Ushuhuda: Biashara ya mchele ni ngumu mno!

Optimists

JF-Expert Member
Oct 17, 2021
278
686
Kijana wenu baada ya kumaliza chuo nikaona nijimix kwenye harakati za maisha nipo Dar es Salaaam japo Nina mda mfupi sana hapa.

Nimezunguka masoko yote hapa dsm kuanzia mabibo mpaka mbagala nilikuja na idea nyingine kwa sababu mtaji sikua nao mkubwa nikashindwa kwa sababu ilihitajika sehemu ya kukodi meza kununua mizani so nikashindwa nikaona nijiingize kwenye issue zingine.

Nilifanikiwa kupita tandale Sokoni kuna soko kubwa linajengwa. kwa nje kuna wafanyabiashara weengi sana nikaanza kufanya research kuhusu biashara ya Mchele kwamba nautoa Mbeya then nawapa madalali wananiuzia, kwa vile niliona sihitaji kutafuta eneo la kazi wala mizani ngoja nianze kufanya hizo issue za kuuza Mchele.

Awali ya yote nilienda pale mwananyamala Sokoni nikakutana na wafanyabiashara wakubwa wa Mchele pale wakaanza kuniambia mwenyewe pale kila kilo waliochukulia mbeya wanapata faida tsh 30_50 yaani anauchukua mbeya kwa 1100 kila kilo kufika Sokoni anauza 1250/1300 akiondoa gharama zake zoote anapata faida hiyo (sema hao wana mitaji mikubwa saana).

Turudi tandale sokoni.

Mimi kwa sababu sikua na mtaji Mkubwa nilikua na around laki 7 nikajitosa kwenda kununua Mchele mzuri sio super saana ila ni mzuri.
Nilichukua mbeya kwa 1300 nikachukua kama kilo 500 total inakua ni 650,000 ukiondoa na gharama zoote na usafiri unajikuta umetumia laki saba na ishirini (720k).

Kufika Sokoni nilitaka niuze kwa 1750@ kilo ili nirudishe gharama zangu lakini naona watu wengi wanahitaji kwa 1600-1650 na mwingine anakwambia umuuzie kwa 1300/1400.

Changamoto nyingine unaweza shusha mzigo Mkubwa kama gunia 30 ukawa unauza 1300 kwa kilo, kesho yake anakuja mwingine anashusha Mchele kama wako anauza 1000/1100 kwa kilo inakua changamoto.

IMG-20211101-WA0029.jpg


Nilichogundua kwenye hii biashara wafanyabiashara wengi ambao wanauza wenyewe wengi wanachanganya mzigo anachukua Mchele super then anachanganya na Mchele mbaya kwa macho mteja hawezi kugundua kwa haraka.

Pia hii biashara kama unataka uone faida yake ni basi inafaa uwe na mtaji Mkubwa sana la sivyo wakuu mambo yatakua ni mazito sana..

Ombi la mwisho wakuu, huo Mchele wangu kwa atakae hitaji anicheck whatsap au normal text kwa namba hii 0757590836 free delivery nitakuletetea popote pale nataka nirudishe gharama yangu nirudi kijijini nikalime.
 
Kijana wenu baada ya kumaliza chuo nikaona nijimix kwenye harakati za maisha nipo dar es salaaam japo Nina mda mfupi sana hapa.
Pole sana mkuu!!hiyo biashara ina hitaji uzoefu mkubwa sana!!mala ya kwanza napeleka DRC, nilikuwa na kama tani 30!!kidogo niukimbie mzigo, kwani fitina niliyokutana nayo kutoka kwa wabongo wenzangu, uchanganye na lugha ya lingala na French, zinazozungumzwa huko, ilikuwa balaa, huku faranga, kule dola!!

!utambue dola halali/fake!!ila nilipambana hadi nikatoboa!!siku ya kwanza niliuza kama faranga milioni 2, kuzibeba kwenye begi la mgongoni hadi bega linauma, kuzihesabu mate yalikauka, nikatafuta bakuli la maji ili kuhesabu.
 
