Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

ONTARIO

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
1,885
17,018
Salute Bosses!!

Kwanza nitangulize shukrani zangu za dhati kwa wote waliobahatika kusoma uzi wangu niliouweka hapa miezi kadhaa iliyopita na tukaShare ideas mbali mbali za kibiashara. Lkn zaidi nimefarijika sana kuwa uzi ule umewafumbua macho watu kadhaa, na kuna wengine kupitia uzi ule wametoka from their comfort zone na kuanza kufanya kitu.

Link ni hii kama hukuusoma: Jinsi nilivyofanikiwa kutengeneza Sh. Milioni 19.9 ndani ya siku 35 kwa kutumia Milioni 3.8

Utangulizi
Biashara yangu ya kwanza nilianza miaka mi4 iliyopita nikiwa chuo mwaka wa 1.

2017-05-22+10.50.jpg
Kampuni yangu ya kwanza ikiwa na miezi 9.

Insta-image-27.jpeg

Kampuni yangu ikiwa na miaka mi2.

7599468930d2a34e3b5507deceb45dd0.jpg

IMG-20170522-WA0001.jpeg
1 ya operations ya kampuni yangu. (Picha ya weekend hii).
IMG-20170522-WA0004.jpeg
Weekend hii.

Basically sikua na mtaji mzito sana, hapa hua nakosa kuaminiwa kila sehemu, mtaji wng wa kwanza ulikua ni posho tuliyokuwa tukipewa tukiwa JKT na chenji nilizobaki nazo kutoka advance. Nilianza kwa ufugaji wa kuku 50 wa broiler, lkn leo tunavyoongea kila mwezi nazalisha thousands of chickens na nimediversify mpk kuwekeza mashambani.

92038617915f6ea5908e55aea3a92a3f.jpg

Heka 6 za cabbage, drip irrigation.

Natengeneza chakula changu mwenyewe cha kuku, ambapo karibu 50% ya malighafi nazalisha mwenyewe kutoka kwenye mashamba yangu. Msibu huu, umekua wa neema sana, nina heka 48 za mahindi na 15 za mihogo, zote zikiwa miono.

b740178ed054a76287845949282d7ba7.jpg
Shamba langu la mahindi

Hapa kati vitu vingi sana sana sana vimetokea - nimefata tubiashara twingi twingi twa kunisogeza, nimepanda, nimeshuka, kusumbuana na mabenki, kuzurura ofisi za watu nk nk... but all I can say is 'the journey has been so boring & interesting at the same time'.

Kwasasa pia nina shares 25% kwenye kampuni ya technology niseme ICT. Ambapo naweza sema nimekuapo tangu wakati ikiwa bado ipo kwenye ideation phase mpk sasa kdg kuna mwanga unaonekana.

Nipo kwenye mchakato pia kua ktk kampuni yangu ya 3, a sort of partnership to be exact. Hii yote ni katika jitihada zangu za kutimiza malengo niliyojiwekea ya kuwa na vyanzo vya pesa kutoka makampuni 5 tofauti kabla sijatimiza miaka 25.

Mafanikio

Kusimama ktk ujasiriamali hadi leo hasa kwa nchi km TZ si jambo dogo, ni mafanikio makubwa sana, achilia mbali kukuza biashara from scratch.

Lkn nimeweza kutambulika kitaifa na kimataifa.
Ni ngumu sana kujiita mfanyabiashara makini kama TPSF hawakufahamu.

7ff02d5ceae13d2a0626d044f4e44a30.jpg
Nikiwa na mkurugenzi wa TPSF Dr. Simbeye

Nimepata awards 4 za kimataifa ktk biashara kutoka organisations mbali mbali ikiwemo Mastercard foundation.

f459cde9f8fbc5d7eb822423caf12b52.jpg
moja kati ya award niliyopata mwaka jana.

Nimekua featured kwenye media stations nyingi sana kitaifa na kimataifa. Mfano:
Forbes, CNN Africa, BBC World Service (outlook), BBC Africa, How we made it in Africa, Africa Successive Stories, The incubators Africa, SABC, Venture Africa, African Business Magazine nk nk. Nimefanya interviews nyingi sana zingine hata sikumbuki.

Nimepata fursa ya kualikwa kuzungumza ama kuattend conferences kubwa as an entrepreneur. Mfano mwaka jana nilizungumza kwenye conference kubwa sn duniani huko Washington DC na nikaalikwa VIP experience katika TEDx Michigan. Hapa Bongo pia nimeongea kwenye conference za kuandaa sera za kilimo mwaka 2016 na mwaka huu pia. Pia nimealikwa kwenye talks hizi za uhamasishaji mara kadhaa.

