Ushosti kwenye pesa unanishinda jamani, ushauri tafadhali

Ushosti kwenye pesa unanishinda jamani, ushauri tafadhali

Asalaam Aleikum mabibi na mabwana jukwaani hapa....

Eeh bana nina shosti angu ambaye tunasaidiana kwenye shida na raha, sasa shosti huyu naona anaelekea kubaya.

Juzi kati alikuja kwenye kijibiashara changu akachagua vitu, kisha akanambia ataniletea pesa baada ya muda fulani. Baada ya huo muda kupita nikamkumbusha akaniuliza bei kwa mara nyingine nikamueleza. Dah, wacha anigeuke. "Ooooh mie huwezi kuniuzia bei hiyo" mara "Mimi na wewe tumetoka mbali, lazima kuwe na tofauti kati yangu na wengine"

Wadau hivi ushosti na biashara vinaendana kweli?? Hata kama huwa ananisaidia katika mambo mbalimbali ndio alipize kwenye biashara?? Mbona hata mie huwa namsaidia lakini silipizi???


Kilichofatia nilipokea pesa aliyonipa lakini ni kama amenirudishia tu pesa niliyonunulia mzigo bila faida.

Kiukweli roho inaniuma mpaka leo, sijamsemesha na yeye hajanisemesha. Ni wiki mbili sasa zimepita...Sijui nifanyeje???

Ramadhani Kareem....

Biashara na urafiki wapi na wapi? Hayo mambo ya wapenda dezo dezo. Mpe ukweli ili uwe huru !
 
Nenda kachukue TV kwake kulipa sehemu ya hela iliobakia, akikuuliza mwambie nyie ni mashosti asikasirike
 
Mapenz hayooo! kwny biashara, mpe live kama vp ipotezee huyo hafai kuwa rafk coz rfk ck zote hawez ku2let down
 
pole best...watu wengine sijui wakoje mxyuuuuuuu
ngoja ninyamaze tu mie
 
pole dada,,,,,,,, ,,
Urafiki kwenye biashara hautakiwi next time kuwa serious unapofanya biashara na rafiki........
Anapokuja hapo dukani muweke wazi ni bora biashara ikue na urafiki ufe for good
 
Ulivyokaa kimya yawezekana ameamini kuwa kwake utandelea kumuuzia kwa punguzo kubwa kuanzia hapo.
 
Rafikii tu mi nilidhania mama yakoo tupa kulwe
 
Nenda kachukue TV kwake kulipa sehemu ya hela iliobakia, akikuuliza mwambie nyie ni mashosti asikasirike

Mkuu TV kabisa??? Hauko serious, by the way namlia time. Soon nitamfungukia kama ni ushosti uishe aisee!!
 
Hlafu hicho kitu kwa wanawake ndo kina tokeaga maana wanaume hawana hizo, yee atakupunguzia mpaka pale faida yake ya mwisho. Kama umekubali kuichukua basi. Sasa huyo ulishindwa kumwambia ukweli kwa bei hiyo hata pesa ya kununua mzigo hajaifikisha. Ukweli unasaidia sana hata kwenye urafiki.
Take it as lesson next time kitu kama hicho kisitokee, kwasababu ugonjwa mkubwa wa biashara kufa ni kushindwa kutofautisha biashara na mwenye nayo, that your business should be a separate person "The business entity concept" kwamba hata wewe ukichukua pesa unakuwa umeikopa biashara yako.
 
Pole sana charminglady ukitaka kuheshimiana na ndugu au rafiki msiingiliane kwenye mambo ya pesa unless muwe mmeiva haswaa na linapokuja swala hilo undugu na urafiki unakaa pembeni,shost kitu gani hata uhubby na uwife kwenye swala la pesa na biashara huwa linakaa pembeni.

Tuliza moyo na hasira ishuke kisha mfungukie ongea naye kiroho safi mwambie hujapenda hiyo tabia,sawa yeye ni best lakini ajue kuwa kuna kodi unalipa ya chumba mpaka serikali,mzigo huo mpka unafika hapo ni pesa,wewe kukaa hapo kila siku ni pesa,na wewe hapo hapo ule na ufanye majukumu mengine ni pesa je hiyo biashara itaendelea kweli? mfungukie tu mama ili upate amani ya moyo.
 
Last edited by a moderator:
Sijawahi kulipwa deni aseeeh!!!!!!!!

ukipata mbinu uninong'oneze na mimi
 
Mfungukie tu mwambie kitendo alicho kifanya hakijakufurahisha na kinadumaza biashara,kukaa kimya sio suruhisho anaweza rudia tena.
 
Back
Top Bottom