Ushirikina: watoto wapotea kimaajabu Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushirikina: watoto wapotea kimaajabu Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bilionea Asigwa, Sep 23, 2012.

 1. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  SHULE ya Msingi Bokorani, Mtoni-Mtongani, wilayani Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni imekumbwa na matukio ya ajabu ya kupotea wanafunzi wanapotoka shule katika mazingira ya kutatanisha.

  Kwa kipindi cha wiki mbili katika mwezi mmoja, imeripotiwa kupotea kwa wanafunzi watatu wa madarasa tofauti, wote wa kike na matukio hayo yamehusishwa na masuala ya kishirikina.

  Tukio la kwanza lilitokea Juni 19 mwaka huu baada ya mwanafunzi wa darasa la kwanza Zawia Mohammed (7) (pichani) kupotea alipotoka shule na mpaka mwishoni mwa wiki, hakuwa amepatikana.

  Taarifa zinaeleza kuwa, katika kipindi cha wiki mbili baada ya Zawia kupotea, wanafunzi wengine wa kike wawili ambao majina yao hayakuweza kupatikana, wa darasa la tano na la sita, walipotea katika mazingira kama hayo.

  Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdallah Mshana alikiri kutokea katika shule yake mwezi Juni na kubainisha kuwa wanafunzi wawili kati ya hao watatu, walipatikana.

  Alisema tukio la kwanza lilimhusu mwanafunzi wa darasa la kwanza, Zawia Mohamed mwenye umri wa miaka saba, na aliripotiwa kupotea Juni 19 mwaka huu na taarifa ilifikishwa kwake Juni 22, "Siku ya tukio nilikuwa kwenye mkutano Halmashauri, siku moja baadaye walimu wakanieleza kuhusu tukio hilo na kesho yake baba wa mtoto alikuja kutoa taarifa na kuuliza kama amepatikana," alisema Mwalimu Mshana.

  Mshana alisema taarifa alizopewa na baba wa mtoto huyo zinadai kuwa, alipotoka shule, alikutana na mtu nje ya geti la shule karibu na barabara kuu ya Kilwa na mtu huyo alimvusha barabara na hajaonekana tena, "Tulichukua hatua sisi na wazazi wake kwenda Ofisi za Serikali za Mitaa kutoa taarifa na tukiwa pale uongozi wa Serikali ulipiga simu Polisi Kituo kidogo cha Mtongani, juhudi za kumtafuta bado zinaendelea".

  Katika hali ya kushangaa, Mshana alisema katika kipindi cha wiki mbili baada ya Zawia kupotea, walipotea wanafunzi wawili wa kike na baada ya kutafutwa kwa siku kadhaa, walipatikana isipokuwa Zawia.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime alithibitisha kupotea kwa mtoto huyo na kueleza kuwa taarifa ilifika Polisi Juni 20 mwaka huu na wanaendelea kumtafuta, "Ni kweli mtoto huyo alipotea na tunaomba wazazi waendelee kuwasiliana na sisi ," alisema.

  Source:HABARI LEO
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Sasa hapo ushirikina uko wapi?, kwamba kuna mtu alimvusha brbr na mtoto hakuonekana tena?!, kumbukeni kuwa biashara ya kuchukua watoto na kuwafanya kafara inaendelea.
   
 3. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,963
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Pelekeni shauri hilo Kanisa la Ufufuo na Uzima Kawe.
   
 4. papason

  papason JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Huku Kanda ya ziwa kwa kiasi kikubwa tumelikomesha tatizo hilo kwa kuwapiga vibiriti na panga 'watuhumiwa'
   
 5. Zuia Sayayi

  Zuia Sayayi JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 834
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkuu acha uongo mbona 2nao huku
  msitun
  simiyu
  na leo tuna mla nyama yule mtoto wa pili kupote!
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  nijuavyo mimi mkoani simiyu watoto hupelekwa kuchinjwa kwenye machimbo ili kupata madini mengi.
   
 7. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,118
  Likes Received: 1,746
  Trophy Points: 280
  Tutasikia mengi,enhe lete habari!
   
 8. m

  mkupuo JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Hiyo pcha ya Zawia mohammed mbona siioni katika uzi wako kama ulivyotujuza?Kuwa makini unapoposti uzi muhimu kama huo.Ningeiona picha yake ningesaidia kumtafuta.
   
Loading...