Pia mwaka jana nilialikwa kwenye conference kubwa sana ya kilimo hapo Nairobi, ambapo 1 ya wageni rasmi alikuepo Bill Gates. Hii ilikua mara yangu ya kwanza kumwamkia Dr. J. Kikwete in person.

0487861fa588f55648a9283c24e0a50f.jpg

Tangu nimeanza biashara nimezunguka nchi nyingi sana. Kitu kizuri zaidi ktk kutembea ni kukutana na watu, watu wa faida kama My business mentor Vusi Thembekwayo, Alex Okosi (CEO wa MTV Afriva), Prof. Thom Jayne, Richard Maponya, Chimamanda Ngozi, Ahmed Ahmad Alhendawi (UN secretary general's envoy on youth), Mo Dewji, Dr. Strive Masiyiwa (CEO Econet), Acha Leke (CEO McKinsey Afr), Dr. Fred Swaniker, Agnes Kalibata... hii list ni ndefu sana, sitaki nikuchoshe.

Mwisho

Katika kipindi hiki ambacho rate ya graduates wanaoingia mtaani ni kubwa kuliko uwezo wa serikali wa kuajiri, nahisi ujasiriamali ndio njia rahisi ya mtu kuingiza mkono kinywani, na kuacha kutegemea wazazi. Pia kuna ndugu zng wale 10,000 - kutokua na cheti si mwisho wako wa maisha.

Sasa nimeona ni jambo la kheri kama nitashare na wewe chochote ninachokifahamu kuhusu biashara. Pia naamini humu JF kuna watu wa kila calibre, so kwa kitu ambacho sitaweza kutoa ufafanuzi makini nakaribisha watu wengine watoe mawazo yao.

Nafahamu JF kuna watu wanaonifahamu either kwa kuniona/kunisoma kwa media ama kumeet in person, naomba ufiche identity yangu kama mimi nilivyoamua kuificha. Ni suala la kuheshimiana tu. The goal is to be successful not to be famous.

Karibuni sana. Nitajitahidi kujibu maswali yote kadri niwezavyo.

Salute!!

Muhimu
Sitoi mawasiliano, na wala sitojibu P.M
 
Mkuu ONTARIO hongera sana, kwa kututia moyo wajasilia mali tarajiwa.

Hivi mkuu nina swali: Je, kwa mtu ali ajiliwa anawezaje kufanya haya yote ili hali

bado anatumikia kibarua chake, maana hapo wengi ndo huwa tuna kwama,

share nasi maujanja ya kufanya.

Il hizo picha watu wana weza kukujua kirahisi kupitia....be very keen

next time dont do the same if you want to hide ur identity as u did.
 
Hilo shamba darasa nimelipenda! Uko vizur!

Jiandae maswali sasa kutoka kwa wakulima Wa kuku!

Wanakuja

Ila mm nisaidie tu unatumbia mbinu gani kuendesha mradi mkubwa kama huu,

Sababu wengi huanzisha nakuishia kufiriska tu!

Unasimamiaje, unaajir aina gani ya vibarua, utawala wake ukoje?
 
Mkuu @ONTARIO hongera sana, kwa kututia moyo wajasilia mali tarajiwa.

Hivi mkuu nina swali: Je, kwa mtu ali ajiliwa anawezaje kufanya haya yote ili hali

bado anatumikia kibarua chake, maana hapo wengi ndo huwa tuna kwama,

share nasi maujanja ya kufanya.

Il hizo picha watu wana weza kukujua kirahisi kupitia....be very keen

next time dont do the same if you want to hide ur identity as u did.
Kuna msemo wazungu wanasema "No one is busy, it's just a matter of priorities".

Niseme tu wazi, kuRun biashara ukiwa umeajiriwa ni changamoto kubwa sana sana. Unajua biashara yoyote inakuja na risks nyingi, na unapokua mbali na biashara yako, basi unaongeza risk juu ya risk ambazo hauzimanage wewe kama wewe. Mimi nikiwa nasoma chuo ilikua rahisi, as you know elimu yetu chuo haiko tight sana, inakupa muda mwingi wa kua free... hata usipoattend lectures mchana usiku unaeza kesha na ukawa hauna utofauti na aliyeingia pindi.

