mizizi mingi tofauti tofauti ya kupata chakula, madini na maji kutoka ardhini.

Ndiyo maana hakuna tajiri yeyote dunia nzima mwenye mkondo mmoja wa kipato. Wengi wanadhani Bill Gates anamiliki Microsoft tu. Ana vyanzo lukuki vya mapato. Kama wewe una chanzo kimoja cha mapato basi uko mbioni kufa maskini.

Na hapo shida siyo eti Rais Magufuli amebana sijui vyuma vimefanyaje shida unataka uwe mwembe kwa kutumia mzizi mmoja. Does it make sense kwako kweli kuwa unataka kuwa successful kwa kutumia mzizi mmoja wa kipato.

Una duka halafu basi.
Ajira basi.
Genge basi.

Hakuna mti wenye mzizi mmoja. Huwezi kuwa smart zaidi ya Mungu. Rekebisha hili kosa.
Acha kulalamika. Jenga mizizi mingine.
Utapiga hatua. Mentor wangu aliponifundisha hilo nikajiona kumbe nilikuwa mjinga kwa miaka mingi.
So WHO IS YOUR MENTOR?

2. MAWAZO MGANDO
Alinifundisha pia kuwa maskini wengi wanafanya kosa la kuishi kwa mawazo ya zamani. Yani unakuta akiwaza biashara anawaza duka. Kwani kuna tajiri yoyote mwenye duka au vibanda 1000 vya MPESA?

Hujiulizi?.

Dunia imebadilika maskini hawabadiliki kichwani. Kampuni kubwa ya TAXI duniani (yani UBER) haimiliki gari hata moja. Lakini ndo kampuni kubwa ya usafiri wa TAXI duniani. Anatumia gari za watu wengine. Wewe bado unawaza kununua bajaji na boda boda!

Things have changed. You must also change. Kuna mengi ya kueleza hapa ngoja niendelee na mengine. Lakini hapo pia palinifanya nielewe kauli ya Bill Gates. Na nikazidi kuona kumbe kukutana na mentor wangu ilikuwa kitu cha bahati kuliko nilivyowahi kufikiri.
So WHO IS YOUR MENTOR?

3. PERSONAL DEVELOPMENT

Hapa nitaongea kwa kina.

Mentor wangu alisema kama husomi vitabu hutakiwi hata kutaja majina kama Bill Gates katika mazungumzo yako maana unawakosea heshima hao watu. Maana wanasoma kweli kweli. ndo maana mpaka umewajua. Akaniambia maskini wengi hawasomi vitabu.

But hakuna tajiri asiyesoma. Bill Gates ana wiki mbili kwa mwaka ambazo yeye huzitumia kusoma vitabu vipya ambavyo hajawahi kusoma maishani

Hebu jiulize Bill Gates anajifungia kusoma vitabu ili iweje? Wewe ukijifungia ndani ujue unaangalia series. Au umeachwa na mpenzi unalia wiki nzima. Ukiulizwa umesoma vitabu vingapi mwaka jana January to December... Usikute labda hujasoma kabisa hata kimoja. Lakini message za WhatsApp ulizosoma mwaka jana mzima zinatosha kuchapisha magazeti ya Nipashe ya kujaa kwenye kabati lako la nguo!

I mean that's a shame.

Vitabu hutaki. Mafanikio unataka. Wakati taarifa za mafanikio zimefichwa kwenye hivyo vitabu.
Ukifa maskini hapo utakataa kuwa si kosa lako?

Si unaona sasa kuwa utakubaliana na Bill Gates pia kuwa ukifa maskini ni kosa lako?

Listen, SOMA VITABU. Acha kuishi kwa knowledge ya Mzumbe University sijui UDSM ya miaka mitano au 7 au 18 iliyopita sijui bachelor of nini. Masters of Environmental nini sijui.

Soma vitabu huko ndo kuna maarifa. Mtaani hela hazifati Ph.D ya mtu. Kama ni hivyo maprofessor wangekuwa ndo matajiri. Knowledge ya pesa ina maarifa yake tofauti na Masters of Arts au Ph.D ya mambo ya mazingira. Kama chanzo chako cha taarifa za mafanikio bado ni Tumaini University au ni magroup ya WhatsApp utachelewa sana kujua habari za mafanikio. Find a mentor atakusaidia hata vitabu gani usome.

Hakuna tajiri asiyefanya personal development.

Mentor wangu alisema hata ungekuwa na elimu kubwa kiasi kipi kama hufanyi personal development utabakia kuwa significant katika maeneo mengine lakini si eneo la fedha. Kwa hiyo vitabu ni sehemu ya hiyo personal development. Kuna seminars, nk. Sasa jiulize semina ngapi zinazoongelea mafanikio umehudhuria mwaka uliopita.?

