Ushirikina unavyozorotesha elimu kisiwani Mafia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushirikina unavyozorotesha elimu kisiwani Mafia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 3, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  WASWAHILI husema tembea uone. Nilidhihirisha usemi huu pale nilipokuwa katika kisiwa cha Mafia kilichopo ndani ya bahari ya Hindi hivi karibuni nilipokuwa katika safari zangu za kikazi.Jambo la kushangaza nilipofika eneo hilo nilichukua chumba jirani kabisa na manispaa ya kisiwa hicho,lakini nilipokuwa nakula usiku nilikuta watoto wa kike wa shule wakiwa wanatokea ndani wakiwa wameongozana na watu wazima ambao wanaweza kuwazaa.

  Nilipatwa na mshituko pale nilipoona watu wakiwa wanaona ni mambo ya kawaida kwani hakuna hata aliyeshtuka, lakini nilipojaribu kuulizia nikaambiwa, hiyo ndiyo Mafia kaka.Naweza kusema kwamba jamii yoyote ile inayotawaliwa na imani za kishirikina ni vigumu sana kwake kuendelea na hii inatokana na kwamba kila mtu wa jamii hiyo huogopa kujiendeleza akihofia kupoteza maisha yake au ya jamaa zake.   Hali hii pia inasababisha hata maendeleo yanakosekana kama suala la elimu kwani kila mtu anajitahidi kadri awezavyo kutafuta njia ama ya kujilinda mwenyewe, familia, ukoo au jamaa kwa ujumla ili asilogwe na wenzake. 

Kwa jinsi hiyo nathubutu kusema kuwa kama umefika mahali ukakuta imani za kishirikina zimetawala, basi ujue hakika asilimia kubwa ya jamii hiyo haijaelimika.

  
Mwalimu mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alitamka wazi kuwa kuna mwenzake amehama Mafia kutokana na imani za kishirikina kwani siku moja alikuwa amelala akasikia mtu anabisha hodi alipokwenda kumfungulia anakuta ni mbwa amelala chini .

  “Yule mwalimu inaonekana hakuaga kwao kwani alitokea bara kama mimi, lakini wengi huku tumeaga ndio maana unatuona huku, tunadunda suala la kuona vituko huku ni la kawaida kaka,”anasema
  Anaongeza kuwa kutokana na hali hiyo inaaminika kuwa walimu wengi wanaohamishiwa katika kisiwa hicho wamekuwa wakikimbia wenyewe kutokana na vitendo hivyo vya ushirikina.

  “Mimi mwenyewe kuna kipindi nilikuwa nikilala najikuta naamkia uwanja wa mpira, nikaamua kwenda kuaga kwanza nyumbani kwa sababu kila nikiwasimulia wenzangu walikuwa wakinicheka.

  ‘’Wizara husika (Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tawala za Mikoa wa Serikali za Mitaa ) zinatakiwa kuweka mikakati madhubuti kuwanusuru watoto wanaoonekana kuikosa elimu yao, huku walimu nao wakikataa kuhamishiwa huku kwa kuhofia usalama wa maisha yao,”anasema

  Pia, inaaminika kuwa karibu maeneo mengi yanayoambaa kando kando ya mikusanyiko ya maji mengi kama vile maziwa, mito mikubwa na bahari, yana historia ya kuamini na 
kutegemea ushirikina

  Katika hatua nyingine ya kusikitisha wazazi wamedaiwa kuwatetea watu wanaowapa ujauzito watoto wao kwa kumalizana kifamilia , huku wakitoa vitisho kwa walimu wanaopeleka kesi hizo mahakamani wilayani Mafia.
  Akizungumza wilayani humo katika kongamano lililoandaliwa na shirika la Kimarekani la Action- Aid, ofisa elimu wa wilaya hiyo , Mohamedi Kahundi alisema kuwa hali hiyo imeshazoeleka wilayani hapo kutokana na kujaa kwa imani za kishirikina.

