Ushirikina upo.

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
625
Napenda tuu kwaasa ndugu zangu wamtafute MUNGU wa kweli kwani waovu wamezidi hii dunia.
Kuna muda mtu unafikia unajisikia huna Amani na wasiwasi tele kumbe ni matokeo ya kazi ya shetani sasa kuepukana na mitego ya shetani mkabidhi MUNGU maisha yako umuombe akulinde dhidi ya wachawi na washirikina.

Wewe ulie na matatizo katika familia yako, kazini, masomoni na popote pale anza kutatua tatizo lako kwa kuanza na MUNGU kwanza.
Wengi watabisha na kusema nguvu za giza hazipo ili siku mkiyashuhudia ndugu zangu mtajua kwamba wanga wapo na wanafanya kazi.
MUNGU awe nanyi ni vyem kusaidiana kama Yesu alivyo tusihi TUPENDANE.
 


Sishangai sana mkuu, sabb watu wote au karibu aslmia yote ya watu wanaokamatia dini huwa pia wanaamini ktk uchawi.
Haya ndo yale unakuta mtu hasomi afu anasema MUNGU atamsaidia kufaulu Mtihani shuleni [emoji2]
Watu wenye ngozi nyeusi sie tuna ujinga sana, kila kitu ambcho hatukijui tunasingizia UCHAWI [emoji2] Badala ya kuongeza UTAFITI na MAARIFA kukifanyia UCHUNGUZI.
Trust me, Waafrica tungekuwa pekee yetu duniani bhaaasi mpk leo tusingekuwa hata na Baiskeli... Hata UMEME huu tungesema ni UCHAWI. [emoji2]
Maana akili zetu bana hatunaga Utafiti wala kujiuliza," Kwa nn kitu flan kipo hivi na sio vile?" afu kisha kuongeza Utafiti na kujaribu kujua ni kw nn.
(Mwafrica kila ktu ambcho hakijui anasema ni Uchawi)
Hata MTU akiumwa magonjwa ya akili, Waafrica utasikia ,"YULE KAROGWA" [emoji2]
Waafrika hata mtu akifariki utasikia "YULE KAFANYWA MSUKULE au KAFARA".
Hata kwenye soka watu wana imani za ajabuuuu ajabuuuuu Mara sijui wafukie nn mara nini sijui LAKINI WAAFRICA NA TIMU ZETU KUFUNGWA KUPO PALEEE PALEEE!!
Na kuna mtu mpk leo anaamini kuna KUPAA KWA UNGO [emoji2]
Hata INTERNET hii Waafrica tungesema ni UCHAWI [emoji23]
#TypicalAfricanMind
Mwafrica asione tu BUNDI usiku basiiiiii kashapagawaaaaaa.. Wakati BUNDI ni Nocturnal Animal (bird) ambaye huruka na kufanya mawindo yake wakt wa usiku, kama Popo, Karunguyeye etc. (nao huw ni ucku ucku)...
FISI ndo tunamuonea kabisaaaa, Yaani hadithi za Kale zile Watu wakt wa ucku kukaa na Babu kusimulia stori bhaaaasiii ndo tumezifanya UKWELI sasa..
(Pengine si ajab kuna watu wanaamini FISI na SUNGURA walkuw marafiki)[emoji2]
Mwafrica hata Teknolojia ya BUNDUKI tu angesema ni Uchawi mpk leo.
RADI ikipiga tu Mwafrika anasema imetumwa hiyo. (HIVI JE TUNAJUA KUWA KWA WASTANI RADI HUWA INAPIGA KTK USO WA DUNIA KILA SIKU KTK SEHM MBALMBAL ZA DUNIA?)

Uzuri ni kwamba IMANI POTOFU huwa zinaenda zikiisha, Kadri vizazi na vizazi vinavyozidi kwenda.
MFANO:- Sidhani km kuna mtu bado anaogopa kuvaa NGUO NYEKUNDU kwa kuhofia kupigwa RADI.[emoji41]
WAAFRIKA BANA, DAAAH TUMEFANYA NDUGU ZETU ALBINO WAISHI KW WASIWASIIII, MTU ANASHINDWA HATA KUJIONGEZA KUWA KM UKIWA NA KIUNGO (kidole, mkono) CHA ALBINO BASI UTAPATA MALI NA PESA, BASIIIII NDUGU ZETU ALBINO WANGEKUWA NDO AKINA MO DEWJI, BAKHRESA, MUFURUKI, R.MENGI, ROSTAM etc... [emoji2][emoji2]
[emoji2][emoji2] Ndo sabb hata MUNGU kajificha haonekani... Maana "WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA"
Kitu "Intellectual" hakunaga kw Mwafrica, Mwafrica akil yake kila KTU anawaza "Superstition" tu.

HATA ULAYA ZAMANIIIIIII WALKUWAGA BAADHI YAO WANAAMINI KTK UPUUZI HUU WA IMANI POTOFU, MWSHO WA SIKU WAKAONA NI UPOTOFU TU HAKUNA KITU.
#ThisisAfrica
#KwaLeoTuishieHapa

Trust me Waafrika hata Mobile Phones hizi tungesema ni Uchawi [emoji2][emoji2]
Ukiwafata Viongozi wa Kidini kichwa kichwa tu basi utaishi maisha ya Hofu sanaaaa.
Na ukiwafata the so called "waganga" nako utajikuta kila pesa yako inaliwa na hao. Na utakorofshana na wenzio (maana waganga kila mkosi watasema ni jirani au ndugu yako)"
#KufikaTutafikaLakiniTukiwaTumechoka
Ajabu leo hii mtu anaamini kuwa akfanya dawa kwa mke wake afu basi mtu atakayetoka kimapenzi na mkewe huyo, basii atakutwa amenasa [emoji23] AKILI KUMKICHWA, KUNA MATUKIO MENGIIII YA KUTENGENEZA NA WATU WANAINGIA KINGI WAKIDHANI NI KWELI AFU MGANGA ANAKULA PESA ZA MABOYA. [emoji2]
Hata Vita ya MajiMaji ingefanyka Leo, bado kuna watu wangeingia mkenge tu wa kudhani watazuia Risasi kw mbinu za MajiMaji.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…