Ushosti kwenye pesa unanishinda jamani, ushauri tafadhali

urafiki ni mgumu,na inahitaji kuelewana kweli kweli,nikimaanisha kila mtu kutambua nafasi na nini kinafanyika...
Rafiki wa dizaini hiyo...hmmm hebu mwambie tu ukweli kumchunia sio suluhu..itakuja tokea ishu nyingine akarudia...
JAPO:kuwa tayari na upokeaji anaweza akanuna kuhisi umemsema au akakubaliana na taarifa.Urafiki wa wanawake ni mgumu sana.
 
Una mashosti wangapi? Kama unao kati ya 3-5 na unaendelea na hako katabia nakuhakikishia ndani ya miezi 3 unafunga fremu. Biashara ni principle hata kama una duka nyumbani halafu kila siku unachota mafuta ya kupikia, mara sabuni, utajimaliza.
 
kwenye biashara hakuna ushosti wala undugu, hao kaa nao mbali watakufilisi
 
Ushost na hela haviendi kabisa naweza kuwa bubu...
Huwa nikianza ushosti na mtu mashart yangu cost sharing.... kazi biashara haikuhusu na uheshimu.... mimi sichelewi kumpa makavu akasonga mbele na maisha yake..... kama unajua kutumia kutoa pia ujue

Eti mchagga akwachie senti zake? hapana.
 
Pole sana. Ili kuweka amani, usingemdai sasa. Umeshamchunia atajielewa baadae, ila kwenye document zako muandikie deni la balance. Siku akirudi kukopa muambie huwezi kukopa kwa sababu unadaiwa hapa, lipa deni kwanza. Atakimbia mwenyewe na utaepuka drama za uanawake.

tambua kitu kimoja, kuna rafiki hafai kwenye mambo ya fedha lakini ukihitaji msaada ama ushauri wa mengine anakufaa. Usiunguze madaraja.
 
weka kibao eneo la biashara kuwa 1
1wewe ni rafiki yangu ni sawa lakini biashara yangu haikutambui
2ningekukopesha lakini naogopa kukudai
hivi viujumbe vinakaaga kama utani lakini muhusika anapata ujumbe kidzain
 
Ni tofauti ya bei gani nimlipie huyo shosti wako?kisha umwambie kuna kaka amekulipia deni lako ili urafiki wenu uendelee
 
Ni tofauti ya bei gani nimlipie huyo shosti wako?kisha umwambie kuna kaka amekulipia deni lako ili urafiki wenu uendelee

Urafiki na mtu wa hivi si wa kubembeleza... huyu akinyimwa tu kitu anatangaza kila mahal...
 
Kama mtu ni rafiki yangu kama ulivyodescribe hapo, siwezi na haitakiwi kumkwamisha katika mipango yake ya maisha. Rafiki akianguka tena rafiki wa karibu hivi naamini na mimi nitakuwa nimeanguka pia.

Jaribu kumsemesha kama bado unataka urafiki uendelee ukiona anakudiss unaendelea na mambo yako.

Hapa natunga sheria, siku nikimfungukia mweh! Nahisi urafiki utaisha...
 
Pole sana. Ili kuweka amani, usingemdai sasa. Umeshamchunia atajielewa baadae, ila kwenye document zako muandikie deni la balance. Siku akirudi kukopa muambie huwezi kukopa kwa sababu unadaiwa hapa, lipa deni kwanza. Atakimbia mwenyewe na utaepuka drama za uanawake.

tambua kitu kimoja, kuna rafiki hafai kwenye mambo ya fedha lakini ukihitaji msaada ama ushauri wa mengine anakufaa. Usiunguze madaraja.

This is the best contribution to the post, kwa werevu.
 
pole sana ndo watanzania wengi walivyo hawapendi kuona mafanikio ya rafiki

two weeks hamsemeshani messege sent n delivered.ushoga wa hivi haufai bora uachane nae tuu

na sio lazima kuwa na ushoga
 
Shoga unajiuliza ufanyaje????

Ni kwamba akija kwako mwambie hujapenda alichokifanya. Na kwa vile unau-value ushosti wenu asichukue tena kitu kwa mkopo kwako.

Baada ya hapo muepuke. Rafiki wa kweli hamfanyii hayo rafikie. Na wala hathubutu kufanya lolote kumrudisha nyuma.....
 
Biashara na ushoti hauendi kAbisa atafilisi biashara anataka kitu aje na hela hataki mlie wa mbuzi bila hvo mwisho wa siku mgombane anza ku condition
Biashara na ushost au mapenzi utafilisika,kuna jamaa yangu ana kiminsupermarket kamtongoza mdada kamlamba dah!!ikawa balaa anakija afanya shopping halipi anamwambia kijana muuza bili atalipa mhusika,jamaa kavaa sura ya kazi kampa makavu na love ikapotea.
 
Pole sana my boss na bila shaka umejifunza kitu kama unataka biashara yako iendelee na kudumu.
Huna sababu ya kumnyamazia we mpigie simu umsalimie tuu.......
Kwanza nilitegemea kwakuwa hakulipa cash alitakiwa kulipa zaidi au kulipa kwa faida lakini hakuna jinsi maana kuna sehemu ulisha kosea.

Kuna maduka ukiingia tuu unakutana na maneno haya Mkopo amesafiri, hapa yupo cash tuu nimegundua haya maneno yana maana sana hata rafiki akiyasoma ana heshimu biashara yako, lakini si maanishi ukayabandike haya bali wewe ni kuweka sheria na kwenda na principle za biashara.mfano mkopo lazima uwe na riba lakini rafiki yako angeweza kulipa kiasi ambacho utakuwa umeingiza faida na si kulipa bei za kununulia.

Marafiki na Ndugu muda mwingine ndio huwa chanzo cha kufa au kudumaza biashara ni vyema ukaweka missingi na kanuni za biashara yako kwa mfano mtu atakaye kuja kuchukua kwa mkopo anatakiwa kulipa zaidi ya bei ya kawaida maana pesa itachelewa na wanatakiwa wajue hayo.

Kwa sasa kataa kukopesha.
 
Huo ni mchezo m-baya sana haiwezekani asikuulize bei siku ile ya kwanza atake kulilipa apunguze sio vizuri biashara haina undugu wa urafiki mweleze wacha kumuogopa si ni rafiki yako woga wa nini sasa??
 
Huo ni mchezo m-baya sana haiwezekani asikuulize bei siku ile ya kwanza atake kulilipa apunguze sio vizuri biashara haina undugu wa urafiki mweleze wacha kumuogopa si ni rafiki yako woga wa nini sasa??
ni weeewe?
 
Back
Top Bottom