  Anasema kuwa walimu wanashindwa kuwasaidia watoto kuendelea kupata elimu kutokana na kupata mimba kila mwaka na wanaowapa mimba hizo wakiwa wanafahamika na kuwaachwa wakirandaranda tu mitaani.
  Kahundi anaeleza kuwa hadi sasa hivi watoto 35 wanaosoma shule za msingi na sekondari wamepata ujauzito kuanzia mwaka 2008, lakini hakuna jitihada zilizofanikiwa kuwakamata wahusika kutokana na walimu kutishiwa na wazazi wa watoto hao.

  “Kinaschoharibu hapa ni imani za kishirikina kwani watu wanawatishia walimu kuwaroga kwa sababu wamewapeleka kesi polisi za watoto kupatiwa mimba ,sasa badala ya mzazi kutoa ushirikiano wanatoa vitisho tena,”anasema Kahundi

  Akizungumza wilayani hapo katika kongamano lililoandaliwa na Aid, afisa elimu wa wilaya hiyo Mohamedi Kahundi anasema kuwa hali hiyo imeshazoeleka wilayani hapo kutokana na kujaa kwa imani za kishirikina.
  Anasema walimu wanashindwa kuwasaidia watoto kuendelea kupata elimu kutokana na kupata mimba kila mwaka na wanaowapa mimba hizo wakiwa wanafahamika na kuwaachwa wakirandaranda tu mitaani.

  Anasema kwa sasa hivi jumla ya watoto 35 wanaosoma shule za msingi na sekondari wamepata ujauzito kuanzia mwaka 2008 mpaka mwaka huu lakini hakuna jitihada zilizofanikiwa kuwakamata wahusika kutokana na walimu kutishiwa na wazazi wa watoto hao.

  “Kinachoharibu hapa ni imani za kishirikina kwani watu wanawatishia walimu kuwaloga kwa sababu wamewapeleka kesi polisi za watoto kupatiwa mimba ,sasa badala ya mzazi kutoa ushirikiano wanatoa vitisho tena”anasema Kahundi

  Mwalimu mkuu wa shule ya Kilindoni, Mwajuma Likindi anasema kuwa wazazi wanachangia sana watoto wao kupata mimba huku wakiwa tupia lawama walimu hao,akitoa mfano anaeleza kuwa kuna mzazi alimfuata shuleni hapo akimuuliza kuwa amemtuma wapi mototo wake mbona amekutana naye akiwa anaingia nyumba ya wageni?
  Mwalimu huyo alisema alipatwa na mshangao sana kwani mzazi Yule badala ya kumwuliza binti yake anaenda kufanya nini katika nyumba ya wageni anakuja na kumwuliza mwalimu kuwa mbona mwanaye anaingia nyumba za wageni.

  “Yaani mimi nimtume mwanafunzi nyumba ya wageni afuate nini sasa wakati mimi nakemea vitendo vya ngono,”anasema mwalimu Yule.Naye mwalimu mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini anasema kuwa kuna mwanafunzi wa darasa la nne alipewa mimba na rafiki wa baba yake, lakini mzazi wa yule mtoto aliposikia rafiki yake anatafutwa alimwambia atoroke.

  ‘’Nilipoendelea kufuatilia nikatishiwa maisha na wahusika nikaachana nao, lakini mpaka leo ninaumia sana roho hali hii itaendelea mpaka lini, “analalamika mwalimu huyo. Kwa upande wake mratibu wa Action Aid nchini, Jovina Nawenzake anasema kuwa wanaotakiwa kupewa lawama ni wazazi kwani wanakosa muda wa kukaa na watoto wao.

  Anasema kwa wilaya ya Mafia kuwaona wanafunzi wakiingia katika nyumba za wageni ni jambo la kawaida ,huku wazazi wakiwa wanafahamu hayo, lakini wanakosa muda wa kuwaadabisha.

  Mwanasheria wa wilaya hiyo, Simon Rendika anasema kuwa mpaka leo hakuna hata kesi ya mwanafunzi mmoja aliyepewa mimba iliyomalizikia mahakamani kwani zote wazazi wanamalizana kifamilia.Anasema hali hiyo imeshazoeleka Mafia kwa sababu za imani za kishirikina na ndio hasa watoto wanaendelea kufanya uhuni na kuzaa hovyo huku wakisema ni ugumu wa maisha.
   
Loading...