Changamoto ilikuja kipindi cha field (sisi tunaita Practical training). But ilikua rahisi kudeal na hii situation, na inaweza kuwork hata kwako.

**Kuwa muwazi.
Kama mkataba wako unakuruhusu kumiliki biashara nje ya ofisi, basi usiwafiche waajiriwa wenzio, boss wako nk. Hii itakupa wewe advantage 1, endapo utakua na dharura basi wenzio hapo ofisini hawatakuwa na maswali mengi ya utata utata, so itakufanya ww uwe usijifeel insecured. Kama Boss wako ni mwelewa itakua rahisi zaidi kwako.

**Strong team.
Hapa ndio inabidi uweke nguvu nyingi zaidi. Kuwa na team makini kwenye biashara yako kwa kiasi fulani itaweza kufeel ile gap ya wewe kutokuwepo. Team ambayo kila mtu yupo accountable, integrity ya hali ya juu na watu wanaothamini unachofanya. Pia unaweza kuwapa motisha kwa kuwaahidi equity ktk kampuni. Mfn kuwaambia, kama biashara itatengeneza faida ya mil 10 kwa mwezi, basi nitawapa 20% kama bonus. Hii inawapa morale ya kupiga mzigo haswa.
 
wapi nitapata mashamba ya kukodi ,eneo lenye rutuba na hali ya hewa nzuri hapa tzania?
all in all hongera sana dogo
Depends na wapi ulipo, wapi ni karibu kutoka makazi yako ya kudumu.

Mimi nimekodi hekari 70 bonde la ruvu, ambapo nalima mpunga, mahindi, bustani (bamia, nyanya, mboga mboga, biringanya nk). Huku mashamba bei average ni 100,000 kwa mwaka. Rutuba si ya kutilia mashaka, wazaramu hawana muda kbs na kikimo.

Changamoto.
Hakuna kilimo kipindi kama hiki cha mvua, mashamba yote yanajaa maji kutoka mtoni, ni kama floods tuseme.

Hakuna maafisa wa kilimo, so itabidi uwawele wewe mwenyewe, mimi hua nachukua wataalamu wa Balton.

Hakuna wafanyakazi... Mimi si mbaguzi, lkn kiukweli watu wa pwani ni wazito sana, hawataki kazi kbs, wao ni Vigodoro, ngoma, uzinzi na maneno. So wafanyakazo mpk uwatoe mkoani huko.
 
Laki moja ni heka au ni kiasi gani mkuu.

Asante kwa ushauri
 
How do I grow from here bro? Give me your contacts or email please!
Boss!! This is huge. Hongera sana.

Lkn swali lako liko too general mkuu. Kuna aina nyingi ya growth hasa kwenye biashara, mfano:-

Kupenya kwenye soko - ama market penetration.

Kuteka soko jipya.

Kupanua uzalishaji wa bidhaa.

Kudiversify kutoka kwenye product 1 mpk kwenye product ingine.

Pia kuna acquisition.

Sasa sijui mkuu unahitaji growth ipi.
 
Hilo shamba darasa nimelipenda! Uko vizur!
Jiandae maswali sasa kutoka kwa wakulima Wa kuku!
Wanakuja
Ila mm nisaidie tu unatumbia mbinu gani kuendesha mradi mkubwa kama huu,
Sababu wengi huanzisha nakuishia kufiriska tu!
Unasimamiaje, unaajir aina gani ya vibarua, utawala wake ukoje?

Hakuna biashara kubwa boss, ni perception ya mtu na mtu. Yani sawa na huu mfn, dadangu Miss Natafuta hapa kaniita Dogo, lkn sehemu nyingine nikienda naamkiwa. Hapa unaona biashar ni kubwa lkn mm ndio kwanza naona nacheza makida.

Iko hivi, biashara ambayo iko imara ni ile yenye 'strong foundation'... na kutengeneza foundation imara inabidi biashara uanze nayo chini, huku unagrow mdogo mdogo, hapo kati utajifunza kila kitu kuhusu hiyo biashara, na kadri inavyokua na wewe pia unakua. Ni sawa na kusoma, mtu haanzi kusoma form 1 - lkn mtoto ambae hajafika form 1 anaona wale ambao wapo form 1 ni magenius ama god fathers. unaanza la kwanza pole pole hadi ufike chuo. Same applies to business.
 
Ahahaaa sijakuita dogo kwa ubaya kwamba biashara ndogo au nini. I mean wewe kwangu ni mdogo young bro ila heshima ipo.
 
Back
Top Bottom