Ngoja nikwambie kitu usipofanya Personal Development thamani yako itabaki kuwa ile ile ya miaka 7 iliyopita. Kuna siku nilikuwa na mfanyabiashara mmoja. And akasema alipata fursa ya kualikwa sehemu kwenda kufanya TRAINING (mafunzo) kwa watu fulani wa "maana". Jumla ya hao watu ni 165. Jumla ya siku ambazo alitakiwa kutoa hayo mafunzo ni siku 5. Na kila mtu katika hao watu 165 alitakiwa kulipa sh 100,000/- kwa siku sawa na 500,000 kwa siku 5 kwa mtu mmoja. Sasa fanya mahesabu sh laki 1 mara 165 hiyo ni hela yake ya siku halafu zidisha mara siku tano!!

Umepiga hiyo hesabu?

Piga kwanza hiyo hesabu. Halafu jiulize wewe ITAKUCHUKUA miaka mingapi kutengeneza hiyo pesa. But point ni kuwa alipata hiyo fursa sababu ana MAARIFA adimu. Anasoma vitabu kweli kweli. Na ana mentor mmoja msomali mmoja tajiri hapa Dar.

Sasa wewe unataka tu ukalime vitunguu au matikiti uwe milionea kesho?
Maarifa unayo?
Unajua aina za vitunguu?
Unajua season za kulima na kuvuna?
Unajua tofauti ya kupanda vitunguu kutumia mbegu na sets na transplant?
Unajua effect ya jua au umande mwingi au mvua hizo variables zinaleta effect gani kwa vitunguu?
Unajua magonjwa na wadudu wanaoshambulia vitunguu?
Unajua vitunguu havipaswi kutoa maua na vikitoa maua shida inakuwa nini?
Una MENTOR wa kukufundisha haya mambo?

Sasa unakutana na message kwenye group la WhatsApp eti vitunguu vinalipa. Unaenda.

Nini hakilipi?

Hata mbolea inalipa
Hata karatasi inalipa
Mbao zinalipa
Nguo zinalipa.

Issue is HOW MUCH OF IT DO YOU KNOW?

Huwezi kupata pesa zaidi ya ufahamu wako kichwani.

Naomba nikuulize swali. Kama idadi ya vitabu ulivyosoma ingekuwa ni pesa yani kila kitabu ulichosoma kiwe milioni moja. Mwaka jana ungetengeneza sh ngapi?

January mwaka huu ungetengeneza milioni ngapi? Okay February hii utatengeneza ngapi?
Wengi tu ni ZERO MILLION. Atabaki kwenye elfu ngapi kwa mwezi au laki tatu mpaka tisa kwa mwezi maisha yake yote.

Kwa sababu watu hawageuzi vitabu kuwa pesa. Kama wasivyotafsiri muda kama pesa.

Maarifa hujengwa taratibu. Siku nyingine ntaongelea vizuri zaidi kuhusu hiyo personal development.

Bottomline READ BOOKS. Mentor alinisaidia sana. WHO IS YOUR MENTOR?

4. TIME MANAGEMENT

Mwaka 2014 mentor wangu aliniambia kuwa kosa jingine maskini wanafanya ni kupoteza muda. Time management mbovu. Hasa vijana.. Hawana ratiba. Akasema tajiri muda wake wa kuoga ni ule ule kila asubuhi. Kuoga yani. Same time. Kuamka same same. nk.

But masikini hasa vijana ni shida. Ratiba pekee waliyonayo baadhi ya vijana ni ratiba ya mechi za premier league anajua ratiba za Manchester hadi mwakani.. na sasa hivi za Aston Villa. Lakini ratiba yake ya kila siku kwamba akiamka anaenda wapi hakuna. Hana hata kadiary au ka notebook hata kale ka sh elfu moja. Angalau awe anaandika vitu muhimu maishani nk.. Nothing. Ndugu zangu hii ni aibu. Halafu anasema anataka kufanikiwa.

Ana magroup ya WhatsApp ya mpira, ya siasa yani moja linaitwa SIMBA MILELE sijui YANGA DAMU jingine MAKAMANDA KASKAZINI, WAZALENDO KANDA YA MAGHARIBI, WAZALENDO BARA NA VISIWANI, mtu huyo huyo mmoja bado yuko magroup ya waliosoma pamoja na waliofanya kazi pamoja ambayo yote hayo habari kuanzia asubuhi hadi jioni ni habari zile zile. Anacopy message za huku anapeleka huku.

Haya. Mwingine ana magroup HAPA KAZI TU, WATASOMA NAMBA, MAGUFULI JEMBE, CCM KAMPENI, UMOJA WA VIJANA, CCM VYUONI, ukimwona yuko busy utadhani karani wa chama. Wengine wako kwenye magroup ya NGONO TU maana huku Facebook na instagram kuna watu wanatangaza kutafuta namba ili wakuunge kwenye hayo magroup na unakuta namba 900 au zaidi.