Biashara rahisi kwenye makaratasi tu lakini ukifika field ndo unaona sasa moto wenyewe. Niliwahi kujitosa kwenye biashara ya mbao milioni 5 kweupe zikayeya ila baadaye nikapata watu wazuri wakongwe wa hiyo biashara wakanielekeza mambo ya muhimu sana ndo kidogo nikapata kaunafuu na baadaye nikafanya vizuri. Hakikisha hapo unaondoka na mafunzo yatakayokusaidia huko unakoenda.

Hata kwenye kilimo usifikiri mambo ni rahisi kihivyo. Ongea na watu walioko huko utapata wenye roho njema watakupa ABC za hilo zao unalotaka kulima. Kwa umri huo ukiendelea hivi kutoboa is only a matter of time...future $ millionaire
 
Imekuchukua muda gani tangu kuanza biashara hadi kukata tamaa!?

Unadhani kuna biashara ambayo ni rahisi kwamba utaanza leo kesho uone faida?

Kwenye kuanza biashara inatakiwa uvumilivu, kuna changamoto huwa hazikwepeki hasa kwa biashara mpya.

Kutokujua sehemu ya kuchukua mzigo, unapataje wateja na unafanyaje ili mteja atayenunua leo na kesho aje, huchangia ugumu wa biashara mwanzo.

NAKUSHAURI chagua biashara Moja na upambane nayo iwe jua iwe mvua.

Hata hao unawaona Wana mitaji mikubwa na wanapata faida walishapita hiyo stage ambayo wewe upo wakavumilia ndio unaona wapo hapo walipo.

MWISHO asije kukudanganya mtu kuwa kuna biashara rahisi, biashara ni rahisi ikiwa kwa mwenzio, kinachoonesha urahisi wa biashara ni uvumilivu, uzoefu na ubunifu mpya kila kukicha.

La SIVYO utakuwa mtu wa kuanza biashara mpya na kuacha
 
Mimi nipo mwananyamala kwenye biashara za nafaka ila sio mchele ni mahindi mtama kunde na vitu kama hivyo.... kuhusu mchele wewe umejichanganya kwenda mbeya kununua mchele uje umuuzie mtu ili na yeye auze dukani kwake... kwasabab mimi nipo hapa sokoni najua jinsi biashara hiyo inavyoenda...

Fanya hivii tafuta ubao sokoni mwananyamala halafu uuze mchele wako wewe mwenyewe ukimaliza unaenda tena mbeya pale unamuacha kijana... sio kama unavyofanya wewe ila mtaji wako mdogo huwezi biashara hii ya mchele ungetakiwa uwe angalau milioni 20 ... fanya hivi nenda dodoma kanunue mtama kwa laki 7 yako utapata gunia 10 za mtama niletee mimi nitanunua
 
mimi nipo mwananyamala kwenye biashara za nafaka ila sio mchele ni mahindi mtama kunde na vitu kama hivyo.... kuhusu mchele wewe umejichanganya kwenda mbeya kununua mchele uje umuuzie mtu ili na yeye auze dukani kwake... kwasabab mimi nipo hapa sokoni najua jinsi biashara hiyo inavyoenda... fanya hivii tafuta ubao sokoni mwananyamala halafu uuze mchele wako wewe mwenyewe ukimaliza unaenda tena mbeya pale unamuacha kijana... sio kama unavyofanya wewe ila mtaji wako mdogo huwezi biashara hii ya mchele ungetakiwa uwe angalau milioni 20 ... fanya hivi nenda dodoma kanunue mtama kwa laki 7 yako utapata gunia 10 za mtama niletee mimi nitanunua
Mkuu kama hutojali naomba mawasiliano yako au nikucheck DM mzigo wangu huu wa Mchele ukiisha nikafate mtama. Leo nimeshinda hapo Mwananyamala kuanzia asubuhi mpaka jioni gunia zangu 5 zilishushwa hapo wakawa wananiambia kwa mtaji wangu hii biashara itanishinda na nitaona ugumu wake, wakanishauri nijaribu kwenye mtama au kunde, choroko pia alinambia Maharage japo mtaji wake ni Mkubwa.

Niliulizia meza hapo Sokoni gharama yake ni kubwa Mara mbili ya mtaji wangu Kesho Mimi nitakua hapo nione sample mzuri inayohitajika Sokoni ili weekend hii nikatafute mtama kiongozi.
 
Back
Top Bottom