Unabaki unashangaa hawa watu muda huo wanaupata wapi? Hapo mtu akishindwa kufanikiwa ni kosa la mzazi? Au la mwenyekiti wa mtaa? Au Naibu Spika? Au la Kubenea? Kweli? Yani Kubenea anahusikaje kukufanya wewe ufanikiwe kiuchumi. Sipatagi connection.

Sikia.
Linda muda wako kwa WIVU MKALI na ujitenge na kila kitu kinachoiba muda wako. Time is MONEY.

Maskini wengi wanatumia hela ili wapoteze muda zaidi.
Siku yake inaanzia Instagram inaishia Instagram. Anajua umbea wote wa mjini mpaka umbea wa keshokutwa anao anasubiri tu utokee.
Na yeye anataka kufanikiwa.

Mungu hadhihakiwi ndugu APANDACHO MTU NDICHO ATAKACHOVUNA (Wagalatia 6:7)

So mind your time! Jali muda. Achana ba ratiba za Bunge. Haya mambo niliyajua kwa kuwa na mentor. Alifungua macho yangu. I am asking again hahahaha Chezea Bibi Sabry
WHO IS YOUR MENTOR?

5. KUTOFIKIRIA VIZAZI VIJAVYO

Nilikuwa nikijiuliza kwa nini my mentor ni mtu aliyefanikiwa lakini bado anapiga kazi sana KULIKO watu ambao hawajafanikiwa. Akanifundisha kuwa kosa kubwa maskini hufanya ni kutofikiria vizazi vijavyo.

Mtu hafikirii kuwekeza kwa ajili ya watoto na wajukuu.

Akasema muda wako ukiutumia vizuri leo utawafanya watoto wako na wajukuu watumikiwe na mataifa.

Lakini kwa style ya wengi wetu hii ya kujifikiria wenyewe ilimradi wewe unamudu kulipa kodi na kula na kuvaa basi watoto Mungu ataleta riziki. Khaaa? Kwa taarifa yako Mungu alisema BABA unapaswa kuacha urithi mpaka kwa wana wa wanao (yani wajukuu).

Sasa jiulize hiyo shughuli yako rasmi kwa sasa mwanao anaweza kuja kuiendeleza baada yako. Kwa ajira hiyo ni impossible. Mungu akikuchukua wanaweka tangazo moja kwenye notice board la kifo chako jingine kwenye gazeti la kutafuta mtu wa kujaza nafasi yako. Hiyo ndo reality.

Hapo Kubenea hahusiki sijui Diwani wenu alihama chama..

Sasa ukianza kuwaza kuhusu vizazi viwili tu baada yako utajiona jinsi ulivyo nyuma mno. But watu wanajifikiria wenyewe tu.

Ndo maana ni rahisi kuridhika na vihela vidogo. Hutaki kuhangaika ili wajukuu waje wafaidi. Unataka ufaidi wewe kwanza eti unasema "kwa nini nijitese". Kwani kwa nini Yesu "alijitesa"? Ukiambiwa hivyo unasema" kwani mi Yesu?"

Unaona akili ya maskini ilivyo. Shauri yako. Watoto wako au wajukuu watafukua kaburi lako afu watatoa hiyo skeleton waitandike bakora weee afu waizike tena. Omba ujengewe kaburi lako kwa nondo na zege.

Wengi wanabaki maskini kwa mawazo ya ubinafsi wa kutowaza watakaokuja after you. My mentor alifanya nikabadili sana ufanyaji kazi wangu. Coming to the point Bibi Sabry asking..
WHO IS YOUR MENTOR?

6. KUFIKIRI KUWA KUANZA BIASHARA INAHITAJI UWE NA MTAJI WA PESA KWANZA
I always tell people kuwa we people not Money"
Kuna siku mwaka 2000 wakati ndo nimekutana na my mentor aliniuliza swali: unadhani changamoto ya vijana wengi kuanzisha biashara ni nini. Nikasema haraka sana: MTAJI.

Akanitazama akaniambia wengi wamekwama hapa.
Anafikiri kuwa inabidi atafute mtaji kwanza afu ndo atafute cha kufanya. Wakati anautafuta mtaji fursa zinaendelea kumpita. Akija kuupata anapata matatizo hela tena inatumika kutatua matatizo ya kifamilia. Anaanza upya tena.
Mwisho anaamua kusema basi nahisi "Mungu hapendi". Huwa nawaambia watu kukata Tamaa ni dhambi mbbaya sana. Bibi Sabry sikati tamaa hata iweje.

Akanifundisha kuwa maskini wengi wana kauli rahisi rahisi tu. Eti "Si wote lazima tuwe matajiri". Anajijumlisha kwenye neno "wote".

Mtu anayefanikiwa anajua mtaji wa kuanza biashara ni kitu cha mwisho na ni kitu chepesi mno kuliko vingine vyote. Lakini wengi wanawaza mtaji. See? Kitu cha mwisho na chepesi anakifanya kiwe cha kwanza na kigumu.

My mentor alinifanya kuielewa sana kauli ile juu ya Bill Gates. Ukifa maskini hilo ni kosa lako.

SO..

Nimefika nilipofika kwa kufanya kazi lakini kwa KUSHIKWA MKONO na kuelekezwa. Lakini naomba nikwambie haikuwa tu kukaa na kuelekezwa. Mpaka nakutana na mentor nilikuwa nimefanya juhudi kubwa. Mentorship is not kitu rahisi tu eti mtu mwenye hela zake aanze kukaa na wewe tu from NOWHERE akufundishe.

Hakuna hicho kitu. You must PROVE YOURSELF. Lazima mentor aone kuwa umekomaa kichwani na uko tayari KUFUNDISHIKA. So ili ajue hilo ukitaka mentorship mentor atakupa vigezo ambavyo vitakuchuja SIKU HIYO HIYO. Maana hataki kupoteza muda wake na mtu asiye serious.

Mentorship in not a stroll in the park. Inahitaji uwe kweli umedhamiria kufanikiwa.

KWA NINI NIMEANDIKA HAYA:
Watu wengi wamekuwa wakiomba kupata mentorship na nimekuwa nikisita kufanya hivyo kwa kuwa najua wengi wanaoomba mentorship hawako tayari kuingia gharama ya mentorship.

Mentorship ni tofauti na ushauri. Mtu anapokuongoza kule kupanda mlima Kilimanjaro siyo eti anakuwa anakupa ushauri. No. Anakwambia pa kupita. So kama HUFUNDISHIKI atakuacha.

Mentorship siyo program ya kushauriwa halafu ufikirie weee halafu useme aah mi nimeona nifanye hivi. Sasa ulitafuta mentor wa nini? Si ungetafuta tu ushauri mtaani kwenu mbona ungepata.

Mentorship ni kitu serious kwa watu serious ambao wameona kuwa sasa wanahitaji GUIDANCE ili waweze kupiga hatua ya kweli kibiashara. Usimgeuze mentor kuwa kama BOYFRIEND wako au GIRLFRIEND wako akuchekee chekee. Mentor ni mtu wa kuimpose DISCIPLINE ya mambo muhimu in your life. Hivyo lazima uwe tayari kufundishika ili mentor naye awe TAYARI.

Kule juu nilisema Mentor ni mtu ambaye ameshapita njia unayotaka kuipita wewe na kupitia changamoto na kuzishinda na ana UZOEFU, UWEZO na UTAYARI wa kukushika mkono na kukuongoza kuipita njia hiyo pia kwa ufanisi. Hilo neno UTAYARI wa huyo mentor ni la muhimu sana. Utayari wa mentor unategemea tu kama ameona wewe uko tayari.

Watafute wakusaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point namba 6 umekimbiakimbia tu, njoo uelezee hata Mentor aliishindwa.

Portfolio | 2020
 
Yapo yenye ukweli kwenye bandiko lako lakini hapo kwenye siasa naona kuna ukakasi,
Kwetu hapa Tz siasa ina mchango mkubwa sana na uchumi wa mmoja mmoja na jumla, maana vitu vingi vinapangwa na wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi ndo resolutions zangu twenty twenty
1.quit social media..am nw a you tuber😊! Nimefanikiwa kwa jf kwa 90%
2.kusoma vitabu walau page 1daily..( Veronica must die)
3.my mentor nadhan ni centonomy na TEDx series!

...its not scary as it looks!√
 
Kupitia maandiko unapata ujuzi wa ziada namna ya kutafuta pesa. Mfano inaongeza maarifa ya kuongeza bidhaa sokoni zenye kuleta tija zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
sawa mkuu mafanikio yamefichwa kwenye maandishi,pia kwenye kusoma haina maana ni mafanikio ya pesa tu hapana,

Pia kuna mafanikio ya kukua kifikra,kiimani,mahusiano kwenye jamii,kuongoza watu n,k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sawa mkuu mafanikio yamefichwa kwenye maandishi,pia kwenye kusoma haina maana ni mafanikio ya pesa tu hapana,

Pia kuna mafanikio ya kukua kifikra,kiimani,mahusiano kwenye jamii,kuongoza watu n,k

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tupo pamoja vyovyote pamoja nakupitia maandiko mbalimbali pia unatakiwa kukuza uelewa wa shughuli za uzalishaji kwa kuwasiliana na watu walio katika sekta husika hivyo huongeza maarifa na mbinu muafaka za kuinua na kupanua kiwango cha mapato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom